PreGE2025 POTOSHI Gazeti la Mwananchi limeandika 'Gwajima aomba rasmi msamaha'

PreGE2025 POTOSHI Gazeti la Mwananchi limeandika 'Gwajima aomba rasmi msamaha'

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
1749211825073.jpeg
 
Tunachokijua
Josephat Gwajima ni Askofu na mwanzilishi wa kanisa la 'Glory of Christ Tanzania Church' GCTC (Ufufuo na Uzima Ministries), kadhalika ni mwanasiasa ambaye mwaka 2020 alichaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM.

Tarehe 24 Mei, 2025 Gwajima alifanya mkutano na waandishi wa habari ambapo alisema kumekuwa na mlolongo wa matukio ya watu kutekwa pamoja na kupotea hivyo kutokana na hayo, aliamua kuitisha mkutano na waandishi wa habari kuongelea kuhusu suala hilo na kisha kutoa ushauri wa namna ya kudhibiti matukio hayo.


Nakala ya gazeti iliyochapishwa mtandaoni kuhusu Gwajima

Katika mtandao wa Facebook imechapishwa nakala ya Gazeti la Mwananchi Juni 06, 2025 ikiwa na kichwa habari kilichoandikwa kwa wino mzito kuwa 'Gwajima rasmi aomba msamaha'

Je, ni upi uhalisia wa nakala hiyo ya gazeti?

Kupitia utafutaji wa kutumia maneno muhimu (Key word search) JamiiCheck imejiridhisha kuwa nakala hiyo ya gazeti imepotoshwa kutoka kwenye nakala halisi ya gazeti la Mwananchi.

Aidha Gazeti la Mwananchi katika ukurasa wake wa mbele halikuandika 'Gwajima rasmi aomba msamaha' bali liliandika 'Sekeseke kanisa la Gwajima halijapoa' huku zikiambatanishwa nukuu za Antony Lusekelo (mzee wa upako) na James Mbatia wakikosoa uamuzi wa kufungiwa kwa kanisa la 'Glory of Christ Tanzania Church' (GCTC) linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima.

Rejea nakala halisi ya Gazeti la Mwananchi
1749211412585-png.3358028
Back
Top Bottom