Kwani kuna tofauti gani kati ya mbowe na chadema? Chadema ni mali ya mkwe wake kwahiyo ni mali yake pia na gaazeti pia ni mali yake unauliza kitu gani?
Informer,
Je wewe ni mwandishi wa gazeti gani? Ni vizuri kulijua gazeti unaloandikia ili tujue kama wewe ni tofauti na hao unao watuhumu.
Kibanda je kweli wewe ni mhariri wa magazeti ya Umoja?Huyu jamaa informer ni mwandishi wa magazeti ya ThisDay na Kulikoni. Aidha anaandikia pia gazeti la Raia Mwema na wakati mwingine huandikia MwanaHalisi. Siku zote amekuwa mchimvi na mnafiki.
On Waberoya
How could you remember someone in relation to his writing while you could not remember exactly what he wrote. It seems you just remember the title of my opinion 'Naliona Anguko la Zitto' and not the content.
First you must understand that being a journalist and political commentator i'm entitled to write my views on issues of national interest. I warned Zitto not to vie for the position then not because I was against him, but because of the political climate within Chadema then. I insisted and I still insist that it was wrong for Zitto to vie for the position at that time. The wounds of his decision haunts him and Chadema to-date. I thank God that Zitto and Chadema elders saw it then and his decision to pull out his name has enabled that party to grow against all odds.
Unless you do not know Tanzanian politics well. Had it not been Mbowe as a chairman today, Dr. Slaa wouldn't have vied for the presidency in October elections, henceforth the party you seems to hate most wouldn't have been stronger and the champions of the opposition politics as it is now. Watch out your sense of arguments. Next time you need to be more smarter.
Huyu jamaa informer ni mwandishi wa magazeti ya ThisDay na Kulikoni. Aidha anaandikia pia gazeti la Raia Mwema na wakati mwingine huandikia MwanaHalisi. Siku zote amekuwa mchimvi na mnafiki. Ni mtu ambaye mnapozungumza kama marafiki huonekana kuwa ni mtu mwema sana na mwenye busara wakati ukweli ni kwamba amejawa chuki na uchimvi wa namna nyingi. Amekuwa informer katika system akiripotia habari za ndani zinazohusu wakubwa wengi ndani ya nchi hii. Nimepata kufanya naye kazi katika chumba kimoja cha habari na ukitukuta pamoja unaweza ukadhani sisi ni marafiki wakubwa. Huyu mtu haoni tabu kabisa kukuzushia jambo lolote na katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ameshiriki kikamilifu kuzusha mambo mengi. Chini ya zulia anawasilisha maslahi yasiyo yake bali ya tajiri mmoja ambaye ana hasira na watu wengi wanaokwenda kinyume chake. Ni mtu asiye na rafiki wa kudumu kutokana na tabia yake ya uchimvi. kwa kifupi kwa hulka ni multi dealer kwani ameshavuka daraja la kuwa double dealer.
Nilikuwanatazama Channel ten kipindi cha mahojiano nilishangaa jinsi Kibanda alivyokuwa akimponda Sitta kwamba alisababisha anguko la CCM kwa kuruhusu mijadala ya EPA na RICHMOND kujadiliwa mjengoni.Maoni ya Kibanda ni kwamba CCM ilifanya vyema kumtosa kwenye Uspika na haitakuwa rahisi JK kumteua kwenye baraza la mawaziri.
Bahati nzuri au mbaya kwake Sitta kapewa uwaziri sijui atajisikiaje.Mara kadha nilikuwa nalishangaa gazeti la Tanzania Daima lilivyokuwa likijitahidi kuwapiga nyundo wapiganaji Sendeka,Mwakiembe,Kilango na Seleli kuna siku nilimuuliza mwanahabari msimamo wa Tanzania daima alibaki akinicheka.The Informer pengine umechelewa mno kugundua Tanzania Daima ni gazeti linalomilikiwa na Freeman Mbowe kuisaidia CHADEMA lakini wakati huo huo kuwajenga mafisadi walioko ndani ya CCM.Unaweza kujiuliza kulikoni mwenye majibu yasiyo na ukakasi ni Mbowe mwenyewe.
Nakubaliana na wewe kwa 1oo%. Kwa takribani kama miaka miwili sasa hali ya Kibanda imebadilika sana . Kibanda wa sasa si yule wa zamani, ni wazi anatumika.