Gavana Ndulu ahofia vijana Tanzania kuingia mitaani kama Misri! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gavana Ndulu ahofia vijana Tanzania kuingia mitaani kama Misri!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fareed, Mar 4, 2011.

 1. F

  Fareed JF-Expert Member

  #1
  Mar 4, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hili nalo neno...

  MGAO WA UMEME...

  Uchumi wayumba

  * Taifa lapoteza sh. trilioni 1 kwa mwezi
  * Hofu yatanda maelfu ya vijana kukosa ajira
  * Ukali wa maisha wawaacha Watanzania hoi
  * Serikali yang'ang'ania mchezo wa Dowans


  MWANDISHI WETU
  Dar es Salaam

  MGAO wa umeme unaoendelea umesababisha madhara makubwa kwa uchumi wa nchi, huku Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Benno Ndulu, akiweka bayana kuwa maelfu ya vijana wasio na ajira kwenye miji mikubwa kama Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya na Arusha, wanaweza kuiyumbisha taifa.

  Wakati makali ya mgao wa umeme yakiendelea, viongozi serikalini wanaonekana kuendelea kucheza 'mchezo mchafu' wa Dowans na kuiona mitambo ya kampuni hiyo tata kuwa suluhisho pekee la tatizo la nishati hapa nchini badala ya kufanya maamuzi mengine ya haraka.


  Macho yote ya serikali sasa hivi yako kwenye mitambo ya Dowans ambayo inauwezo wa kuzalisha megawati 100 tu wakati uhaba wa umeme ulipo ni megawati 260.

  "Tatizo tulionalo ni kuwa baadhi ya vigogo wa serikali na Bungeni wanatoa msukumo kwa mradi wa Dowans ili kufanikisha uporaji wa pesa za umma," mwanasheria mmoja aliye karibu na serikali ameiambia KuliKoni.

  "Eti wanataka taifa liione mitambo ya Dowans kuwa ndiyo mkombozi pekee wa uhaba mkubwa wa nishati nchini. Ukweli ni kuwa hata mitambo ya Dowans ikiwashwa leo, mgao wa umeme bado utaendelea."


  Akizungumza kwenye mkutano wa kimataifa wa uwekezaji uliofanyika Dar es Salaam mapema wiki hii, Gavana Ndulu amesema kuwa idadi kubwa ya vijana wasio na ajira kwenye miji mikubwa ya nchi ni tatizo linalo mkosesha usingizi.


  "Nina hofu na tabaka linalokuwa kwa kasi kubwa kuliko yote la masikini waliopo kwenye maeneo ya mijini, ambao ni vijana waliokuja kutafuta ajira lakini hawapati hizo ajira," alisema Ndulu.


  Katika ripoti yake mpya ya mwelekeo wa uchumi iliyotoka wiki hii (Monetary Policy Statement) Benki Kuu imeonya kuwa tatizo la umeme hapa nchini huenda likaleta madhara makubwa kwa uchumi.


  Benki Kuu imesema kuwa italazimika kuchukua hatua kadhaa kuhakikisha kuwa mgao wa umeme na ongezeko la bei ya umeme lilioanza Januari 1 mwaka huu hayaendelei kuleta madhara makubwa kwa uchumi.


  Gavana alisema kuwa ingawa lengo la serikali ni kwa uchumi kukua kwa asilimia 7.1 mwaka huu, kuna uwezekano kuwa lengo hilo lisifikiwe kutokana na hofu ya ukame na kupanda kwa bei ya mafuta kwenye soko la dunia.


  Kwa mujibu wa Prof. Ndulu, kuna uwezekano ukuaji wa uchumi ukashuka mpaka kufikia asilimia 6.5 mwaka huu kutoka wastani wa ukuaji uchumi wa wasilimia 7.0 mwaka jana.


  Baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanakiri kuwa kundi kubwa la vijana wasio na ajira wanatishia utawala wa serikali.


  "Vijana wengi maeneo ya mijini na kwenye vyuo vikuu wanaichukia sana CCM na serikali kutokana na hali ngumu ya uchumi na ukosefu wa ajira. Ndiyo maana wapinzani wameonekana kuwa na nguvu kwenye miji mikubwa hapa nchini," alisema kada mmoja wa CCM.


  Hivi karibuni, imetangazwa kuwa zaidi ya viwanda 50 vikubwa nchini vimefungwa huku vingine vingi vikilazimika kupunguza uzalishaji kutokana na makali ya mgao wa umeme unaoendelea.


  Hii ina maana kuwa maelfu ya vijana ambao walikuwa wanajipatia ajira kama vibarua kwenye viwanda hivi wameachwa solemba.


  Mfanya biashara na mchumi aliyebobea, Ali Mufuruki, ameonya wiki hii kuwa uchumi wa taifa unapoteza shilingi trilioni 1 kwa mwezi tangu mgao wa umeme uanze.


  Mufuruki ambaye ni mtendaji mkuu (chairman & CEO) wa kampuni ya uwekezaji ya Infotech Investment Group yenye makao yake makuu jijini Dar es Salaam,

  Makali ya maisha yanazidi kuwakamata Watanzania, huku mfumuko wa bei ukiendelea kupaa.

  Tayari bei za sukari, mafuta ya taa, mchele, sembe, maharage, mkate, nyama na mahitaji mengine muhimu zimekuwa zikiendelea kuongezeka kwa kasi siku hadi siku.


  Wadadisi wa masuala ya kisiasa wamesema kuwa ufisadi serikalini, ukosefu wa ajira na ukali wa maisha vimechangia kwa kiasi kikubwa kukisaidia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kujizolea umaarufu miongoni mwa Watanzania, wengi wao wakiwa ni vijana.


  Kutokana na hofu iliyopo serikalini kuwa vijana waliokata tamaa ya maisha wanaweza kuingia mitaani na kutaka kuleta mapinduzi ya wananchi kama yaliyofanyika Misri na kwingineko, Rais Kikwete ameonya kuwa amani ya nchi sasa iko hatarani.


  Katika hotuba yake kwa taifa hivi karibuni, Kikwete aliwashutumu viongozi wa CHADEMA kwa kupanga kuindoa serikali yake madarakani kwa kutumia mabavu.


  (Source: KULIKONI Toleo la Machi 4, 2011)
   
 2. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #2
  Mar 4, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Gavana alisema kuwa ingawa lengo la serikali ni kwa uchumi kukua kwa asilimia 7.1 mwaka huu, kuna uwezekano kuwa lengo hilo lisifikiwe kutokana na hofu ya ukame na kupanda kwa bei ya mafuta kwenye soko la dunia.
  SASA HIVI VISINGIZIO VIMEKUWA VINGI LAKINI KWA KWELI HAKUNA UBISHI UCHUMI UNAYUMBA
   
 3. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #3
  Mar 4, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Chadema inaelimisha na inafundisha hakuna ubishi itajizolea wanachama wengi tu!
   
 4. MANI

  MANI Platinum Member

  #4
  Mar 4, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Tatizo ni kuwa Pinda amesema kuwa pamoja na mgao uchumi unakuwa,sasa huyu gavana na pinda nani mkweli?
   
 5. Ole

  Ole JF-Expert Member

  #5
  Mar 4, 2011
  Joined: Dec 16, 2006
  Messages: 751
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ati serikali bado inaongelea swala la Dowans , huu ni ushahidi tosha JK ni mmiliki wa Dowans anafanya kila njia kila mbinu ili mitambo yake inunuliwe kwa njia yoyote ile. Mwacheni siku zke za kwenda kunyea debe zinahesabika.
   
 6. sijuikitu

  sijuikitu JF-Expert Member

  #6
  Mar 4, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sababu tunazo
   
 7. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #7
  Mar 4, 2011
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Hii ni moja ya matokeo rasmi ya namna CHADEMA inavyowaingia kichwani hata kwa watu kama gavana Ndulu.

  Mawazo yake yanakuja wakti muafaka kabisa kwani yanaonesha kwamba huko miaka ya nyuma chombo hiki cha benki kuu kimekuwa chini ya amri ya kwamba kiseme ni au kitoe taarifa gani na kwa namna ipi.

  Benki kuu yoyote duniani ni chombo kinachotakiwa kuwa "independent" katika kutoa muelekeo wa uchumi wa nchi kwa kueleza mambo kama jambo hili alilolisema bwana Ndulu ambalo naweza kuliweka kwamba ni CPI- Consumer Price Index kwamba uwezo wa wananchi kufanya manunuzi haupo kwa sasa na vijana Tanzania wana wakti mgumu.

  Wananchi wakiweza kuwa na fedha mfukoni na huku viashiria uchumi vyote vikiwa vipo sahihi basi hakutakuwa na matatizo.

  Lakini kama umeme unakatwa kila ifikapo saa kumi jioni basi hapo uchumi hamna Tanzania.

  Mzee Ndulu nampa tano kwa hili.
   
 8. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #8
  Mar 4, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Ndio wanagutuka??? What do you expect if 60% of youth in urban areas are unemployed (Wizara ya kazi statistics, 2006)???
   
 9. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #9
  Mar 4, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Hivi na wewe bado unamsikiliza pinda, yeye anasema alichotumwa tuu, ndo maana hata bungeni alitumwa akawashutumu Chadema lakini kwa bahati mbaya akaishia kupata aibu ya kudanganya bunge
   
 10. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #10
  Mar 4, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Amejaribu kuona mbali angalau kiduchu. HV ikulu wana mgao? kama hawana basi watugawie kidogo kama kwenye migodi walivyoshauriwa ili angalau hii adha kila mmoja wetu aonje wanjameni.

  Mr. Pres. JK angeonja hii hali lazima atakuwa creative kutoa tangible solution badala ya kusubiri kudura za mwenyenzi Mungu. Hivi Mkapa mbona alishalimaliza hili tatizo JK anaturudisha tena nyuma.
   
 11. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #11
  Mar 4, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Tunaelekea kuwa kama Zimbabwe kiuchumi.
   
 12. regam

  regam JF-Expert Member

  #12
  Mar 4, 2011
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 268
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Jamani naomba maelekezo nifanyeje ikiwa kiongozi mkuu wa taasisi kuu akionekana anadanganya watanzania nifanyeje?
  Pinda alisema pamoja na mgao wa umeme uchumi hautayumba! Naye ndulu anasema utayumba!
   
 13. F

  Felister JF-Expert Member

  #13
  Mar 4, 2011
  Joined: Aug 5, 2008
  Messages: 377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Duuh I wish I could finish the assignment I have ili nije kujipatia utajiri wa milele huku nikipunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la ajira kwa vijana maana ni bonge la consultancy...Its so strange katika nchi ambayo ardhi siyo tatizo, nyumba asilimia 80% ni mbovu bara bara zote in local places ni mbovu na population ya 40m plus yenye kuhitaji kula, kunywa na kuvaa, miji karibu yote ni michafu, kaya kadhaa hazina vyoo vyakudumu alafu Gavana anayelipwa pesa nyingi kupita raia wote Tz anakuja na hadithi ya anasikitika eti hakuna ajira...Sasa Rais afanye nini? Kama ni kazi amempatia na kama ni solution yeye ndo anatakiwa kuitoa then anarudisha paper ya exams kwa mtunga mtihani eti anasikitika hawezi kujibu maswali...Duuh sasa sijui kama wewe ndiyo mwl utamfanyaje huyo mtahiniwa ukasome badala yake alafu umjazie majibu ili yeye apate 100%? Wakati mwingine tuache ushabiki wa kisiasa Gavana hastahili wala sidhani kama anapaswa kuongea hayo maana kazi yake ni zaidi ya kufanya hayo mahesabu na kutuletea figures...nipamoja na kutoa majibu ya nini cha kufanya mpaka hapo hajafafanua jinsi atakavyo create jobs ili ku absorb hiyo presure...
   
 14. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #14
  Mar 4, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  ntahamia bukoba maana inaendeshwa na uganda , huko hamna mgao wa umeme na vijana kibao wanakimbilia south sudan. Pinda karibu lakini ukileta siasa tu yaliyomtokea Lowasa richmond Ukerewe nawe yatakukumba
   
 15. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #15
  Mar 4, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,148
  Likes Received: 1,882
  Trophy Points: 280
  Mkulo hajasema chochote?
  Naikumbuka ile sauti yake ya bembeleza toto baba taka lala eehee!
   
 16. s

  sitakuwafisadi Member

  #16
  Mar 4, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 62
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  MAISHA MAGUMU KILA KUKICHA HERI YA JANA KIKWETE HAJUI UGUMU WA MAISHA YETU ...!!..Usually
  when people are sad they don't do anything they just CRY over their
  condition but when they gel Angry they bring about a change" (MALCOLM X)
  .
   
 17. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #17
  Mar 4, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Pinda amezoea kusema uwongo. Unakumbuka bungeni ameumbuliwa na mheshimiwa Lema? On the other hand, Ndulu na timu yake wamefanya hini kusaidia kupunguza mfumuko wa gharama za maisha?
   
 18. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #18
  Mar 4, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Gavana kasema kweli, na hawa wanafik wa Chadema ndio opportunity wanayotumia ya kuwarubuni (brainwash) hawa vijana wasio na kazi maalum. Wanawadanganya kuwa Serikali iliyopo madarakani ikiondoka leo, kesho nyie wote mna kazi tena za kuwaongoza hawa tunaowatoa madarakani. Duhh, uongo mtupu!
   
 19. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #19
  Mar 4, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Dawa ya migomo ni maendeleo bila hivyo Vijana wataleta fujo tu na si lazima iwe leo lakini inakuja.
   
 20. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #20
  Mar 4, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  * Taifa lapoteza sh. trilioni 1 kwa mwezi

  Si nyinyi ndio mlipinga hii mitambo ya Dowans isinunuliwe?


  * Hofu yatanda maelfu ya vijana kukosa ajira

  Wasiokuwa na ajira ndio watapata ajira serikali hii ikiondoka? Ajira alizoahidi ni million moja, mpaka sasa kisha towa zaidi ya hizo.

  * Ukali wa maisha wawaacha Watanzania hoi

  Hoi kuliko wakati wa Nyerere? Hata viwembe vya kunyolea ilikuwa havipatikani! Ukikogea Lux, harufu tuu, unaonekana wa maana? Wakati upi hoi zaidi?

  * Serikali yang'ang'ania mchezo wa Dowans

  Mchezo upi wa Dowans? Jee, Dowans wanakosa lipi? Na inawahusu nini siasa yenu?

  Kwa nini mnaingiza matatizo ya umeme kwenye siasa? Kwani matatizo ya umeme yalianza kwa JK?

  Mlianza na kutomtambuwa Rais, mkaona hapa pagumu!

  Mkaja na Katiba, mkanuyamazishwa kiulaini.

  Mnakuja na Dowans, kaja mwenye Dowans bado hamtaki. Na majuha wanawasikiliza.
   
Loading...