Gazeti la Jamhuri linatumika kumchafua Dr. Mpoki

tutafikatu

JF-Expert Member
Dec 17, 2011
3,307
4,585
Nimebahatika kumfahamu Dr. Mpoki tukiwa Muhimbili. Namfahamu ni kati ya watu honest sana. Nimehuzunika kuona gazeti la Jamhuri likitumika kuandika habari zake ambazo kwa nafasi yangu nimebahatika kuujua ukweli wake, huku likiacha big picture. Inawezekana Dr. Mpoki ni jipu, lakini sidhani kama waweza ukaona jipu dogo, kabla hujaona kubwa. Kama kweli hawa Jamhuri wameona ubadhirifu wa Dr. Mpoki bila shaka wliona ubadhirifu mkubwa zaidi Mbeya, lakini kwa kuwa wanajua malengo yao hawawezi wakasema chochote. Hivi hawashtuki mtu aliyekuwa naibu mkurugenzi kwa miaka zaidi ya kumi, akinunua CT scan baada ya hiyo nafasi kuisha; wakati huyohuyo mkurugenzi hakuiwezesha hospitali yake kuwa na CT Scan kwa miaka yote akiwa kiongozi?

Kama kweli gazeti la Jamhuri wana nia ya kuisaidia serikali, wangeanza na wizi wa mamilioni ya pesa za HIV pale Mbeya Referral Hospital kwa zaidi ya miaka kumi, ambayo ilikuwa ikipata kila mwaka zaidi ya 1.5 billion na nyingi zikawa zinaishia kwa wajanja kwa kudanganya uagizaji wa vifaa tiba, semina za uongo na kweli, supervision za uongo, n.k. Dr. Mpoki kafika Mbeya wakati Walter Reed wameshika control ya pesa, na kupunguza zaidi ya nusu ya budget ya kila mwaka.

Ninafahamu Dr. Mpoki ana mgogoro mkubwa sana na Dr. Mselle wa Muhimbili National Hospital, ambaye alikuwa mwajiriwa mwenzake na kila mmoja aliwahi kuwa mkuu wa Idara wa mwenzake. Magomvi yote yalitokana na kugombea ukuu wa idara. Ombeni Sefue aliposimamishwa u KMK Dr. Mselle alifanya sherehe, akidhani Sefue ndiye anayembeba Dr. Mpoki. Inajulikana Mselle amekuwa akifanya figisufigisu za chini kwa chini ili Mpoki aonekane ni mbadhirifu, lakini hushindwa.

Dr. Mpoki alipoteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa Mbeya alikuta kuna wizi mkubwa umefanyika wa pesa za HIV toka Walter Reed, (hadi budget yao kwa hospitali ikapunguzwa, na baadhi ya vitu kama kununua dawa wakaanza kuvifanya wao) na kwa bahati mbaya akakutana na team ya former administrators ambao walikuwa wakigombea kwa udi na uvumba mmoja wao kuwa mkurugenzi wa hospitali ya rufaa Mbeya.

Kuna team ya mapambano dhidi ya Dr. Mpoki iliundwa na viongozi walionufaika na miradi ya HIV, timu hii ilikuwa ikifanya kila namna kumtengenezea mabomu Dr. Mpoki hasahasa katika kupitisha malipo ya vifaa tiba, hasa wakitaka kutumia ugeni wake. Hawa walikuwa wanafanya kila jitihada ya kumharibia Dr. Mpoki, ili aondoke hospitali ya rufaa kwa sababu aliwabana sana. Hawa walikuwa baadhi ya wana timu:

1. Humphrey Kiwelu ambaye kwa kipindi kirefu alikuwa naibu Mkurugenzi, na baada ya kuacha hiyo nafasi akanunua mashine binafsi ya CT scan, wakati hospitali ya rufaa Mbeya aliyokuwa akiiongoza haijawahi kuwa na CT Scan toka ianzishwe. Dr. Kiwelu amekula pesa nyingi za HIV toka Walter Reed, kutoa invoice fake na kulipwa pesa kwa vifaa vya radiology vilivyotolewa kwa msaada, n.k.

2. Dr. Msafiri Birigi, huyu pia alihusika katika ulaji wa pesa za HIV na kuna kipindi alikuwa msimamizi wa kutoa magovi mkoa.

3. Nsekela. Huyu ni accountant ambaye nasikia sasa kahamia Dar es Salaam. Anahusika katika wizi wa pesa mbalimbali za hospitali na mara nyingi amekuwa akijifanya ni usalama wa taifa. Yeye ni Dr. Mpoki ni kama paka na panya.

4. Aisha Mtanda, huyu alikuwa katibu wa hospitali, ambaye alishawahi kumfokea Dr. Mpoki. Anahusika kutumia pesa za HIV kwa matumizi mbalimbali. Alitajwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mmoja wa Wakuu wa wilaya wa Mbeya (sasa ni mbunge) na pia Jina la mbunge lilitumika kulipwa pesa kwa ajili ya kitu kisichohusiana na hospitali kwa safari ya kwenda Canada, kwa masuala ya kilimo. Aisha pia alikuwa akichukua pesa za hospitali, akidai ni ada za vyuo anavyosoma full time nje jambo ambalo si kweli.

5. Mama Wanguvu. Huyu ni mmoja ya accountant anayehusika na yote hayo hapo juu.

6. Sadick wa engineering.

7. Patron Isdory ambaye alihusika sana kutengeneza budget za pesa toka Walter Reed na pamoja na kuzipiga zikifika.

8. Dr. Mabula, ambaye walikuwa wakikosana na Dr. Mpoki hasa kutokana na kutotumia muda wake mwingi kuwa kazini, badala yake akishinda kwenye kliniki yake. Pia Dr. Mpoki alikuwa akizikataa qualifications za Dr. Mabula kwamba yeye ni daktari bingwa kwa sababu anadai alisoma China na kwa kipindi kisichofika miaka miwili. Dr. Mabula alihamishwa na wizara kwenda hospitali ya Dodoma lakini ndani ya mwezi mmoja barua iliyosainiwa na Dr. Mbando ikambakisha kwenye kituo chake cha Mbeya.

Dr. Mpoki anatajwa na gazeti la Jamhuri kujiuzia gari, kitu kisichokuwa kweli, kwanza Dr. Mpoki alikuwa ni kati ya watu wengi wakihusisha madaktari walioomba kuuziwa gari hilo na mpaka sasa hawajajibiwa maombi yao na Transport Officer wa MoH. Gari hii ilitolewa na Walter Reed na ina zaidi ya miaka mitano sasa na haina gharama hizo zinazotajwa.

Usalama wa taifa, PCCB na vyombo vya ulinzi vinafahamu haya, ajabu hayashughulikiwi. Tunajua watu wa PCCB Mbeya wamekuwa kwa kipindi kirefu wamekuwa wakihongwa vipesa vidogovidogo na kusumbua watu wasiokuwa na matatizo ambao hawako radhi kuwapoza kwa allegations wasizohusika nazo.

MAONI

Serikali, ikague matumizi ya pesa za HIV toka Walter Reed katika hospitali ya Rufaa Mbeya, na pia nyanda za juu kusini kwa ujumla - Mbeya, Rukwa, Songea, Katavi ambao huu mradi wa Walter Reed unafanya kazi.

Serikali iwachunguze watajwa hapo juu, pamoja na Dr. Mpoki na Dr. Elietery Samky aliyekuwa Mkurugenzi Mstaafu Mbeya ili kujiridhisha. Ni ajabu kuona Dr. Humphrey Kiwelu kununua CT scan soon after kutoka kwenye nafasi yake ya Ukurugenzi na ukakaa kimya huku ukijua allegations nyingi na za muda mrefu juu yake, tena hizi allegations ndizo zilimnyima Ukurugenzi wa hospitali (huwa anajifanya ana ushirikiano wa kumiliki CT scan na mtu toka Australia).
 
Yaani hawa jamaa nadhani wanataka watumie vibaya sifa ya kusifiwa na Rais.
Nadhani viongozi wa kiserikali waache kutoa promo kwa vyombo vya habari.
 
Duuh! Mara nyingi waovu ndiyo huwa wana mbinu nyingi sana za kuwaharibia watu wema ktk maofisi. Na bahati mbaya hata vyombo ambavyo vilitakiwa kuwa msaada kwenye mambo haya mf. PCCB, usalama wa taifa, n.k vimekuwa vikiingia ama kuingjzwa kwenye hizi game chafu. Lkn huyu Dr. Mpoki haki yake haitapotea.
 
image.jpeg
 
siAsa siasani! kazi bila siasa haziendi. ni zaid ya kugombe ubunge jimboni. ukiona jinsi watu wanavyopigania vyeo, waone wenzao waharikiwe wenyewe wapete.
 
Yaani hawa jamaa nadhani wanataka watumie vibaya sifa ya kusifiwa na Rais.
Nadhani viongozi wa kiserikali waache kutoa promo kwa vyombo vya habari.
Wewe jamaa unachekesha kweli. Katuhumiwa kujiuzia gari la serikali kwa bei chee, katuhumiwa kusafiri nje ya nchi bila kibali cha JPM. Wewe unatetea kipi hapo. Unaleta story za RUFAA MBEYA zina uhusiano gani na hayo. Kwa utetezi wako Magu hawezi kumaliza ufisadi nchi hii. Muacheni abebe msalaba wake. Hata shetani alikuwa malaika mkuu mbinguni, alifanya mengi mazuri kwa Mungu lakini alipoacha njia alitupwa chini. Dr. Mpoki OUT
 
Wewe ni mtetezi wake?hujui the other side ya tabia yake?
Wewe unye ijua tabia take iweke hapa, usiwe kama kagazete jamhuri kana seam uongo mchana kweupee.

Hilo gari waliloonesha toka lini likauzwa shs 300 milioni?
 
Wewe jamaa unachekesha kweli. Katuhumiwa kujiuzia gari la serikali kwa bei chee, katuhumiwa kusafiri nje ya nchi bila kibali cha JPM. Wewe unatetea kipi hapo. Unaleta story za RUFAA MBEYA zina uhusiano gani na hayo. Kwa utetezi wako Magu hawezi kumaliza ufisadi nchi hii. Muacheni abebe msalaba wake. Hata shetani alikuwa malaika mkuu mbinguni, alifanya mengi mazuri kwa Mungu lakini alipoacha njia alitupwa chini. Dr. Mpoki OUT
OUT kwa tuhuma za kwenye Gazeti? zimefanyiwa uchunguzi ikagundulika ni kweli? so siku hizi mtu akiandikwa tu kwenye gazeti basi OUT maana ni jipu! Nimelidharau kabisa gazeti la Jamuhuri! Hilo Gari analo alishauziwa? unaweza kuthibitisha hapa?
 
Majipu yanapotumbuliwa lazima mtu aweweseke......hasa yale yaliyopo sehemu ile mbaya......WIzara ya Afya kuna ufisadi mkubwa sana.....MPOKI GO....GO....GO....GO.....utasemewa mabaya zaidi ya haya, wewe ukishirikiana na wenzako na timu nzima ya JPM endeleeni kuyatumbua tu hayo majipu.....yataweweseka......yatalia......NYIE YATUMBUENI TUUUU na safisha kabisa mahusaa ili yasiote tena.....TUMBUAAAAA.......
 
kweli wanaochapa kazi ndio wanaopigwa vita.wito wangu kwa takukuru hilo swala wadilichukulie jujuu wafanye uchunguz.na wakibain ukweli waweke wazi.imeniuma sana kusoma hizi tuhuma juu ya dk mpok aliye iokoa rufaa toka mikononi mwa mafisi.ila siwezi kumtetea sana watu wana pande mbili.lakini nijuavyo mimi mpoki ni mtu wa kazi na muadilifu saana.
 
Watapigana na hawatashinda, jiran yangu Dr Mpoki piga kazi endelea kuonesha weledi wako katika wizara mpya.

GBU
 
Ukisoma pande zote utagundua kwamba kila mtu ana yake aliyotenda ambayo yanayoliumiza taifa. Kinachotakiwa ni kufanya uchunguzi maeneo yote yanayoainishwa sio pekee na Gazeti la Jamhuri bali na Mtoa Bandiko. Inaonekana kila mtu anapenda ashike kitengo, na ugomvi wao hauwasaidii wananchi. Nia ni kupata ukweli na kuepuka na migogoro isiyo na tija kwa serikali yetu na watu wanaopata huduma pale hospitalini.
 
Mpoki matuhuma mengi kayakubali sasa watetezi mnasimamisha mihipa ya shingo ya nini?
 
Hili gazeti la Jamhuri kumbe ni la hovyo hivi???
Linachafua watendaji wema , Kwa manufaa ya wachache.
Mbona lilikaa kimya kashfa ya Januari Makamba Na mzungu wa dadake????

NASHAURI SERIKALI IWE MAKINI NA WIZARA YA AFYA , INAWEZEKANA IKAWA NI WIZARA INAYOONGOZA KWA MAJUNGU AFRIKA MASHARIKI ,
HAIWEZEKANI KILA KATIBU MKUU, WAZIRI , AU NAIBU WAZIRI AWE NA KASHFA.... CHUNGUZA WALIOPITA KTK HIVYO VYEO WOTE WALIJERUHIWA NA KASHFA SABABU YA VYEO VYAO.
Mti wenye matunda matamu ndio hupigwa mawe .
 
Mtetezi wa Dr. Mpoki atambue kuwa uowu wa watu wengine hauwezi kuwa kinga kwa mtu mwingine dhidi ya maovu yake. Gazeti la Jamhuri limeandika Dr Mpoki amesafiri nje ya nchi bila kibali toka ofisi ya rais, je mtetezi anasemaje kuhusu hilo?
 
Back
Top Bottom