Gavana ballali hajafa- source:gazeti la fahamu

Head teacher

JF-Expert Member
Mar 10, 2012
1,796
411
Kuna maswali mengi mimi kama mtanzania nimekuwa nikijiuliza mazingira tata ya kifo, na kuzikwa kwa gavana wa bot, daud ballali. Leo gazeti la fahamu limenitegulia kitendawili kuwa ballali hajafa.

Najiuliza ni kwa nini serikali imepokea taarifa ya kifo cha ballali bila kufuatilia hospitali aliyokuwa anatibiwa huko marekani, mahali ulipofanyika msiba, na sehemu alipozikwa. Kama hilo ni gumu, watuonyeshe walau picha za mazishi.

Kama suala hili lina ukweli serikali ijiandae kuvuna aibu asubuhi.

Wadau wa jf, siri hii ina maanisha niiiini?
 
ww mgeni nchi hii? Au ndo mwl mkuu umewekewa iternet unaanza kuweweseka. Basi ujue nchi hii ni ya walangizi kitu kama hicho ni kawaida.
 
Baadhi ya maelezo kwenye gazeti hilo yanasomeka "... Akaunti zake Marekani zinafanya kazi"

mie huwa napata gadhabu sana mtu anapotoa hoja nusu nusu namna hii utafikiri kila anaesoma hii thread ameshikilia hilo gazeti mkononi! Kwa nini usikae chini upangilie thread yako vizuri kabla ya kupost? Sasa sisi wapita njia unafikili tutasoma hilo gazeti kwa kusadikika? Hebu mwaga kila kitu hapa ili tuchangie hii thread otherwise utakuwa mmbea!
 
Mwalimu Mkuu,

Wengine hatujaona hilo gazeti, unaonaje ukitupatia summary ya hiyo news, maana najua haliko mtandaoni na hivyo huwezi kutuwekea hapa habari nzima.

Kwenye mazishi nadhani kuna watu wa ubalozi wa Tanzania Washington DC walihudhuria ingawa hakuna aliyeruhusiwa kuona mwili wa marehemu.

Hayo maswala mengine ya kwamba serikali haikufuatilia hospitali aliyokuwa anatibiwa, sidhani kama ni sahihi maana aliugua akiwa Gavana wa Benki Kuu na lazima Benki Kuu ilikuwa inalipa gharama zake na bado aliendelea kupewa mshahara wake kama kawaida na pia hata barua ya kuomba kujiuzuru aliandika akiwa US. So, serikali ilikuwa inajua kila kitu ila haikutaka kuweka wazi may be kwa sababu zao wao wenyewe.

Lakini kuelekea 2015 kuna mengi sana yatafumka ili wale wanaowania kupeperesha bendera ya CCM kuelekea Magogoni waweze kumalizana wao kwa wao. CHADEMA kaeni mkao wa kupewa clues za ufisadi na inawezekana details zote zikawekwa wazi na hivyo unakuwa ni mtaji.

Mukama juzi amelia na Kamati za Bunge kwamba iweje tuhuma zinazojadiliwa kwenye Kamati ya Bunge zifike kwa waandishi wa habari kabla tuhuma hizo hazijafikishwa kwa Spika ili afanye maamuzi kama ziwe discuessed au la. Hatimaye akaropoka kwamba hizi zote ni njama za wanaotaka kuvuliwa magamba. Kwa hiyo joto ndani ya CCM ni kubwa sana na likiendelea hivi Mkapa akae mkao wa kueleweka maana ataumbuka tena na sijui ataficha wapi uso wake.

CCM ina hali mbaya sana kwa kuwa makundi yamekamiana, hata Mukama aliyekuwa anasema kuwa na makundi ni sawa, lakini victim mkubwa ni chama maana siasa za makundi zinaishia kukipaka matope chama chote na pia kuipaka matope serikali. Namna ya kuja kujinasua kutoka kwenye hilo tope itakuwa ngumu sana na mwisho wa siku wote watakosa. Ndugu zangu wa Morogoro wana msemo wa "kazopata", kwamba bora tukose wote maana ukipata utaringa sana na kututambia.
 
Akiuficha moto,moshi utamuumbua"kama kweli hajafa basi hatakufa tu!tutakuja kujua ukweli hemu tumwachie mungu ilo janga
 
Jamani napita maana habari hii ni kama tetesi,mleta habari ungeiweka kwa kina ingewa poa sana
 
Kuna maswali mengi mimi kama mtanzania nimekuwa nikijiuliza mazingira tata ya kifo, na kuzikwa kwa gavana wa bot, daud ballali. Leo gazeti la fahamu limenitegulia kitendawili kuwa ballali hajafa.

Najiuliza ni kwa nini serikali imepokea taarifa ya kifo cha ballali bila kufuatilia hospitali aliyokuwa anatibiwa huko marekani, mahali ulipofanyika msiba, na sehemu alipozikwa. Kama hilo ni gumu, watuonyeshe walau picha za mazishi.

Kama suala hili lina ukweli serikali ijiandae kuvuna aibu asubuhi.

Wadau wa jf, siri hii ina maanisha niiiini?

We Head Teacher,

Mbona unachekesha mno. Nani alikwambia kuwa Balali amekufa? Mbona mnazusha tuuu habari ambayo hamuijui? Jamaaa mbona anakula good time na anasikitishwa saana na wale wanaomwobea mabaya. Anajipanga kutoa tamko hivi karibuni.

Mduu
 
Balali amefariki na amezikwa FULLSTOP.
Ndugu zake wamelia sana na walishiriki katika maziko pia serikali na vyama vya kijamii na visivyokuwa vya kiserikali vilishiriki.
Kama mnataka picha tuweke hapa, na yupo mwanafamilia aliwahi kuelezea uchungu wake humu JF kwa wanaosema yupo Hai.
 
Nilikuwa na wasiwasi sana na uraia wako kutokana na jinsi unavyopost pumba humu! Sasa nimeamini we hauko tanzania, na wala historia ya matukio yaliyotokea Tz huijui. Mfano mzuri ni hii thread.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom