Gazeti la Seif Khatib lazuiliwa Pemba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gazeti la Seif Khatib lazuiliwa Pemba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mpita Njia, Jan 12, 2009.

 1. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #1
  Jan 12, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Waziri Mohammed Seif Khatib, kupitia kampuni yake ya Zanzibar media Corporation aliamua kulibadili gazeti lake la Asumini na kuliita Taifa Huru. gazeti hili lilikuwa lizinduliwe leo wakati wa sherehe za mapinduzi. Kwa maandalizi yatari alishachapisha kopi 200 za gazeti hilo ambazo zilipangwa zigawiwe bure kwa watu watakaohudhuris maadhimisho ya sherehe za mapinduzi katika kiwanja cha Gombani hiko pemba.
  lakini kwa mashanga wa Seif Khatib na wafanyakazi wake, vigogo wa SMZ (ambao hawajatajwa hadi sasa) walizuia kyugawanywa kwa gazeti hilo.
  Msajili wa magazeti Zenji, Issa Mohamed anasema alishalisajili gazeti hilo bila matatizo na yeye anashangaa kwa nini viongozi hao wa serikali wamelizuia gazeti hilo.
  Seif Khatib mwenyewe naye amesema hajua ni kwa nini gazeti lake limezuiliwa licha ya kutoa taarifa kwa wahusika kwua wamelenga kuchapisha gazeti na kuligawa bure kwa wasomaji watakaohudhuria sherehe za mapinduzi.
  walioliona gazeti hilo wanasema limechapisha habari za kawaida tu, ambazo haziwezi kuwa kkigezo cha kulifungua gazeti
   
 2. M

  Masatu JF-Expert Member

  #2
  Jan 12, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kinyanga'anyiro cha urais Zanzibar 2010 hicho kimeshaanza.

  Halafu huu ujasiriamali mkorogo mtupu waziri yeye, entrepreneur yeye mmh haya...
   
 3. Black Jesus

  Black Jesus JF-Expert Member

  #3
  Jan 12, 2009
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kadri usiku utakavyokuwa mkubwa basi ni lazima Alfajiri itachomoza ( )
   
 4. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #4
  Jan 13, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tuweke pembeni suala la kuwa gazeti hilo ni la Mohameed Seif Khatib. Hilo ni gazeti la kibinafsi . Sherehe za Mapinduzi ni za Kitaifa na maadhimishao yake yanafanywa na Serikali. Hivi kuna umuhimu gani au uhalali gani wa kuruhusu gazeti hilo la Binafsi kuingizwa katika ratiba za sherehe zinazodhimishwa na Serikali katika uwanja wa Gombani? Nafikiri Mohammed Seif Khatib ange"organise" kihafla chake mbali na maadhimisho ya Gombani na akagawa kijigazeti chake bure kwa waalikwa ikiwa kama ni sehemu ya Kampuni yake kusherehekea Maadhimisho ya Sherehe za Mapinduzi na kuanzishwa kwa kijigazeti chake. Kwa maoni yangu ni sahihi kabisa Maofisa wa Habari kukuzuia kisiingilie mtiririko wa ratinba ya Gombani.
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  Jan 13, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hoja sidhani kama ni kuingilia sherehe. Hoja ni kulizuia gazeti ambalo tayari limeshasajiliwa. kama ingekuwa ni hoja ya kutoingilia sherehe nadhani Seif Khatib angeambiwa akatafute sehemu nyingine ya kugawia gazeti lake. Lakini hata kama angegawa hilo gazeti wakatiw a sherehe hatua hiyo ingekuwa na athari gani?
   
 6. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #6
  Jan 13, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nielewavyo mimi hakuzuiwa kusambaza gazeti lake aliloruhusiwa kisheria kuchapisha. amezuiwa kuligawa katika Sherere za Gombani na waandaaji wa Sherehe hizo (Serikali). Hivi ukiwa na sherehe zako (taarab) na ukakataza watu fulani wasitunze hapo (wataharibu madoido ya sherehe) itakuwa ni kosa? Unafikiri kama watatokea watu saba kama Mo'd Seif wakitaka kusambaza vijarida vyao hapo Jee uruhusu tu?
   
 7. C

  Campana JF-Expert Member

  #7
  Jan 13, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Sheria na taratibu zao kandamizi zinawakandamiza wao sasa
   
Loading...