Gazeti la Freeman Mbowe latumika kumsafisha LOWASSA

Mimi mwenyewe nikiwa ni mwandishi wa habari, nimeshtushwa, nimeshangaa na kupigwa butwaa na kitendo cha gazeti la Tanzania Daima, ambalo linamilikiwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, kutumika kumsafisha Edward Lowassa.

Pamoja ni kweli kuwa Mbowe anasifika kwa kutoa uhuru kwa wahariri wake na huwa haingilii editorial independence ya newsroom, naona sasa gazeti hili limekwenda too far.

Tanzania Daima la leo Jumamosi Novemba 27, 2010, kina habari kwenye ukurasa wa mbele yenye kichwa cha habari: "Lowassa: Nimechoka kuzushiwa. * Mwanaye ajipanga kuchukua hatua za kisheria kujisafisha."

Kwenye habari hiyo, gazeti la Tanzania Daima kwa makusudi kabisa linamuita Lowassa Waziri Mkuu "mstaafu."

Huu ni upotoshaji wa makusudi kwani taifa zima linajua Lowassa kamwe hakustaafu, alilazimika kujiuzulu mwaka 2008 baada ya kuhusishwa na kashfa ya ufisadi ya Richmond.

Kitendo cha Tanzania Daima kumuita Lowassa kimakosa kwa makusudi kuwa ni Waziri Mkuu "mstaafu" kina lengo maalum ya kumuweka mwanasiasa huyu aliyechafuka kwenye kundi moja kama mawaziri wakuu wa zamani waliostaafu kiheshima kama Cleopa David Msuya, Salim Ahmed Salim, Joseph Warioba, John Malecela na Frederick Sumaye.

Ukweli utabaki palepale kuwa Lowassa ni waziri mkuu "aliyejiuzulu" kwa kashfa ya ufisadi na si "mstaafu."

Kwenye habari hiyo inayombeba waziwazi Lowassa, hakuna sehemu popote ambapo kashfa ya Richmond inatajwa wala mazingira ya Lowassa kutoka serikalini kuelezwa.

Badala yake, gazeti hili limetoa platform prominently kwenye ukurasa wa kwanza kwa Lowassa kueleza kuchoshwa kwake "kuzushiwa" mambo na kusisitiza kuwa yeye hajatoswa na Kikwete na wala alikuwa hataki nafasi yoyote ya uwaziri.

Pia, gazeti hilo limetumika kama mouthpiece kwa kutoa fursa ndefu kwa Lowassa kumtetea mtoto wake Frederick, ambaye aliripotiwa na gazeti la RAIA MWEMA la wiki hii kuwa anachunguzwa na polisi Uingereza kwa tuhuma za money laundering baada ya kununua nyumba huko UK yenye thamani ya shilingi bilioni 1/-.

Inaeleweka kuwa Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, Absalom Kibanda, ni rafiki wa karibu wa Lowassa na pia anafanya kazi kwenye magazine ya Lowassa inayoitwa UMOJA.

Hivi mmiliki wa Tanzania Daima, Freeman Mbowe, anaelewa kuwa gazeti lake limekuwa likitumika mara kwa mara kumsafisha Lowassa na swahiba wake Rostam Aziz?

Kama jibu ndiyo, kwa nini anaachia hali hii na kuendelea kuwa na Mhariri Mkuu Kibanda mwenye conflict of interest kwa kuwa pia ameajiriwa na Lowassa?

Acha porojo weweeeeee!!!
 
Huko ndie kule kusema unasoma btn the lines, unasoma na kuona hapana something is wrong somewhere! I have been doing so even kwa mwanahalisi na nikaja kugundua ni la JK, na sasa kumbe TZ daima la Lowassa! niliacha kusoma Tz daima mwaka wa nne sasa.

Kuna vitu unasoma, unatafakari/meditate na unaona havijakaa sawa, haviko vinavyotakiwa kuwa they call this 'critical thinking' unaangalia manufaa ya mwananchi kwa kusoma hiyo habari.

Kibanda tangu alipoingilia uchaguzi wa mwenyekiti wa chadema nilianza kuwa na wasiwasi naye kama huyu mwandishi wa habari kweli yuko fair, nilishangaa pia kuona hata Kubenea ana uvuruga ule uchaguzi na kusaidia kubakwa kwa demokrasia waziwazi!

asanteni kwa michango yenu, napata soda bariiidi hapa huku nikitafakari mliyoyaandika

Kaka hapo kwenye red naomba ufafanue..... Mhhh Kaazi Kweli kweli
 
Kwa nini harakati za Lowasa kushambuliwa kutoka ndani ya CCM sasa zipo juu. Kuna nini. Lowasa ni fisadi, sawa! Lakini hizi harakati za kumshambulia (akiwemo Malaria Sugu) zimenishtua. WanaJF nani insider atusaidie. Kuna kitu kisichokuwa cha kawaida ndani ya CCM!!!!
 
Wameshajua ni mzigo watu wamechoka na ufisadi wamegundia kwa JK kubeba mafisadi ndio akapoteza kura na ashukuru Chadema hawakujipanga vyema nchi nzima na hawakua wamoja saaana, na baadhi hawakuamini watachukua nchi,ss kuelekea 2015 hawataki mafisadi tena
 
Kumbuka Tanzania Daima ni gazeti huru, au mnadhani kwa vile linamilikiwa na Mbowe kutoka upinzani basi ndio maisha halitakiwi kuripoti habari za watu wa upande wa pili? Hili si sawa na magazeti ya Mtanzania na Rai ambayo hayajui hata kuandika habari za wapinzani wao siku moja moja.
 
Kitendo cha Tanzania Daima kumuita Lowassa kimakosa kwa makusudi kuwa ni Waziri Mkuu "mstaafu" kina lengo maalum ya kumuweka mwanasiasa huyu aliyechafuka kwenye kundi moja kama mawaziri wakuu wa zamani waliostaafu kiheshima kama Cleopa David Msuya, Salim Ahmed Salim, Joseph Warioba, John Malecela na Frederick Sumaye.

Ukweli utabaki palepale kuwa Lowassa ni waziri mkuu "aliyejiuzulu" kwa kashfa ya ufisadi na si "mstaafu."

Fikra zangu zinanituma kusema kwamba Informer aamechukua kipande kidogo sana cha ile habari kufanya hitimisho. WanaJF nao wameingia kichwa kichwa tu kujalidi hicho kipande. Nimesoma gazeti hilo na sijaona huo usafishaji ulipo. The positive side of that story inatuambia kuwa Mbowe haingilii utendaji kazi mahala ambapo taaluma inahitajika. He is a freeman and would want other people to have a free mind. Tuzungumze hoja zingine kwani hoja hii haituongezei wanachama.
 
Acheni fitina chadema sio chama cha mtu mmoja ni chama cha watu kama wewe mamluki na umetumwa ukome.
 
Kaka hapo kwenye red naomba ufafanue..... Mhhh Kaazi Kweli kweli

kweli kazi unafikiri ndogo, fanya assignment, mwenywe kwanza, nipe habari yeote ya mwanahalisi ambayo imemwandika vibaya JK, compare na zile zilizompa shavu kiaina.

rudi nyuma muulize kubenea ni mwanachama wa chama gani? alivyotaka kugombea ubunge uchaguzi uliopita alitaka kugombea kwa tiketi ya chama gani?

Some details are shocking brother,

kwa kifupi taarifa nyingi za ufisadi kutoka gazeti hili zinamuinua na kumuimarisha JK!
 
Acheni fitina chadema sio chama cha mtu mmoja ni chama cha watu kama wewe mamluki na umetumwa ukome.
 
Kwa nini harakati za Lowasa kushambuliwa kutoka ndani ya CCM sasa zipo juu. Kuna nini. Lowasa ni fisadi, sawa! Lakini hizi harakati za kumshambulia (akiwemo Malaria Sugu) zimenishtua. WanaJF nani insider atusaidie. Kuna kitu kisichokuwa cha kawaida ndani ya CCM!!!!

Hata mimi nimeanza ku - reason on those lines inashangaza..... kinachotisha zaidi ni kwanini kuanza kumuhusisha na Chadema ambayo inapinga mafisadi, Je hii ni njia moja ya kutaka kuisarambatisha Chadema... (This allegation ya uhusiano na Mbowe) kwanini iletwe sasa? Why Now? kwaufupi kuna more questions than answears na kila jibu linaleta maswali mengi zaidi
 
Nimesoma maoni ya wanajamii. Hii si mara ya kwanza kwa Kibanda ambaye ni mimi kuingia katika msukosuko wa kushambuliwa hasa ninapogusa hisia za watu au taasisi kupitia katika safu yangu ya 'TUENDAKO' au kupitia maandishi katika gazeti la Tanzania Daima ambalo mimi ni mwajiriwa wake.

KUCHAFUA

Kwanza napenda kusema bayana kwamba 'kusafisha' na 'kuchafua' ni misamiati ambayo siku zote nimesimama kidete kukabiliana nayo kwa maneno, maandishi na matendo. Ninaamini tena kwa dhati kabisa kwamba, wajibu wangu wa msingi kama mwanahabari ni kuhakikisha kuwa siku zote niko juu ya siasa za makundi hususan yale yaliyo ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Msimamo wangu huo nimeuweka bayana katika majukwaa mbalimbali ya kihabari na kitaaluma. Ni kwa kuwa na imani hiyo ndiyo maana maandishi yangu, hususan yale ya kupitia katika safu yangu yamekuwa above political inclinations ambazo katika zama hizi zinatawaliwa na kuongozwa na matakwa ya makundi ya akina Samuel Sitta (kwa upande mmoja) na Edward Lowassa (kwa upande wa pili).

Kwangu mimi tatizo ni ufisadi na kwamba miongoni mwa wanasiasa wa ndani ya CCM waliopata kushika nyadhifa za juu kama za uwaziri, uspika na ubunge kupitia katika chama hicho hakuna hata mmoja mwenye ubavu wa kumnyoshea kidole mwingine kwa ufisadi.

Ni kwa sababu hiyo basi, Tanzania Daima, gazeti ambalo nimepewa dhamana ya kuliongoza limekuwa huru kuwasifu inapobidi na kuwaponda inapolazimu wanasiasa wa makundi yote ndani ya CCM wawe ni wale wanaojiita makamanda wa ufisadi au wale majeruhi wa ufisadi. Nikiwa kiongozi wa gazeti hili nimekataa katakata kuingia katika mtego wa kuwa mateka wa kundi lolote lile ndani ya CCM. Juhudi kubwa ambazo zimekuwa zikifanywa na makundi yote hayo mawili ya kutaka kuliingiza gazeti hili na mimi mwenyewe katika harakati za moja kwa moja za mojawapo ya makundi hayo mawili nimekuwa nikizikataa kwa nguvu kubwa. Nimekataa kuwa wakala wa makamanda wa ufisadi ambao wamekuwa na ajenda za kuwashambulia wale wanaowaita mafisa na wakati huo huo nimekataa katakata kuwa mouthpiece ya majeruhi wa ufisadi ambao kila mara wamekuwa wakipambana kuwashambulia hao wanaojiita makamanda wa ufisadi.

Natambua vyema kwamba informer ambaye yuko katika payroll ya kifisadi ya kundi la makamanda wa ufisadi amekuwa akilipwa kwa kazi ya kuwachafua watu wa upande mwingine. Huyu Bwana ambaye tunafahamiana vizuri kwa kuwa tumefanya naye kazi za kihabari kwa muda mwingi na ambaye katika jukwaa hili anatumia zaidi ya majina 10 bandia amekuwa wakala wa ile idara ya kishushushu ya umma inayomlipa fedha kila mwezi kwa kazi maalum ya kuwachafua watu wa kundi jingine. Jitihada zao za kuniingiza katika kundi hilo wakimtumia yule mzee wao mwenye mvi zimegonga ukuta siku zote na kimsingi hizo ndizo hasira zao juu ya msimamo wangu katika masuala yanayohusu mustakabali wa taifa letu.

Ni kutokana na kusimamia misingi hiyo ndiyo maana baada ya habari zinazomhusu Lowassa kuandikwa kwanza kupitia Raia Mwema na baadaye Kulikoni, tuliona ni muhimu kumtafuta Lowassa ili kusikia maoni yake kuhusu habari hizo. Kwa kuwa Lowassa anatambua fika msimamo wangu kuhusu mapambano yao ya kimakundi ndani ya CCM alichukua jukumu la kujiridhisha kwangu kwamba kile atakachohojiwa na kukieleza kitaandikwa pasipo kupotoshwa kwa malengo ya wapinzani wake. Tulipomhakikishia hilo akakubali kuhojiwa na sisi na sisi tukaiandika habari ile katika misingi ya kihabari na pasipo kutia chumvi za namna yoyote zenye mwelekeo wa kumsafisha.

Ni wazi kwamba tunaweza kujadili hili la kumwita Lowassa Waziri Mkuu mstaafu au Waziri Mkuu aliyejiuzulu. Nalitambua shinikizo linaloongozwa na mzee wetu ninayemheshimu sana na adui mkubwa wa Lowassa ambaye siku zote amekuwa akikerwa na maamuzi yetu (Tanzania Daima) ya kumuita Lowassa Waziri Mkuu mstaafu. Msingi wetu wa kutumia maneno hayo ni rahisi kabisa. Huyu mtu anapewa hadhi zile zile wanazopewa akina Malecela, Warioba, Sumaye, Salim na Msuya. Yuko kwenye orodha rasmi ya mawaziri wakuu wastaafu. Analipwa kama waziri mkuu mstaafu etc. Kwa kumwita mstaafu haina maana hata kidogo kwamba tunasahau ukweli kwamba kuondoka kwake kulikuja kwa njia ya kujiuzulu.

Ni jambo la bahati mbaya sana kwamba sikuzote nimekataa kuwa mwandishi wa habari mwanaharakati anayeandika habari kwa mtazamo wa chuki dhidi ya fulani na ushabiki dhidi ya mwingine. Tumeandika na kuzipa uzito unaostahili habari zinazohusu wanasiasa wa aina ya Sitta, Mwakyembe na wengine wote ambao ni makamanda wa ufisadi. Ni jambo la kushangaza kwamba kila tunapofanya hivyo huwa tunaonekana tumetimzia wajibu inagwa tukifanya hivyo kwa watu wa aina ya Lowassa na Rostam tunaonekana tunawasafisha watu fulani.

Hata hivyo kinyume cha mapenzi ya marafiki zangu ambao wako kwenye payroll ya mzee wangu anayewatuma kuwachafua wapinzani wake, ninayo furaha na amani moyoni kwamba siko katika payroll yoyote ya mtu au kikundi cha chatu chenye kazi ya kusafisha au kuwachafua watu fulani fulani katika jamii. Nachelea kusema kwamba, aina ya uandishi wa kujitambulisha kuwa katika moja kati ya makundi hayo mawili ni uandishi wa hovyo kabisa.

Sisi wa Tanzania Daima tunatembea kifua mbele kwa kuwa msimamo wetu thabiti unatuwezesha kuinua simu wakati wowote kumpigia Sitta, Mwakyembe, Lowassa, Rostam, Mbowe, Pinda, Kinana, Makamba, Mengi, Manji n.k. na kuwahoji kuhusu jambo lolote na tukaliandika habari pasipo kuegemea upande wowote. Tanzania Daima nililopewa dhamana ya kuliongoza si gazeti linaloegemea upande wowote hususan katika siasa za makundi hasa yale yaliyo ndani ya CCM au miongoni mwa wafanyabiashara. Tunajivunia uhuru wetu ambao kwa wengine ni kero. Hatutatikiswa na waandishi wanaotaka kutuingiza katika harakati ambazo tunatambua fika kwamba zimebeba dhamira chafu zilizojificha nyuma ya kivuli cha uzalendo na maslahi ya taifa wakati tukiujua ukweli kwamba huo pia ni ufisadi ambao miaka si mingi utafichuka.
 
Inaeleweka kuwa Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, Absalom Kibanda, ni rafiki wa karibu wa Lowassa na pia anafanya kazi kwenye magazine ya Lowassa inayoitwa UMOJA.

Uzushi mwingine Bwana. Jarida la UMOJA halimilikiwi na Lowassa ndugu yangu au unadhani umiliki wa jarida letu umejificha kama ule wa magazeti unayofanyia kazi wewe au lile ambalo wewe ni mkurugenzi uliyejificha! Hivi ndugu yangu unadhani utaendelea kuwapotosha Watanzania hadi lini Budha? Time will Tell.
 
Thanks kwa information its about time tunajua ukweli upo wapi... Hizi smear propaganda naona zimekuwa nyingi
 
Nilikuwanatazama Channel ten kipindi cha mahojiano nilishangaa jinsi Kibanda alivyokuwa akimponda Sitta kwamba alisababisha anguko la CCM kwa kuruhusu mijadala ya EPA na RICHMOND kujadiliwa mjengoni.Maoni ya Kibanda ni kwamba CCM ilifanya vyema kumtosa kwenye Uspika na haitakuwa rahisi JK kumteua kwenye baraza la mawaziri..[/SIZE][/FONT][/B]

Huu ni uzushi. Nadhani upeo wako wa kuelewa mambo mdogo. Nimeutazama tena mkanda wa mazungumzo yangu Channel ten, sikumponda Sitta na wala sikuzungumzia uteuzi katika serikali. Nilichosema kiko bayana kwamba, Sitta alijigharimu mwenyewe ndani ya CCM na nikasema nashangaa anabaki anafanya nini ndani ya chama ambacho kimsingi yeye ni mpinzani
 
Hii ndiyo gharama ya kuwa mkweli dhidi ya vibaraka waliojitwika joho la ushujaa, wala rushwa wakubwa ndani ya vyumba vya habari waliojitwalia sifa za watu safi kwa sababu ya kuishi kwa njia ya kuwarubuni watu.
 
Mkuu Kibanda,

Binafsi sikufahamu na pia sio msomaji wa Tanzania Daima. Lakini kama ulichoandika hapo ndio msimamo wako basi hongera sana.

Watanzania wamegeuka kuwa mabingwa wa majungu na watu wa kuchafua wengine bila hata tone la ushahidi na bahati mbaya magazeti mengi yamekuwa yakitumika kufanya hiyo kazi. Watu kama hao wanadhalilisha hata fani yao ya uandishi wa habari.
 
Mimi mwenyewe nikiwa ni mwandishi wa habari, nimeshtushwa, nimeshangaa na kupigwa butwaa na kitendo cha gazeti la Tanzania Daima, ambalo linamilikiwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, kutumika kumsafisha Edward Lowassa.

Informer,

Je wewe ni mwandishi wa gazeti gani? Ni vizuri kulijua gazeti unaloandikia ili tujue kama wewe ni tofauti na hao unao watuhumu.
 
Nimesoma maoni ya wanajamii. Hii si mara ya kwanza kwa Kibanda ambaye ni mimi kuingia katika msukosuko wa kushambuliwa hasa ninapogusa hisia za watu au taasisi kupitia katika safu yangu ya 'TUENDAKO' au kupitia maandishi katika gazeti la Tanzania Daima ambalo mimi ni mwajiriwa wake.

KUCHAFUA

Kwanza napenda kusema bayana kwamba 'kusafisha' na 'kuchafua' ni misamiati ambayo siku zote nimesimama kidete kukabiliana nayo kwa maneno, maandishi na matendo. Ninaamini tena kwa dhati kabisa kwamba, wajibu wangu wa msingi kama mwanahabari ni kuhakikisha kuwa siku zote niko juu ya siasa za makundi hususan yale yaliyo ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Msimamo wangu huo nimeuweka bayana katika majukwaa mbalimbali ya kihabari na kitaaluma. Ni kwa kuwa na imani hiyo ndiyo maana maandishi yangu, hususan yale ya kupitia katika safu yangu yamekuwa above political inclinations ambazo katika zama hizi zinatawaliwa na kuongozwa na matakwa ya makundi ya akina Samuel Sitta (kwa upande mmoja) na Edward Lowassa (kwa upande wa pili).

Kwangu mimi tatizo ni ufisadi na kwamba miongoni mwa wanasiasa wa ndani ya CCM waliopata kushika nyadhifa za juu kama za uwaziri, uspika na ubunge kupitia katika chama hicho hakuna hata mmoja mwenye ubavu wa kumnyoshea kidole mwingine kwa ufisadi.

Ni kwa sababu hiyo basi, Tanzania Daima, gazeti ambalo nimepewa dhamana ya kuliongoza limekuwa huru kuwasifu inapobidi na kuwaponda inapolazimu wanasiasa wa makundi yote ndani ya CCM wawe ni wale wanaojiita makamanda wa ufisadi au wale majeruhi wa ufisadi. Nikiwa kiongozi wa gazeti hili nimekataa katakata kuingia katika mtego wa kuwa mateka wa kundi lolote lile ndani ya CCM. Juhudi kubwa ambazo zimekuwa zikifanywa na makundi yote hayo mawili ya kutaka kuliingiza gazeti hili na mimi mwenyewe katika harakati za moja kwa moja za mojawapo ya makundi hayo mawili nimekuwa nikizikataa kwa nguvu kubwa. Nimekataa kuwa wakala wa makamanda wa ufisadi ambao wamekuwa na ajenda za kuwashambulia wale wanaowaita mafisa na wakati huo huo nimekataa katakata kuwa mouthpiece ya majeruhi wa ufisadi ambao kila mara wamekuwa wakipambana kuwashambulia hao wanaojiita makamanda wa ufisadi.

Natambua vyema kwamba informer ambaye yuko katika payroll ya kifisadi ya kundi la makamanda wa ufisadi amekuwa akilipwa kwa kazi ya kuwachafua watu wa upande mwingine. Huyu Bwana ambaye tunafahamiana vizuri kwa kuwa tumefanya naye kazi za kihabari kwa muda mwingi na ambaye katika jukwaa hili anatumia zaidi ya majina 10 bandia amekuwa wakala wa ile idara ya kishushushu ya umma inayomlipa fedha kila mwezi kwa kazi maalum ya kuwachafua watu wa kundi jingine. Jitihada zao za kuniingiza katika kundi hilo wakimtumia yule mzee wao mwenye mvi zimegonga ukuta siku zote na kimsingi hizo ndizo hasira zao juu ya msimamo wangu katika masuala yanayohusu mustakabali wa taifa letu.

Ni kutokana na kusimamia misingi hiyo ndiyo maana baada ya habari zinazomhusu Lowassa kuandikwa kwanza kupitia Raia Mwema na baadaye Kulikoni, tuliona ni muhimu kumtafuta Lowassa ili kusikia maoni yake kuhusu habari hizo. Kwa kuwa Lowassa anatambua fika msimamo wangu kuhusu mapambano yao ya kimakundi ndani ya CCM alichukua jukumu la kujiridhisha kwangu kwamba kile atakachohojiwa na kukieleza kitaandikwa pasipo kupotoshwa kwa malengo ya wapinzani wake. Tulipomhakikishia hilo akakubali kuhojiwa na sisi na sisi tukaiandika habari ile katika misingi ya kihabari na pasipo kutia chumvi za namna yoyote zenye mwelekeo wa kumsafisha.

Ni wazi kwamba tunaweza kujadili hili la kumwita Lowassa Waziri Mkuu mstaafu au Waziri Mkuu aliyejiuzulu. Nalitambua shinikizo linaloongozwa na mzee wetu ninayemheshimu sana na adui mkubwa wa Lowassa ambaye siku zote amekuwa akikerwa na maamuzi yetu (Tanzania Daima) ya kumuita Lowassa Waziri Mkuu mstaafu. Msingi wetu wa kutumia maneno hayo ni rahisi kabisa. Huyu mtu anapewa hadhi zile zile wanazopewa akina Malecela, Warioba, Sumaye, Salim na Msuya. Yuko kwenye orodha rasmi ya mawaziri wakuu wastaafu. Analipwa kama waziri mkuu mstaafu etc. Kwa kumwita mstaafu haina maana hata kidogo kwamba tunasahau ukweli kwamba kuondoka kwake kulikuja kwa njia ya kujiuzulu.

Ni jambo la bahati mbaya sana kwamba sikuzote nimekataa kuwa mwandishi wa habari mwanaharakati anayeandika habari kwa mtazamo wa chuki dhidi ya fulani na ushabiki dhidi ya mwingine. Tumeandika na kuzipa uzito unaostahili habari zinazohusu wanasiasa wa aina ya Sitta, Mwakyembe na wengine wote ambao ni makamanda wa ufisadi. Ni jambo la kushangaza kwamba kila tunapofanya hivyo huwa tunaonekana tumetimzia wajibu inagwa tukifanya hivyo kwa watu wa aina ya Lowassa na Rostam tunaonekana tunawasafisha watu fulani.

Hata hivyo kinyume cha mapenzi ya marafiki zangu ambao wako kwenye payroll ya mzee wangu anayewatuma kuwachafua wapinzani wake, ninayo furaha na amani moyoni kwamba siko katika payroll yoyote ya mtu au kikundi cha chatu chenye kazi ya kusafisha au kuwachafua watu fulani fulani katika jamii. Nachelea kusema kwamba, aina ya uandishi wa kujitambulisha kuwa katika moja kati ya makundi hayo mawili ni uandishi wa hovyo kabisa.

Sisi wa Tanzania Daima tunatembea kifua mbele kwa kuwa msimamo wetu thabiti unatuwezesha kuinua simu wakati wowote kumpigia Sitta, Mwakyembe, Lowassa, Rostam, Mbowe, Pinda, Kinana, Makamba, Mengi, Manji n.k. na kuwahoji kuhusu jambo lolote na tukaliandika habari pasipo kuegemea upande wowote. Tanzania Daima nililopewa dhamana ya kuliongoza si gazeti linaloegemea upande wowote hususan katika siasa za makundi hasa yale yaliyo ndani ya CCM au miongoni mwa wafanyabiashara. Tunajivunia uhuru wetu ambao kwa wengine ni kero. Hatutatikiswa na waandishi wanaotaka kutuingiza katika harakati ambazo tunatambua fika kwamba zimebeba dhamira chafu zilizojificha nyuma ya kivuli cha uzalendo na maslahi ya taifa wakati tukiujua ukweli kwamba huo pia ni ufisadi ambao miaka si mingi utafichuka.

It is very easy to write all sort of good and believable things, also its is easy to swear and look innocent before accuser that is an old trick that every thief does.

I commend you being fair and open like this, if this is true, then is good for you and like you have said time will tell

I remember your well narrated article of "NALIONA ANGUKO LA ZITTO", I fail to forget your remerkable part in all those 'elections' within chadema including your stands on that particular moments. I forget not your fully participation of abusing the democracy which you never played a role to zip up your mouth or not disallowing your hands not to write anything.

IF someone asks me where to place you, YES you belong to chadema where democracy is not in their brains but in their mouth. That to say I fail to believe your defence not because it is not understandable, but because your history hunts you on.
 
you are all behind the scine! mbona Kubenea wa Mwana halisi,semtawa wa mwananchi wapo kwenye pay roll ya mengi na Membe na wote hao kila siku waandikapo taarifa zao juu ya ama kuwachafua wengine au kuwasifia Membe na Mengi hakuna anayeulizia hilo au ndo ule msemo wa kiswahili kuwa kunya anche kuku akinya bata kaharisha? na zaidi zipo taarifa sahihi za mtu wa usalama wa Taifa nayefanya kazi ya kila mwezi kuwanunua waandishi wa habari kwa interest za 2015
live kibanda alone!
 
On Waberoya

How could you remember someone in relation to his writing while you could not remember exactly what he wrote. It seems you just remember the title of my opinion 'Naliona Anguko la Zitto' and not the content.

First you must understand that being a journalist and political commentator i'm entitled to write my views on issues of national interest. I warned Zitto not to vie for the position then not because I was against him, but because of the political climate within Chadema then. I insisted and I still insist that it was wrong for Zitto to vie for the position at that time. The wounds of his decision haunts him and Chadema to-date. I thank God that Zitto and Chadema elders saw it then and his decision to pull out his name has enabled that party to grow against all odds.

Unless you do not know Tanzanian politics well. Had it not been Mbowe as a chairman today, Dr. Slaa wouldn't have vied for the presidency in October elections, henceforth the party you seems to hate most wouldn't have been stronger and the champions of the opposition politics as it is now. Watch out your sense of arguments. Next time you need to be more smarter.
 
Back
Top Bottom