Wapendwa salaam. Nimesoma post zote kuhusu Dk. Mpoki. Kabla sijachangia maana walioleta ujumbe huu nikisoma naona hata wao wanauone aibu naomba kusema machache yafuatayo.
1. Kwa muda mrefu kwenye jukwaa hili na mengine wadau mmekuwa mkilalamika kuwa ubora wa uandishi Tanzania umeshuka na vyombo vya Habari vimeooteza sifa.
2. Sisi JAMHURI tukakaa wahariri wanne tukasema tuanzishe gazeti la uchunguzi litakalotoa mfano wa Habari bora za Uchunguzi. Tukaanzisha gazeti la JAMHURI.
3. Tusipoandika jambo fulani (kama waandishi nchini) kupitia jamvi hili au mengine tunaambiwa tumehongwa.
4. Tukichunguza na kuandika jambo Fulani kama hili la Dk. Mpoki, Bandari/Kipande, Maliasili, Flow Meters, Dawa za Kulevya, Wauza Madini feki, Merereni, na sasa TBL... Tunaambiwa JAMHURI tunatumika.
5. Ningependa tushauriane Tanzania tunahitaji uandishi wa aina gani?
Baada ya utangulizi huo, niseme mahususi hili la Dk. Mpoke. Nashindwa kuelewa wanaomtetea wanapa wapi ujasiri kwa sababu zifuatazo:-
1. Hatukumvizia. Mimi na Manyerere baada ya kukamilisha uchunguzi tulikwenda ofisini kwake na vielelezo vyite, zikiwamo nakala za risiti za kufoji alizoandika kwa mkono wake, akakiri kuwa ni Mwandiko wake na akatueleza hayo aliyosema.
2. Mashine inayouzwa dola 41,000 amekiri kuinunua dola 91,000. Key holders zinazouzwa Sh 3,500, amekiri kuzinunua dola 25 kila moja.
3. Pamoja na kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Mbeya, wanasema Sheria ya Ununuzi wa Umma (2004/2011), ameifahamu aliooteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Afya na kwenda semina Ikulu (a very irresponsible statement).
4. Wapambe wake wakiwamo hawa walioleta hoja hapa wanapishana ofisini kwetu tangu Siku ya kwanza tulipomhoji Dk. Mpoki wakibembeleza habari hii tusiitoe (ushahidi wa CCTV Camera upo).
5. Wamenunua Magazeti yetu ju.la Mbeya, Iringa, Dodoma na sehemu nyingine baada ya kugonga mwamba juu ya ahadi zao kwetu zinazonuka rushwa.
6. Mpoki ni mtu mzima. Anakuwa na gari la Serikali bila aibu wanasema liligonga ng'ombe likaharibika difu, hakuripoti Polisi na gari hilo 'bovu' akaandaa mchakato wa kulinunua!
Nisiwachoahe, ila nihitimishe kwa kuwambia hivi, Gazeti la JAMHURI ni makini. Lilistahili kusifiwa na Rais Magufuli. Mwambie Dk. Mpoki aje hapa athubutu kukanusha hata neno kati ya tuliyoyaandika.
Kwa hawa walioleta mada hii niwashauri tu, kwamba inawezekana hamthamini tena heshima zenu, ila basi Siku nyingine msikubali kufanywa ngao katika masuala kama haya kwa heshima ya familia zetu.
JAMHURI, litaendelea kutumbua majipu kwa ufasaha, maneno kama haya tuliyatarajia maana usaa ukitoka ngozi inauma. Ni rahisi mirija inayoona chupa inavunjwa, itajuwa Tayari kupigana kuepusha uji usimwagike.
Deodatus Balile,
Mkurugenzi/Mhariri Mtendaji,
Gazeti la JAMHURI (lisome kila Jumanne kwa Habari makini za uchunguzi).