Gazeti la Freeman Mbowe latumika kumsafisha LOWASSA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gazeti la Freeman Mbowe latumika kumsafisha LOWASSA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The Informer, Nov 27, 2010.

 1. T

  The Informer Senior Member

  #1
  Nov 27, 2010
  Joined: Jun 14, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi mwenyewe nikiwa ni mwandishi wa habari, nimeshtushwa, nimeshangaa na kupigwa butwaa na kitendo cha gazeti la Tanzania Daima, ambalo linamilikiwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, kutumika kumsafisha Edward Lowassa.

  Pamoja ni kweli kuwa Mbowe anasifika kwa kutoa uhuru kwa wahariri wake na huwa haingilii editorial independence ya newsroom, naona sasa gazeti hili limekwenda too far.

  Tanzania Daima la leo Jumamosi Novemba 27, 2010, kina habari kwenye ukurasa wa mbele yenye kichwa cha habari: "Lowassa: Nimechoka kuzushiwa. * Mwanaye ajipanga kuchukua hatua za kisheria kujisafisha."

  Kwenye habari hiyo, gazeti la Tanzania Daima kwa makusudi kabisa linamuita Lowassa Waziri Mkuu "mstaafu."

  Huu ni upotoshaji wa makusudi kwani taifa zima linajua Lowassa kamwe hakustaafu, alilazimika kujiuzulu mwaka 2008 baada ya kuhusishwa na kashfa ya ufisadi ya Richmond.

  Kitendo cha Tanzania Daima kumuita Lowassa kimakosa kwa makusudi kuwa ni Waziri Mkuu "mstaafu" kina lengo maalum ya kumuweka mwanasiasa huyu aliyechafuka kwenye kundi moja kama mawaziri wakuu wa zamani waliostaafu kiheshima kama Cleopa David Msuya, Salim Ahmed Salim, Joseph Warioba, John Malecela na Frederick Sumaye.

  Ukweli utabaki palepale kuwa Lowassa ni waziri mkuu "aliyejiuzulu" kwa kashfa ya ufisadi na si "mstaafu."

  Kwenye habari hiyo inayombeba waziwazi Lowassa, hakuna sehemu popote ambapo kashfa ya Richmond inatajwa wala mazingira ya Lowassa kutoka serikalini kuelezwa.

  Badala yake, gazeti hili limetoa platform prominently kwenye ukurasa wa kwanza kwa Lowassa kueleza kuchoshwa kwake "kuzushiwa" mambo na kusisitiza kuwa yeye hajatoswa na Kikwete na wala alikuwa hataki nafasi yoyote ya uwaziri.

  Pia, gazeti hilo limetumika kama mouthpiece kwa kutoa fursa ndefu kwa Lowassa kumtetea mtoto wake Frederick, ambaye aliripotiwa na gazeti la RAIA MWEMA la wiki hii kuwa anachunguzwa na polisi Uingereza kwa tuhuma za money laundering baada ya kununua nyumba huko UK yenye thamani ya shilingi bilioni 1/-.

  Inaeleweka kuwa Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, Absalom Kibanda, ni rafiki wa karibu wa Lowassa na pia anafanya kazi kwenye magazine ya Lowassa inayoitwa UMOJA.

  Hivi mmiliki wa Tanzania Daima, Freeman Mbowe, anaelewa kuwa gazeti lake limekuwa likitumika mara kwa mara kumsafisha Lowassa na swahiba wake Rostam Aziz?

  Kama jibu ndiyo, kwa nini anaachia hali hii na kuendelea kuwa na Mhariri Mkuu Kibanda mwenye conflict of interest kwa kuwa pia ameajiriwa na Lowassa?
   
 2. d

  dotto JF-Expert Member

  #2
  Nov 27, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Astaafu au ajiuzuru bado ni kituko tu katika nchi hii.
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Nov 27, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hujui alistaafu kwa manufaa ya umma
   
 4. a

  asha ngedere Member

  #4
  Nov 27, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Nakushangaa wewe unajiita Informer halafu hujui, tena ni mwandishi wa habari. Hivi hujui kwamba watu wamo kwenye payroll ya Lowassa na Rostam? Au hujasikia kwamba Kibanda (Mhariri Mtendaji) ndiye atakayekuwa Mhariri Mtendaji wa gazeti lijalo la Lowassa? Kama ulikuwa hujui, ndo nakupasha upashike, maana siye tuko mtaani lakini tumezinasa. Ofisi tayari imepatikana tangu mwaka jana, iko mikocheni, timu ya waandishi inaandaliwa na Kibanda. awali lilikuwa lianze Oktoba, wakasema Desemba Mosi, wakasema Mei, sasa sijui wanasubiria nini!? lakini HABARI NDIO HIYOOOOOO, USISHANGAE KIBANDA AKIMSAFISHA LOWASSA NDANI YA TANZANIA DAIMA KWA SABABU HUYO NI BOSI WAKE MTARAJIWA!!!!!!
   
 5. Absolute

  Absolute JF-Expert Member

  #5
  Nov 27, 2010
  Joined: Jan 19, 2007
  Messages: 335
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Am a bit mixed up, kwani hilo gazeti ni la mbowe au CHADEMA? Tafazali naombeni jibu.
   
 6. F

  Fareed JF-Expert Member

  #6
  Nov 27, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kiongozi hustafishwa na Rais kwa manufaa ya umma. There is no such thing as mtu kustaafu kwa hiari kwa manufaa ya umma. Lowassa ni waziri mkuu aliyejiuzuru. Let's call a spade a spade.

  Pia wewe The Informer uko behind the news sana. Mbona kina Lowassa na Rostam wamekuwa wakilitumia Tanzania Daima kwa siku nyingi sana kujaribu kujisafisha ili angalau habari hizo ziaminike kwa vile zimeandikwa na gazeti "huru." Wanajua fika kuwa watu siku hizi wameyadharau magazeti yanayomilikiwa na Rostam Aziz -- RAI na MTANZANIA -- na wameacha kabisa kuyasoma.
   
 7. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #7
  Nov 27, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  poor kibanda unajidhalilisha
   
 8. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #8
  Nov 27, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo tuseme alijiuzuru kwa manufaa ya umma maana kuendelea kuwepo pale ulikuwa mzigo kwa umma
   
 9. F

  Fareed JF-Expert Member

  #9
  Nov 27, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Haswaaaa!....
   
 10. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #10
  Nov 27, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kwani kuna tofauti gani kati ya mbowe na chadema? Chadema ni mali ya mkwe wake kwahiyo ni mali yake pia na gaazeti pia ni mali yake unauliza kitu gani?
   
 11. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #11
  Nov 27, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mpaka sasa ni mzigo kwa umma maana ana ulinzi na anagharamikiwa na serikali kama Waziri Mkuu mstaafu ndio maana JK aliamua amwambie ajiuzulu ili aendelee kula bata
   
 12. Absolute

  Absolute JF-Expert Member

  #12
  Nov 27, 2010
  Joined: Jan 19, 2007
  Messages: 335
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkwe?
  Oooh nimekupata... hope you mean yule Honorable - Mwasisi

  Asante sana mkuu
   
 13. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #13
  Nov 27, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kwani wewe hujui? as wakati jamaa anapewa uenyekiti inasemekana Mwasisi alisema hawawezi kumpa Zitto "someone from no where" ndio akampa "someone from somewhere" ili aendelee kuwa remote wadanganyika na ndio maana unaona hata waliopo juu madarakani wengi wao wanakeofu ya mzee mwenyewe "someone from somewhere we know"
   
 14. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #14
  Nov 27, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,365
  Likes Received: 7,000
  Trophy Points: 280
  akustahafu, bali alijiuzuru kwa manufaa ya umma na yake mwenyewe binafsi
   
 15. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #15
  Nov 27, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Inabidi sheria iangaliwe upya mtu akijiuzuru asipewe hayo malupu lupu hiyo ni sawa sawa na kufukuzwa kazi
   
 16. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #16
  Nov 27, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hivi siku zote nnvyowaambia kuwa Mbowe ni system nyinyi hamuamini?
   
 17. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #17
  Nov 27, 2010
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hata kama ingekuwa mali ya mke wake katiba ya chma si-ipo? Hatu angalii mali za mtu ila kazipataje kama halali ni haki yake, tutatoa support kwake labda itokee vinginevyo. Tunahitaji watu wenye waliokomaa, wakikubaliana jambo kwenye kikao lenye maslahi kwa Taifa wabaki kuwa wamoja na walipiganie na kulitetea, siyo huyu akitoka kikaoni anajifanya kuwasaliti wenzake kwa kulopoka hovyo hovyo kwenye kadamnasi. People's power forever!
   
 18. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #18
  Nov 27, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Nilikuwanatazama Channel ten kipindi cha mahojiano nilishangaa jinsi Kibanda alivyokuwa akimponda Sitta kwamba alisababisha anguko la CCM kwa kuruhusu mijadala ya EPA na RICHMOND kujadiliwa mjengoni.Maoni ya Kibanda ni kwamba CCM ilifanya vyema kumtosa kwenye Uspika na haitakuwa rahisi JK kumteua kwenye baraza la mawaziri.

  Bahati nzuri au mbaya kwake Sitta kapewa uwaziri sijui atajisikiaje.Mara kadha nilikuwa nalishangaa gazeti la Tanzania Daima lilivyokuwa likijitahidi kuwapiga nyundo wapiganaji Sendeka,Mwakiembe,Kilango na Seleli kuna siku nilimuuliza mwanahabari msimamo wa Tanzania daima alibaki akinicheka.The Informer pengine umechelewa mno kugundua Tanzania Daima ni gazeti linalomilikiwa na Freeman Mbowe kuisaidia CHADEMA lakini wakati huo huo kuwajenga mafisadi walioko ndani ya CCM.Unaweza kujiuliza kulikoni mwenye majibu yasiyo na ukakasi ni Mbowe mwenyewe.
   
 19. F

  Fareed JF-Expert Member

  #19
  Nov 27, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Nakuunga mkono asilimia 100. Haiwezekani waziri mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya ufisadi kama Lowassa aendelee kulipwa mafao makubwa kama mawaziri wakuu waliostaafu kiheshima. Ni muhimu sheria hii ikaangaliwa upya. Kwani anaweza siku waziri mkuu akafukuzwa kazi kwa ufisadi, akapelekwa mahakamani na kuhukumiwa kwa wizi na bado akaendelea kupokea mafao akiwa keko. On second thought, hakuna haja ya kubadili sheria hii mpaka WILLIBROD SLAA akiwa Rais. Ni serikali gani ya CCM itamshitaki PM au Rais wake mstaafu?
   
 20. K

  Kiranja JF-Expert Member

  #20
  Nov 27, 2010
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 754
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mungu atunusuru na hili na lingine lijalo. Kuna siri nzito sana inakuja
   
Loading...