Gavana ballali hajafa- source:gazeti la fahamu

Mwalimu Mkuu,

Wengine hatujaona hilo gazeti, unaonaje ukitupatia summary ya hiyo news, maana najua haliko mtandaoni na hivyo huwezi kutuwekea hapa habari nzima.

Kwenye mazishi nadhani kuna watu wa ubalozi wa Tanzania Washington DC walihudhuria ingawa hakuna aliyeruhusiwa kuona mwili wa marehemu.

Hayo maswala mengine ya kwamba serikali haikufuatilia hospitali aliyokuwa anatibiwa, sidhani kama ni sahihi maana aliugua akiwa Gavana wa Benki Kuu na lazima Benki Kuu ilikuwa inalipa gharama zake na bado aliendelea kupewa mshahara wake kama kawaida na pia hata barua ya kuomba kujiuzuru aliandika akiwa US. So, serikali ilikuwa inajua kila kitu ila haikutaka kuweka wazi may be kwa sababu zao wao wenyewe.

Lakini kuelekea 2015 kuna mengi sana yatafumka ili wale wanaowania kupeperesha bendera ya CCM kuelekea Magogoni waweze kumalizana wao kwa wao. CHADEMA kaeni mkao wa kupewa clues za ufisadi na inawezekana details zote zikawekwa wazi na hivyo unakuwa ni mtaji.

Mukama juzi amelia na Kamati za Bunge kwamba iweje tuhuma zinazojadiliwa kwenye Kamati ya Bunge zifike kwa waandishi wa habari kabla tuhuma hizo hazijafikishwa kwa Spika ili afanye maamuzi kama ziwe discuessed au la. Hatimaye akaropoka kwamba hizi zote ni njama za wanaotaka kuvuliwa magamba. Kwa hiyo joto ndani ya CCM ni kubwa sana na likiendelea hivi Mkapa akae mkao wa kueleweka maana ataumbuka tena na sijui ataficha wapi uso wake.

CCM ina hali mbaya sana kwa kuwa makundi yamekamiana, hata Mukama aliyekuwa anasema kuwa na makundi ni sawa, lakini victim mkubwa ni chama maana siasa za makundi zinaishia kukipaka matope chama chote na pia kuipaka matope serikali. Namna ya kuja kujinasua kutoka kwenye hilo tope itakuwa ngumu sana na mwisho wa siku wote watakosa. Ndugu zangu wa Morogoro wana msemo wa "kazopata", kwamba bora tukose wote maana ukipata utaringa sana na kututambia.
hapo kwenye red umenikumbusha mbali sana mkuu nimekulia moro
 
Balali amefariki na amezikwa FULLSTOP.
Ndugu zake wamelia sana na walishiriki katika maziko pia serikali na vyama vya kijamii na visivyokuwa vya kiserikali vilishiriki.
Kama mnataka picha tuweke hapa, na yupo mwanafamilia aliwahi kuelezea uchungu wake humu JF kwa wanaosema yupo Hai.
Wewe umeamini huo uchungu alioelezea? Hivi ukilipwa dola milioni moja ukapewa kazi ya kumlilia hadharani utashindwa? Mbona yule jamaa alijifanya kuzimia kule Igunga wakati RA alipojiuzulu alifaulu usanii wake, halafu eti ambulance ilikuwa hapo hapo karibu ikamchukua na waandishi wa habari wakapiga picha. Eti Ambulance ilikuwa mkutanoni Igunga ikingoja kuwahudumia watakaozimia.
Nchi yetu wacha Bwana. Pindi Wamarekani watakapogundua tulivyo wasanii hodari watahamisha makao makuu ya Hollywood yawe Dar-es-salaam.
 
Mwisho wa drama ya Balali utatokea siku atakapofariki kiukweli!
Hakuna uwongo unaoweza kuwa uwongo kwa watu wote kwa muda wote!
 
Balali amefariki na amezikwa FULLSTOP.
Ndugu zake wamelia sana na walishiriki katika maziko pia serikali na vyama vya kijamii na visivyokuwa vya kiserikali vilishiriki.
Kama mnataka picha tuweke hapa, na yupo mwanafamilia aliwahi kuelezea uchungu wake humu JF kwa wanaosema yupo Hai.

Nilikuwa na wasiwasi sana na uraia wako kutokana na jinsi unavyopost pumba humu! Sasa nimeamini we hauko tanzania, na wala historia ya matukio yaliyotokea Tz huijui. Mfano mzuri ni hii thread.

Kwani balali amezikwa TANZANIA! Mimi sio mtanzania mimi ni MZANZIBAR taifa linaloexist sio nyie watanganyika mmeuza nchi yenu!
 
Kuna maswali mengi mimi kama mtanzania nimekuwa nikijiuliza mazingira tata ya kifo, na kuzikwa kwa gavana wa bot, daud ballali. Leo gazeti la fahamu limenitegulia kitendawili kuwa ballali hajafa.

Najiuliza ni kwa nini serikali imepokea taarifa ya kifo cha ballali bila kufuatilia hospitali aliyokuwa anatibiwa huko marekani, mahali ulipofanyika msiba, na sehemu alipozikwa. Kama hilo ni gumu, watuonyeshe walau picha za mazishi.

Kama suala hili lina ukweli serikali ijiandae kuvuna aibu asubuhi.

Wadau wa jf, siri hii ina maanisha niiiini?

Nafikiri sisi tuamini kuwa amekufa maana sio kitu cha ajabu, angakuwa hai ingeshajulikana na angeshajitokeza nafikiri tusichoshe akili zetu kudadisi mambo ambayo yanatupotezea muda, maana hata angekuwapo kusingekuwa na jipya
 
:disapointed: Ndugu! bado unaumiza kichwa kuhusu Balali. Kibongobongo huyu mtu ameshakufa, hata akija leo serikali itasema "ni mzuka wake tu, wananchi msiogope"
 
Mtu kama gavana wa nchi kufa na kuzikwa "NCHI YA WATU, BILA HATA RAIS KUHUDHURIA MAZISHI AU MUWAKILISHI YEYOTE KUTOKA NCHINI ni danganya toto. Huku ni kutufanya Watanzaina ni wajinga hatujui kitu na hatuwezi kitu.
INAWEZEKANA KABISA KUWA BALALI YUKO HAI ANAFICHWA NA WAHUSIKA WA MAMBO FULANI.
 
Watawala/kikundi fulani ktk nchi hii kinatufanya wananchi kama wajinga fulani ambao wanaweza kukubali kudanganywa au kuamini uongo wao,haifai.
 
Mods hii thread tulishajadili wengine wakasema kaja TZ kabadilishwa sura
Mm naona kafa na kazikwa kwani mke watoto wasingekubali umaskini huu, tuliambiwa malori yake na biashara zake zilikuwa juu ya mawe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom