Gazeti la MwanaHalisi mmetuchosha

mzee wa njaa

JF-Expert Member
Jun 16, 2011
1,366
223
Gazeti la Mwanahalisi mmetuchosha sana. Hivi hamna webiste editor au kazi imewashinda?
"""" Hii habari ya Rostam na Lowassa kumzima Kikwete"""" mtaiondoa lini imekaa kwenye front page wiki ya 2 na zaidi sasa. Badilisheni na wekeni ya wiki iliyoisha mnatuzingua nyie vp? Nendeni na wakati basi...wewe saed kubenea hulioni hili au mpaka tuwachafue mtuone wabaya? Tunataka mambo mapya sio kila siku yale yale. Tumechooooooka badilisheni habari iliyopo inatutia mafua tu.
 
Duh.......! Labda mwanahalisi watakusikia watarekebisha. Ila Raia Mwema kwa magazeti ya Wiki nalipenda sana,waandishi wake,bodi ya wahariri na management yake ni makini sana hata kama kuna mapungufu lakini naamini si mateka wa kifikra . Kuweni makini nanyi msije mkaangusha tasnia ya habari,watanzania makini wana imani nanyi sana

Yamebaki magazeti machache sana yaliyo huru siku hizi,mengi yamekuwa magazeti pendwa ya kisiasa.Magazeti/waandishi badilikeni,najua kuna wengi wazuri ila wanaharibiwa kazi zao na waajiri/wamiliki wa magazeti na waandishi wengine waganga njaa.Turejeshe Imani
 
sahihi kabisa,,mwanahalisi hawako current,ukifungua mtandaoni ni gazeti hilo la tarehe 8 june nadhani habari za akina rostam. raia mwema na mwananchi ndo pekee yanayoonekana mtandaoni yakienda na wakati
 
Inawezekana webmaster ni Kubenea mwenyewe. 2 weeks ago Mwanahalisi walisema kuwa Kubenea alikuwa anasafiri kwenda overseas. Sasa tangu ameondoka website imebaki kama ilivyokuwa kabla hajaondoka. Inaonekana hata email box yake itakuwa imejaa maana angeweza kufanya hizo updates akiwa hata chooni sijui India or somewhere.
 
MwanaHalisi imepoteza mwelekeo. Kubenea ameshawekwa sawa na Lowassa, Rostam na Chenge. Sasa hivi kazi yake kubwa ni kumshambulia Kikwete tu na kina Samuel Sitta na Nape Nnauye. Everybody has a price, Kubenea kwishnei!
 
Gazeti la Mwanahalisi mmetuchosha sana. Hivi hamna webiste editor au kazi imewashinda?"""" Hii habari ya Rostam na Lowassa kumzima Kikwete"""" mtaiondoa lini imekaa kwenye front page wiki ya 2 na zaidi sasa. Badilisheni na wekeni ya wiki iliyoisha mnatuzingua nyie vp? Nendeni na wakati basi...wewe saed kubenea hulioni hili au mpaka tuwachafue mtuone wabaya? Tunataka mambo mapya sio kila siku yale yale. Tumechooooooka badilisheni habari iliyopo inatutia mafua tu.
Unawalazimisha wawe update. Lakn wewe unachoktaka zaidi ni kusoma magazet kupitia mtandao, kitendo ambacho kinaua biashara na mitaji. Kuwa mzalendo kwa kununua gazet la mwanahalisi, usingoje litundikwe kwenye website.
 
Ni sahihi wakiwa wanaupdate mtandaoni,kwa sab nimelizoea ni lzm nilinunue kila jtano
Kwa sisi tuliozoea na kulisoma mstari kwa mstari makala zote,hata wakiaupdate mtandaoni kila mara bado tutanunua hard copy,natumai mlalamikaji hamaanishi kwamba kama linapatikana mtandaoni hatanunua vijiweni
 
Unawalazimisha wawe update. Lakn wewe unachoktaka zaidi ni kusoma magazet kupitia mtandao, kitendo ambacho kinaua biashara na mitaji. Kuwa mzalendo kwa kununua gazet la mwanahalisi, usingoje litundikwe kwenye website.

Kaka mi niko huku Australia ninue gazeti nitalipata wapi sasa? kuwa makini ndugu unajua huu ni utandawazi ni muhimu mtu uwe unapata habari mpya sasa ndio maana tunalalamika hii ni kwa wale ambao ni vigumu kupata magazeti....kama unaweza tutumie hayo magazeti huku lazima tuwaeleze wanachemka Tz ya leo sio ya kufanya website inakaa na hbr moja wiki 3.
 
MwanaHalisi imepoteza mwelekeo. Kubenea ameshawekwa sawa na Lowassa, Rostam na Chenge. Sasa hivi kazi yake kubwa ni kumshambulia Kikwete tu na kina Samuel Sitta na Nape Nnauye. Everybody has a price, Kubenea kwishnei!
Si rahisi kiasi hicho! Hilo ni kosa la kawaida linalofanywa karibuni na kila asasi na kwa gazeti la Mwanahalisi naona hii ni mara ya kwanza. Hata website ya BBCswahili mara kadhaa huwa haiwi updated, haswa haswa weekends. Ni kweli kila mtu ana bei yake lakini wapo pia wasionunulika kirahisi. Kama unabisha niambie bei za Mwinyi, Mkapa na JK et al tunazifahamu, lakini Nyerere au Sokoine zilikuwa kiasi gani? ukipata jibu zingatia Tanzania bado inayo wengi kama hao wa mwisho ila bado haijawagundua au kuwaamini kama wanaweza. Muda utadhihirisha!
 
Gazeti la Mwanahalisi mmetuchosha sana. Hivi hamna webiste editor au kazi imewashinda?
"""" Hii habari ya Rostam na Lowassa kumzima Kikwete"""" mtaiondoa lini imekaa kwenye front page wiki ya 2 na zaidi sasa. Badilisheni na wekeni ya wiki iliyoisha mnatuzingua nyie vp? Nendeni na wakati basi...wewe saed kubenea hulioni hili au mpaka tuwachafue mtuone wabaya? Tunataka mambo mapya sio kila siku yale yale. Tumechooooooka badilisheni habari iliyopo inatutia mafua tu.

Bila majina hayo kwenye front page gazeti halinunuliwi!
 
Hahahahah watanzanai wako radhi wakakae kwa wauza magazetu apige porojo huku akipitia kichwa cha habari kimoja baaada ya kingine, baadae anaaga hata kumuungisha muuzaji.

Sasa wewe mwenye tabia hii unaua biashara za wengine. kwa mlioko nje ya nchi tunaelewa sana, lazima mlalame siku zingine siku haziendi kabisaa.Big up sana mkuu kwa kuwakumbusha. Jiunge SACCOSS tupunguze njaa na urasimu wa kulalamika hatusaidiwi.

NI rahisi tu, tuma jina, namba ya simu, na email address (jina halisi siyo nickname). Au nitumie message kwenye simu yangu 0655 447788 ukinipa hizo details zako.

karibu sana wadau, tujenge utaratibu wa kujitegemea.

CD
 
caroline danzi umejibu vyema pamoja na kwamba wengi hawapendi kununua magazeti ila hupenda kusoma yale ambayo yameshanunuliwa pia uchumi na jambo lingine linalowakaba wananchi. sasa umetaja saccos ya nini tena hapo nipe kwenye 0653050735
 
Hii habari haipo sehemu yake potelea mbali sababu na shabaha ya kuianzisha
 
pamoja na mambo mengine,Mwana Halisi limepoteza dira kabisa na mvuto wake wa awali umepungua kiasi cha kusubiri tu muda mfupi wa kulizika kabisa gazeti hili.
Gazeti limekua ni la UDAKU wa kisiasa kwa muda mrefu sasa,lime acha kuandika habari za kiuchunguzi na kuandika personal issues za watu wawili tu.ROSTAM NA LOWASA..fuatilieni matoleo yake 95% ya front page zake ni either RA au EL huu ni udaku ku discuss mtu kwa kumuandama badala ya issues za msingi.EL na RA wana madudu yao YES.lakini MWANA HALISI kuifanya ndo ajenda yao ya kudumu kwa miaka 3 ni jambo la kutiliwa shaka sana kama Gazeti hili lilianzishwa ajiri ya kuibua issues sensitive katika Jamii au lengo lake ni CHARACTER ASSASSINATION kwa hawa watu2?
 
Tatizo lao ni kuuza hardcopy ndio maana wanachelewa kuliweka mtandaoni, ila sasa cha ajabu likitoka tu mikoni linaisha siku hiyo hiyo ukilipata siku inayofuata ni bahati yako kwahiyo niwaombe tu wahusika Kubenea & Co mtuwekee mapema angalau baada ya siku 2 tangu litoke
 
Yaani watanzania ni wepesi sana kuamini hadithi nyepesi nyepesi,Ingefanyika Research tungeweza kuja na conclussion ni kwanini magazeti pendwa yananunulika kwa wingi.Watanzania tumefikia hatua mbaya ya kutopenda kusoma analytical stories au kutafakari kilichoandikwa kwenye magazeti.Ndiyo maana inakuwa Rahisi kuingizwa mkenge na vigazeti Pendwa.

Kwenye hili Bunge la Bajeti utashuhudia baadhi ya magazeti yanaandika kishabiki tu,hakuna analysis.Na hata wakiona hoja nzito zinazotolewa na watu wasioelewana nao hawataandika,je wanaitendea haki jamii?Je, magazeti kama hayo yanajua ni kwanini yameingia katika Tasnia ya habari? Gazeti lolote linalojipambanua la kiuchunguzi au linalojiita-pro change ni lazima lingejenga hoja na kuzipa uzito hoja zinazohusu mjadala wa Posho uliochokozwa na Zitto ..!!!!!!??????!!........Ni matumaini yangu sasa wataandika kuhusu suala la posho na hoja zinazotolewa kwenye hili Bunge la bajeti!

Vyombo vya habari ni sehemu ya democracy,ni mhimili mwingine wa Dola.Huu ni mhimili muhimu katika kurekebisha,kukosoa na kuwahabarisha umma juu ya mapungufu ya hiyo mihimili mitatu.Tusiruhusu na tusiwachukulie serious wale waandishi na vyombo ambavyo ni corrupt,Biased nk.Huo nao ni ufisadi katika mhimili Muhimu
 
Ni kweli vichwa vya habari havibadiliki sana,kwa mimi ninavyofahamu hawa wanaosemwa vibaya kama ingekuwa uongo hili gazeti lingeshafutwa siku nyingi sana.We andika habari za kijiji cha kazimzumbwi kama litauzika,umechoka kusoma mwanahalisi kumbe unataka usome gazeti la uhuru au mzalendo nenda kasome wala hakuna anakukataza,mtandao wa mafisadi hauishi kwa siku moja,hizo ni habari endelevu kamwe usichoke kusoma habari za EL,RA na JK hawa ndio walioifikisha nchi yetu hapa tulipo, ndio maadui zetu wakubwa,suala la kubenea kanunuliwa tu kwasababu anamwandika JK mimi siungani na wewe data unazo???2.leo ukiandika sanaaaa habari za simba kesho uiandika habari za yanga kwahiyo umenunuliwa???Hii ni biashara unaangalia hot news ni zipi watu wazisome bila kujali zinatokea upande wa jk au rachel.
 
Back
Top Bottom