Gazeti la Tanzania Daima laadimika mtaani

Gazeti la Tanzania Daima laadimika mtaani

Status
Not open for further replies.
Kwa wale wakazi wa Tabata Kimanga leo asubuhi kwa wale waliopita St Mary's maeneo ya Hai Bar kulikuwa na kijana mmoja amevaa combat za Chui Chui akielekeza magari baada ya kutokea jam. Yule alikuwa akiwahi magazeti ya Tanzania Daima Tabata Kimanga. Nilijiuliza hawa vijana na kombati zile mara nyingi huvaa wawapo kule kwao leo yupo hivi hivi huku uraiani kumbe ndiyo wanunuzi wa magazeti. Du!!!! hii kali.
 
Acheni kuwahadaa wananchi na kuleta chuki zisizo na msingi wewe umeenda kwa wauza magazeti watano umekosa magazeti una generalize kuwa magazeti yote ya T.daima yamenunuliwa na watu wasiojulikana???? na watu wanakuungamkono bila kufikiria japo kidogo!!!!!!!!!!! Nipe majibu ya haya maswali haya kabla hatujaendeleza siasa chafu humu. 1. Ulipoamka leo kwanini uliwaza kununua gazeti la Tanzania Daima? 2. Ulikua unawaza kununa hilo gazeti mwenyewe hivyo ukaamini kuwa litakuwepo linakusubiri? Unafahamu maana ya hot news na kwamba husababisha watu kukimbilia gazeti husika kwa kiwango kisicho cha kawaida? umesema muuza magazeti alimesema walionunua ni watu wasiojulikana, je huwa anakumbukumbu ya kila anayenunua magazeti kila siku?

Mimi nilipokua naelekea airport majira ya saa 2 asubuhi nimelipata gazeti hilo pale ubungo nikajinyakulia nakala yangu nimefika mwanza nimelikuta kenye kibanda cha magazeti sasa sijui mtu anapataje guts za kusema magazeti yamenunuliwa na usalama wa taifa au ndiyo zile tafiti za kukaa mezani na kukubaliana tuweke takwimu hizi ili kupambana na na taasisi nyingine?

Mwenye kufuatilia vyema akumbuke kipindi gazeti la The citizen la Kenya lilipotoa habari ya utatanishi kuhusu Moi nini kilitokea kama siyo kuliteka gari la magazeti, na kuteka kiwanda cha kuprint magazeti hayo kama majambazi na kucho magazeti yote yaliyokuwa tayari ila kwa uwezo wa kipesa gazeti likaprintiwa nchi jirani siitaji maana sina uhakika!!!!!!! sembuse T. Daima inatoa copy ngapi kwa siku na kuuza ngapi?
 
Hebu tujibu ulipofika Ubungo ukajinyakulia nakala ya gazeti la Tanzania Daima na ulipofika Mwanza ukakuta gazeti hilo kwenye kinda cha kuuza magazeti. Swali kwanini ulikuwa unalifuatilia sana leo na siyo jana???
 
Nadhani mahakama itabaki ya wananchi wenyewe. Mungu ilinde Tanzania na wabariki watu wake wote wajiongoze vyema
 
Acheni kuwahadaa wananchi na kuleta chuki zisizo na msingi wewe umeenda kwa wauza magazeti watano umekosa magazeti una generalize kuwa magazeti yote ya T.daima yamenunuliwa na watu wasiojulikana???? na watu wanakuungamkono bila kufikiria japo kidogo!!!!!!!!!!! Nipe majibu ya haya maswali haya kabla hatujaendeleza siasa chafu humu. 1. Ulipoamka leo kwanini uliwaza kununua gazeti la Tanzania Daima? 2. Ulikua unawaza kununa hilo gazeti mwenyewe hivyo ukaamini kuwa litakuwepo linakusubiri? Unafahamu maana ya hot news na kwamba husababisha watu kukimbilia gazeti husika kwa kiwango kisicho cha kawaida? umesema muuza magazeti alimesema walionunua ni watu wasiojulikana, je huwa anakumbukumbu ya kila anayenunua magazeti kila siku?

Mimi nilipokua naelekea airport majira ya saa 2 asubuhi nimelipata gazeti hilo pale ubungo nikajinyakulia nakala yangu nimefika mwanza nimelikuta kenye kibanda cha magazeti sasa sijui mtu anapataje guts za kusema magazeti yamenunuliwa na usalama wa taifa au ndiyo zile tafiti za kukaa mezani na kukubaliana tuweke takwimu hizi ili kupambana na na taasisi nyingine?

Mwenye kufuatilia vyema akumbuke kipindi gazeti la The citizen la Kenya lilipotoa habari ya utatanishi kuhusu Moi nini kilitokea kama siyo kuliteka gari la magazeti, na kuteka kiwanda cha kuprint magazeti hayo kama majambazi na kucho magazeti yote yaliyokuwa tayari ila kwa uwezo wa kipesa gazeti likaprintiwa nchi jirani siitaji maana sina uhakika!!!!!!! sembuse T. Daima inatoa copy ngapi kwa siku na kuuza ngapi?

mkuu kifupi hili gazeti sio kawaida kuadimika kihivyo,nilipita ubungo maziwa mpaka stand ya mkoa sijapata nakala hata moja ilikuwa sa 4 asubuhi, kuna mdau mmoja (mzito kabwela amesema alienda ofisini kwao na wamemwambia waliishiwa makaratasi ya kuchapishia sina uhakika kama ni kweli au naye ameongea kisiasa! Ulizia k'koo kama lilikuwepo hilo gazeti leo.
 
duh nmeshalisoma aisee kweli lwakatare kukamatwa imekua njia ya ukombozi kwa Watanzania Tanzania Daima wameweka kila kitu waz adi waliokuwa wamejfcha nyuma ya pazia...
 
Wajanja washanitupia link kitambo...thx thou
 
tafuta Mtanzania, Nipashe, habari leo na majira utapata waraka huo?

Asante Mkuu, nimeshaisoma ila pia hapa JF wameshaitoa au? Maana hii issue ni public interest na kwa kuwa imeshawekwa wazi basi JF waiache idumu.
 
aisee,hata mimi nimehangaika kweli kutafuta gazeti la Tanzania Daima hamwezi amini sijaambulia chochote.Lowassa kaanza tena mambo yake nini???ndo michezo yake hii
 
Nakijibu swali moja tu kujuondolea ukwasi! Jana nikisoma bandiko la mzee wangu humu JF,wakili maarafu na shushu la kimataifa,jina unalo) so wakt narudi home kichwani nikawa na mawazo na maswali bila majibu,sasa asbh na mapema wakat naenda kazini nikasema ebu nipate tzdaima nione kama watakuwa wameandika nilichokisoma jana na sikuwaza kununua gazeti jingine tofauti na tzdaima.

Nafika meza ya magezeti jamaa ananiambia gazeti lako leo limeisha mapema kabisa,nikaanza waza mmmh tzdaima leo mapema ivi jmn? Nikaamua kwenda sehemu nyingine huko ndo nikakuta story sasa kuwa kuna watu wamenunua copy zote at once,from there nikaamua kufatilia kwa makini kwa wauzaji wengine tena hadi wa 5 hakuwa na hilo gazeti..................
 
Tutaichapisha kwenye toleo lingine wiki hii hii halafu myanunue yote tena.
 
Ni ajabu kuona CCM wanavyohangaika kuzuia jua la CHADEMA kwa kutumia ungo hivi.
 
wakuu wasalaam?
leo asbh nimeamka nikiwa na wazo moja tu kichwani,la kununua gazeti la T-DAIMA ili nisome madai ya CHADEMA kufichua siri za watu wa usalama kukihujumu chama cha CHADEMA, sasa katika pita pita yangu amini usiamini mpk sasa nimepita sehemu 5 hakuna gazeti la T-daima na madai ya wauzaji wanasema kuna watu wamekuja wakanunua yote,mara wengine"leo mie nimeletewa copy3 tu" wengine copy 5

kama issue kujulikana ishajulikana toka jana,tumeisoma humu JF, sasa ya nini wanausalama wanahaha kununua magazeti mtaani?<sina hakika kama ni usalama> ama wanataka watz wa kawaida wacjui what is going on?

MY TAKE:
CCM TEKELEZENI SERA ZA CHAMA CHA MAPINDUZI WANANCHI TUKO TAYARI KUWAUNGA MKONO.WAACHENI CDM WAFANYE KAZI ZAO KIUFANISI KWANI WANAWAKUMBUSHENI MAJUKUMU YENU KILA MNAPOJISAHAU,TZ NI YETU SOTE,WEWE,MIMI,NA YULE
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetaja majina ya baadhi ya watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikidai kuwa ndio wanaopanga mipango ya kishetani na kisha kuwasingizia watu wengine.
Hatua hiyo inakuja huku Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa chama hicho, Wilfred Lwakatare pamoja na Ludovick Joseph wakikabiliwa na kesi ya ugadi, wakidaiwa kupanga mikakati ya kuteka na kudhuru watu.
Sakata hilo limeibua gumzo hadi bungeni baada ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba kudai kuwa ndiye alipeleka video ya Lwakatare polisi na kukituhumu chama hicho akidai ni cha kigaidi.
Hata hivyo, CHADEMA kupitia kwa viongozi wake wakuu, wamekuwa wakidai kuwa video hiyo imetengenezwa na CCM kwa kushirikiana na vyombo vya dola ili kukidhohofisha chama hicho, na hivyo kuahidi kufichua mpango huo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Makao Makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam, Mjumbe wa Baraza Kuu wa CHADEMA, Mabere Marandu alisema kutokana na njama hizo kuanzia leo ataongoza jopo la mawakili sita wa chama kumtetea Lwakatare.
“Wenzangu wengine katika kesi hii ni Prof. Abdallah Safari, Tundu Lissu, Edson Mbogoro, Peter Kibatara na Nyaronyo Kicheere. Huko mbele tutaongeza mawakili wengine, akiwamo mmoja anayewekwa na familia ya Lwakatare.
Ifuatayo ni taarifa kamili ya Marando ambaye pia ni mwanasheria maarufu nchini na mmoja wa wakongwe wastaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa:
“Leo tumewaita hapa ili kuwaomba mtufikishie ujumbe kwa Watanzania, kwamba nikiwa mwanasheria na mtu ambaye nimepata ujuzi wa kazi za ushushushu, nimefanya uchunguzi matukio haya ya utekaji na utesaji na kugundua mambo mengi mno.
Uchunguzi huu nimeufanya kabla na baada ya kukamatwa kwa Mkurugenzi wetu wa Ulinzi na Usalama, Wilifred Muganyizi Lwakatare, ambaye hivi sasa anashtakiwa mahakamani kwa tuhuma za kupanga ugaidi.
Nimefanya hivyo kwa kuangalia maslahi mapana ya taifa langu na chama changu. Katika uchunguzi wangu huo, nimegundua mambo mengi ikiwamo kuwapo kwa genge la watu ndani ya serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM), wanaopanga mipango hii ya kishetani na kisha kuwasingizia watu wengine.
Angalieni mfano huu: Unaoitwa na polisi na Mwigulu Nchemba “mkanda wa Lwakatare” unadaiwa uliwasilishwa Jeshi la Polisi Desemba mwaka jana.
Lakini jeshi hilo halikumkamata yeyote wala kumhoji, hadi pale Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda alipovamiwa na kuumizwa.
Aidha, Nchemba amedai kumiliki video ile Desemba mwaka jana, lakini rekodi hiyo iliwekwa kwenye mitandao ya kijamii (YouTube na Jamii Forum) baada ya kutekwa kwa Kibanda. Hapa mtu makini anaweza kujiuliza, hiki kimelenga nini?
Kwamba genge hili la kina Nchemba na wenzake, walipanga kumteka Kibanda, wakatimiza lengo lao hilo, baadaye wakaingia kwenye plan B ya kutaka kuihusisha CHADEMA.
Wakamtumia Ludovick Joseph Rwezahula ambaye ni mshtakiwa wa pili katika kesi ya Lwakatare, kufanikisha mkakati wao huu wa kishetani.
Huu ni mchezo mchafu na wa hatari mno ambao kwa vyovyote vile, haupaswi kuvumiliwa.
Kuanzia sasa nimeamua kwa dhati kabisa kukomesha mchezo huu ambao unahatarisha uhai wa taifa letu.
Mnaweza kujiuliza kwanini CHADEMA kimechukua uamuzi huu wa kuweka kundi kubwa la wanasheria katika kesi hii ya Lwakatare. Jibu ni kwamba tumegundua kuwa kesi hii imefunguliwa kwa lengo maalumu la kuidhoofisha CHADEMA na kuinusuru CCM ambayo inakabiliwa na dhahama ya kushindwa katika uchaguzi mkuu ujao kutokana na kushamiri kwa makundi.
Hivyo wameamua kumfungulia kesi Lwakatare, kwa lengo la kutaka kuaminisha umma kuwa CHADEMA ni chama cha magaidi, kinapanga ugaidi na hivyo kichukiwe. Hilo ndilo lengo lao. Basi!
Pili, nitakwenda mahakamani kuwasilisha ombi maalumu la kuomba amri ya mahakama kuagiza makampuni ya simu za mkononi kuwasilisha mahakamani statement za simu za watu kumi (10) ili kusaidia mahakama kutenda haki na jamii kujua ukweli wa mambo haya.
Watu ambao nitaomba mahakama itoe amri ya kuletwa taarifa zao za simu na meseji (sms) ni Naibu Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa nchini (TISS), Jack Zoka, anayetumia simu Na. 255756809535, Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwigulu Lameck Nchemba, anayetumia simu tano zikiwamo 0754 008888, 0757 946223, 0714 008888 na 0787 513446 na Ludovick Joseph Rwezahula ambaye simu zake ni 0715 927100 na 0753 927100.
Mwingine ambaye mawasiliano yake yanahitajika, ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Emmanuel Nchimbi anayetumia simu Na. 0754 003388, Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Mwananchi, Dennis Msacky anayetumia simu mbili; 0655 331010 na 0764 331010 na Sinbad Mwagha, ambaye ni Ofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa, anayetumia simu 0754 006355.
Wengine ni Shaali Ali, Ofisa mwingine wa Usalama wa Taifa anayetumia simu Na. 0716990099, Saumu K. Malungu, mwenye kutumia simu 0719 541 434 na 0789 614 629, simu mbili zinazotumiwa na mtuhumiwa mkuu wa utekaji wa Dk. Steven Ulimboka, Ramadhani Abeid Ighondo ikiwamo 0713 760 473, simu za Ridhiwani Kikwete ambazo ni 0754 566299, 0784 566 299, simu ya Dk. Ulimboka ambayo ni 0713 731 610, pamoja na simu zote tatu za Wilfred Lwakatare, ambazo ni 0786 774697, 0713 237869 na 0758 417169.
Mtu mwingine muhimu nitakayeomba mahakama itoe amri ya kutolewa kwa taarifa zake, ni mwandishi wa habari na mpigapicha wa magazeti ya serikali, Muhidini Issa Michuzi.
Mwandani huyu wa Ikulu, ndiye aliyeandika ujumbe kwa njia ya barua pepe kuipongeza ofisi binafsi ya rais (OBR) na usalama wa taifa kwa kupata video ya Lwakatare.
Pongezi za Michuzi kwa TISS ndizo zinanisukuma kuiomba mahakama kuagiza kupatikana taarifa zake. Michuzi anaipongeza TISS kwa kuibua njama za wahalifu, lakini mimi ninajua TISS ikipata njama za aina hiyo haraka inapeleka ushahidi polisi, lakini huu wa Lwakatare ulipelekwa Youtube, badala ya kwenye vyombo vya sheria.
Maneno ya Michuzi kwamba ni TISS imeibua hiyo video yanathibitisha ushiriki wa TISS kwenye mchezo huo mchafu, na kwamba CHADEMA kinajua kuwa Michuzi alishirikiana na watu wa usalama wa taifa katika kazi hiyo chafu.
Software za video (editing) walizotumia zilitoka kwake. Fedha ya kuandaa hiyo video zilitoka Usalama na Ikulu. Tunajua kuwa wale vijana wa Ada Estate na yule jamaa aliyempelekea kigogo wa Jamii Forum, walilalamika sana kwa mmoja wa wamiliki wa JF.
CHADEMA kinajua kuwa mmoja wa watuhumiwa hawa, Mwigulu Nchemba anafanya mipango na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Vodacom ili kumsaidia kufuta taarifa zake.
Nachukua nafasi hii kuionya kampuni hiyo kuacha kucheza mchezo huo kwa kuwa ni kinyume na sheria za Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA).
Tunahitaji mawasiliano haya kwa kuwa simu za Mwigulu zinaonesha mtuhumiwa huyo akifanya mawasiliano mfululizo na Ludovick, yakiwamo yale ya tarehe 4 Machi 2013. Hii ilikuwa siku moja kabla ya Kibanda kutekwa.
Hawa niliowataja ni watu muhimu sana katika upangaji wa mkakati wa utengenezaji wa video ya Lwakatare na vitendo vya kihalifu vya utekwaji wa Kibanda na tukio la kutekwa na kisha kutupwa msutuni kwa mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka.
Kwa mfano, simu ya Mwigulu Nchemba namba 0714 008888, 0756 008888 na 0757 946223, zimefanya mawasiliano mara kadhaa na Ludovick Joseph, Saumu K. Malungu, Jack Zoka, Ali Shaali na Ramadhani Ighondo.
Mawasiliano hayo yalifanyika katika kipindi ambacho mgomo wa madaktari ulishamiri; baadaye yakarudi tena kati ya 26 Desemba mwaka jana na 15 Machi mwaka huu.
Miongoni mwa mawasiliano ambayo tunaona yanahusika na ujambazi huu, ni yale ya 28 Desemba, siku ambayo mkanda wa Lwakatare umerekodiwa.
Tarehe 4 hadi 6 Machi 2013, siku moja kabla ya Kibanda kutekwa na yale ya usiku wa manane (saa 8:17) wa 13 Machi 2013, ambako mchana uliofuata Lwakatare alikamatwa.
Huyu Mwagha ndiye aliyekuwa anatumika kuwasiliana na Saumu Malungu ambaye tulimtaja kuwa ndiye aliyekuwa amepewa kazi na Mwigulu na Usalama wa Taifa, kurubuni vijana wetu kwa fedha ili kutoa ushahidi wa uongo juu ya video ya Lwakatare.
Vilevile, mawasiliano ya Mwigulu na Mwagha katika kipindi hicho nayo tunayahitaji. Kwa sababu huyu Mwagha anayetumia simu 0754006355, mbali na kuwasiliana na Mwigulu, ndiye aliyekuwa anawasiliana na mmoja wa waliomteka Ulimboka; na ndiye aliyewasiliana na Saumu kati ya tarehe 20 Januari na Machi 6 mwaka huu.
Ludovick alifanya mawasiliano ya mwisho na Joyce Augustine, ambaye anatumia simu Na. 0717 559210, mawasiliano ambayo yalifanyika saa 5:13 usiku.
Hiyo ndiyo ilikuwa simu yake ya mwisho usiku huo; katika siku hiyo Ludovick aliwasilisna na Joyce mara tisa kuanzia saa 12: 54 asubuhi.
Kwa mujibu wa taarifa za kwenye mtandao wa Jamii Forum, ambako video ya Lwakatare ilitumwa, Ludovick alikamatwa Machi 15 mwaka huu.
Hata hivyo, rekodi katika simu yake Na. 0715 927100 inaonyesha tarehe 17 Machi, Ludovick alifanya mawasiliano na Joyce Augustine. Mawasiliano hayo yalifanyika saa 8:09 usiku, wakati inadaiwa na polisi alishakamatwa.
Nayemhariri wa Mwananchi, Msacky ambaye anatajwa kutaka kutekwa na Ludovick na Lwakatare, amekuwa na mawasiliano kadhaa na Ludovick – mtu anayepanga kumteka.
Ludovick na Msacky walifanya mawasiliano mfululizo kati 27 Desema 2012, siku moja kabla ya video ya Lwakatare haijarekodiwa na tarehe 7 Machi siku moja baada ya Kibanda kutekwa.
Msacky alitumia simu zake hizo mbili (0764 331010 na 0655 331010) kuwasiliana na Ludovick, huku Ludovick akitumia 0753927100.
Mawasiliano ya 31 Desemba yalifanyika Ludovick akiwa Tegeta, jijini Dar es Salaam. Mawakala hawa wawili wa Usalama wa Taifa (Ludovick na Msacky) walikutana 31 Desemba 2012, katika hoteli ya Tamal, Mwenge jijini Dar es Salaam.
Baada ya kupitia taarifa hizi za mawasiliano ya simu za Mwigulu Nchemba, Ludovick Joseph, Ramadhani Ighondo na Saumu Malungu tumegundua yafuatayo:
Kwamba, Ramadhani Ighondo amefanya mawasiliano mara nyingi na Mwigulu, Mwagha na Zoka; naye Mwagha amefanya mawasiliano na Mwigulu na Saumu; naye Saumu amefanya mawasiliano na Mwagha, Mwigulu na Shaali Ali, ambaye ni ofisa Usalama wa Taifa.
Tumegundua vilevile, kuwapo mawasiliano kadhaa kati ya Ludovick na Msacky; Ludovick na Mwigulu; Msacky na Nchimbi; Msacky na Mwagha, Saumu na Mwagha na Ramadhani Ighondo Abeid, anayetuhumiwa kumteka Dk. Ulimboka na Mwagha na Mwigulu.
Tumegundua pia kuwapo mawasiliano kati ya Ulimboka na Ramadhani; Zoka na Ighondo na Ridhiwani na Ighondo. Mawasiliano haya yalifanywa mfululizo usiku wa Juni 2012 siku ambayo Dk. Ulimboka alitekwa.
Tumepata kufahamu pia kwamba baadhi ya watu waliotajwa na gazeti la MwanaHALISI kuwa waliwasiliana na Ighondo usiku wa Juni 26, mwaka 2012, wamefanya mawasiliano pia na Mwigulu, Mwagha na Shaali Ali.
Mwagha ni ofisa Usalama wa Taifa anayefanya kazi makao makuu ya idara hiyo. Ndiye yule anayetumika kuendesha michezo ya kuhonga wanasiasa wa CCM na upinzani.
Ni Mwagha anayepanga wabunge na kuwapanga waongee nini kwa maslahi ya CCM. Ushenzi wote anaoongea Mwigulu bungeni hupewa na Mwagha kwa maelekezo ya Jack Zoka.
Naye Shaali ndiye aliyekutana na ofisa wetu wa usalama, Ahmed Sabula na mwenzake, Machi 29 mwaka huu katika hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam. Katika mkutano huo kati ya Sabula, kijana wetu wa usalama na ofisa usalama wa serikali, Shaali alitaka Sabula akubali kutumika kwa kutoa taarifa za vikao vya chama, kuwasilisha kwake nyaraka za Kamati Kuu na kueleza mipango ya chama katika kesi ya Lwakatare.
Kwenye mpango huu, ofisa huyo wa Usalama wa Taifa ambaye ninamfahamu vizuri, alimuahidi Sabula kiasi cha sh milioni 30 na kwamba fedha hizo angelipwa wiki iliyopita. Aliahidiwa pia kwamba kila nyaraka atakayopeleka atalipwa ujira.
Aidha, Sabula aliahidiwa kulipwa sh 500,000 kila mwezi; ofisa wetu huyu ameripoti tukio hilo kwa viongozi wake wa chama. Yule mwenzake aliandaliwa kuwa shahidi wa kesi ya Lwakatare; aliambiwa akikubali dili hiyo atalipwa kila mwezi sh 500,000 lakini akaombwa kuwa mvumilivu kwa kuwa atalazimika kupotea kwa miezi kama mitano hadi sita.
Kitendo cha Mwigulu kuwasiliana na Ramadhani Ighondo, Mwigulu kuwasiliana na Ludovick, Saumu kuwasiliana na Mwigulu, Ighondo kuwasiliana na Ulimboka, Zoka kuwasiliana na Ighondo, tena katika muda ule ule ambao Ighondo amewasiliana na Ulimboka na Saumu kuwasiliana na Mwagha, ni uthibitisho tosha kwamba Usalama wa Taifa wako nyuma ya mipango hii michafu ya kupanga utekaji na kisha kutaka kukichafua CHADEMA.
Aidha, kitendo cha Ludovick kuwasiliana na Msacky; Ighondo kuwasiliana na Mwagha, Ridhiwani Kikwete kuwasiliana na Ighondo, tena kila baada ya Ighondo kuwasiliana na Ulimboka na Jack Zoka, ni uthibitisho mwingine kuwa genge hili la wahalifu linashirikiana na baadhi ya watu kutaka kuangamiza taifa.
Ni uthibitisho tosha kwamba hawa ndiyo wanaowahonga wanachama wa CHADEMA na watu wengine ili watoe ushahidi feki dhidi ya Lwakatare, na kwamba ni Usalama wa Taifa walioandaa ile video uchwara inayopigiwa chapuo na Mwigulu.
Chama Cha Mapinduzi kinajua kwa hali ya sasa hakiwezi kushinda uchaguzi wa mwaka 2015 huku CHADEMA ikiwa katika hali nzuri ya kisiasa tunayoiona sasa.
Wanajua kabisa CCM imegawanyika, kundi lolote litakalopita ndani ya CCM, litahujumu kundi jingine. Ni kama ilivyotokea uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki.
Ndiyo maana wanapanga kila mbinu kutaka kuiangamiza CHADEMA. Nasi tunasema katu hatutakubali kuona CHADEMA kinakufa. Tutapambana usiku na mchana. Jua na mvua hadi tushinde hila hizi.
Tunawaambia wanachama wetu na wale wanaotuunga mkono, CHADEMA ni chama kikubwa. Kina mtandao kila mahali, kuanzia Ikulu hadi polisi; na hivyo hakitakufa au kuzorota kwa mambo ya kupikwa.
Ni imani yangu kwamba amri ya mahakama itawafichua wote hawa na kuirudisha Tanzania katika amani yake. Ni lazima tufikie mahala watu hawa wafahamike mbele ya umma, tunataka wafahamu kuwa maisha ya mwanadamu yana thamani kuliko siasa chafu na ufisadi wanaouendeleza,” alihitimisha Marando.

[TD="bgcolor: #ffffff"]
CHADEMA yafichua njama za vigogo
• Yawahusisha na matukio ya Ulimboka, Kibanda, Lwakatare

na Josephat Isango

[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF, align: center"]
amka2.gif
[/TD]
 
waraka wa magaidi kuweweseka kujinasua na ugaidi

Pilipili uso ila yakuwashaje? Kwa nini uweweseke kiasi cha kujaribu kuhujumu uhuru wa Watanzania Kuhabarika kama hukuguswa? Kati ya CDM na Magamba nani anaweweseka?
 
Acheni kuwahadaa wananchi na kuleta chuki zisizo na msingi wewe umeenda kwa wauza magazeti watano umekosa magazeti una generalize kuwa magazeti yote ya T.daima yamenunuliwa na watu wasiojulikana???? na watu wanakuungamkono bila kufikiria japo kidogo!!!!!!!!!!! Nipe majibu ya haya maswali haya kabla hatujaendeleza siasa chafu humu. 1. Ulipoamka leo kwanini uliwaza kununua gazeti la Tanzania Daima? 2. Ulikua unawaza kununa hilo gazeti mwenyewe hivyo ukaamini kuwa litakuwepo linakusubiri? Unafahamu maana ya hot news na kwamba husababisha watu kukimbilia gazeti husika kwa kiwango kisicho cha kawaida? umesema muuza magazeti alimesema walionunua ni watu wasiojulikana, je huwa anakumbukumbu ya kila anayenunua magazeti kila siku?

Mimi nilipokua naelekea airport majira ya saa 2 asubuhi nimelipata gazeti hilo pale ubungo nikajinyakulia nakala yangu nimefika mwanza nimelikuta kenye kibanda cha magazeti sasa sijui mtu anapataje guts za kusema magazeti yamenunuliwa na usalama wa taifa au ndiyo zile tafiti za kukaa mezani na kukubaliana tuweke takwimu hizi ili kupambana na na taasisi nyingine?

Mwenye kufuatilia vyema akumbuke kipindi gazeti la The citizen la Kenya lilipotoa habari ya utatanishi kuhusu Moi nini kilitokea kama siyo kuliteka gari la magazeti, na kuteka kiwanda cha kuprint magazeti hayo kama majambazi na kucho magazeti yote yaliyokuwa tayari ila kwa uwezo wa kipesa gazeti likaprintiwa nchi jirani siitaji maana sina uhakika!!!!!!! sembuse T. Daima inatoa copy ngapi kwa siku na kuuza ngapi?

Mzee usivurumishe kombora zito, nimepita pale Ubungo stend, vijiwe vyote vya kuuzia magazeti unavyovijua pale havikuwa na hata nakala MOJA ya gazeti hilo!
 
Free media fanyeni muirudie hii habari kwa siku kadhaa halafu tuwaone waendelee kuyanunua
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom