Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,850
- 30,193
KUMBUKUMBU YANGU FUPI YA MOHAMMED SEIF KHATIB
Mara yangu ya kwanza kukutana na Mohammed Seif Khatib uso kwa macho ilikuwa Makka wakati wa Hijja mwaka 1998.
Balozi Ramadhani Dau alinichukua kwenda kumsalimia Mzee Aboud Jumbe ambae alikuwa amefikia kwenye nyumba za wageni wa Mfalme wa Saudi Arabia.
Mzee Jumbe alifurahi sana kutuona.
Tulipokuwa tumekaa tunazungumza na Mzee Jumbe, Mohammed Seif Khatib akaja na kundi dogo la Wazanzibari kumwamkia Mzee Jumbe.
Furaha ya Mzee Jumbe ikazidi kwani Mohammed Seif Khatib akawa anatuzungumzisha akijaribu kutia maneno ya Kiarabu katika kuusifia utukufu na ukarimu wa serikali ya Saudia inavyokirimu wageni wake. Tukawa sote tunamsikiliza na kucheka.
Mara ya pili kukutana na Mohammed Seif Khatib ilikuwa mwaka wa 2007 Kilimanjaro Kempiski Hotel alipoalikwa na Oxford University Press (OUP), Nairobi kuja kuzindua Kamusi ya Kiswahili pamoja na kitabu changu, "The Torch on Kilimanjaro."
Katika sherehe ile Mohammed Seif Khatib alipokaribishwa kuzungumza na kuzindua vitabu hivi viwili aliomba radhi kuwa hatokizungumza "The Torch on Kilimanjaro," kwa kuwa hamfahamu mwandishi wake. Lakini mimi nikimfahamu yeye vyema kwa ajili ya ile staili yake ya uandishi wa makala zake katika Mzalendo, gazeti la CCM.
Katika timu ya OUP iliyokuja kutoka Nairobi kuhudhuria uzinduzi ule alikuwapo Sheikh Abdillah Nasir. Mohammed Seif Khatib alimsifia sana Sheikh Abdillah Nasir akasema alimsaidia katika uhariri wa mswada wa kitabu chake kimoja ambacho OUP walikichapa.
Mohamed Seif Khatib alipomaliza kuzungumza OUP waliniomba nikizungumze kitabu changu.
Hii ndiyo kumbukumbu yangu ya huyu ndugu yetu aliyetangulia mbele ya haki.
Allah amfanyie wepesi katika safari yake hii.