Gavana Ndulu(BoT): Kufungua akaunti maalum si kosa, fedha kuliwa ni vigumu

kweli kabisaa anatudanganya vitu ambavyo mtu kujua kama anadanganywa sio mpaka afauli darasa la nne ili kujua kama anatudanganya
ila mara nyingi yuko sahihi,kama lile suala la VAT kwenye miamala.Alisema ukweli na ndivyo ilivyokuwa,TRA wao walipotosha kumfurahisha Rais lakini Ndulu akasema ukweli kuwa gharama zitabebwa na mtumiaji na si mabank.
 
Seleboy2010 soma hii comment utaelewa.Nimesoma comment yako mpaka nikashika kichwa,yaani mawazo yako fixed deposit pesa inakaa tu bank imewekwa.
 
Planned ili ajibu hivyo then atumbuliwe ili paonekane pana uwajibikaji,ni game inachezwa,subirini mtasikia muda si mrefu,swali la uchokozi "kwani gavana atastaafu lini?"
 
Wengine tukipinga tuogopa kufanyiwa ya Lema. Nilishangaa speech ile kuitolea kwa wasomi wale Wa OUT na wao wakawa wanashangilia uamuzi ule; Nilishangaa sana.
Mkuu si umeshasema OUT! Ila kumbuka hata UDSM wakati akiwaita vijana wetu vi.. L... a... za walishangilia mkuu, siku hizi vijana wetu walioko vyuo vikuu ni magonjwa Mtambuka!!!
 
Bwana ndulu Fedha za Mradi zikiwekwa Fixed Account mzunguko wa fedha unahusikia vip maana hapo mimi navyojua hela zikiwa fixed hazitoki baada ya muda kazaa sasa huo muda tutazipata vip hizo fedha zituzungukie?
Du ndg yangu, yaani wewe hujui kuwa zinapowekwa FD kwenye benki hazifungiwi kwenye makabati Bali zinatumika kuwakopesha wanananchi na viwanda wanaokuja kukopa.
 
Rais hana idea na mambo ya uchumi, lakini nadhani na washauri wake wa mambo ya uchumi watakua vihio au ndio wale wale.

Anyway governor jiandae kutumbuliwa maana mukulu ukweli kwake ni tusi
 
Bado mi naamini mh Rais yuko sahihi...watu wachache walituchezea sana akili! hela imeletwa kwa ajili miradi mbalimbali ndani ya shirika we unaidhinisha iende fixed acc ili riba itakayopatikana uweke mfukoni.....asante sana mh Rais shikilia hapohapo ili na wao waishi kama "mashetani"!!!
 
Wengine tukipinga tuogopa kufanyiwa ya Lema. Nilishangaa speech ile kuitolea kwa wasomi wale Wa OUT na wao wakawa wanashangilia uamuzi ule; Nilishangaa sana.
Ndio wasomi wetu mkuu unategemea wale wakipewa kitengo si yatakua yale yale ya kina ndio mzee
 
Bwana huyu jamaa sijuii anaongea vitu gani maana hela zimewekwa fixed alafu anasema zinaongeza mzunguko jaman jaman muachen rais bhana ajakosea hata kidogo hapo kati ya huyo gavana na raisi gavana ndio anafanya pesa isitufikie huku
Kwani fedha zikiwekwa fixed unadhani benki wanazifungia ndani,zinazungushwa,zinakopeshwa zinaleta faida,acha umbumbumbu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…