Hata kama hajafanyiwa baya, kuna kila sababu kama binadamu kuweka mahali japo kwa watu wa karibu taarifa zote sahihi ili "WAKATI MWAFAKA" ukweli ujulikane. NAAMINI mambo mengi yana walakini na Watanzania tunajikuta tukiburuzwa bila kufanya utafiti wa kutosha. Upo uwezekano wa kesho kukuta magazeti mengi yakaandika habari ya Ballali, lakini bado najiuliza je, kuna NINI hadi tufikie mahali pa serikali KUPWAYA KIASI CHA KUENDESHWA NA KISANII? MUTAKUJA KUKUBALIANA NA MIMI KWAMBA kutatokea taarifa za KISANII SANA
Kwanza nashukuru kwa hizi habari.
Lakini Jasusi sijui huo undani wa hii habari yako especially in Red, sijui ulikua karibu kiasi gani hadi ukaweza kupata habari hiyo.
Other´wise kama kwa namna moja ama ingine alikua poisoned na mtu yeyote katika kutaka kumtoa kafara. Ni muda mwafaka kwake kusema yaliyojiri ili hata ikitokea vinginevyo hao wahusika wa BOT waumbuke, vinginevyo na yeye yumo so anataka kufa na tai yake shingoni.
Ugua pole na karibu bongo tena wasikutishe, Bongo bado salama
Jambo la msingi uwe na kumbukumbu ama uwe unafuatilia bila kukosa ili usipoteze mtiririko.
Quote: Halisi
Hata kama hajafanyiwa baya, kuna kila sababu kama binadamu kuweka mahali japo kwa watu wa karibu taarifa zote sahihi ili "WAKATI MWAFAKA" ukweli ujulikane. NAAMINI mambo mengi yana walakini na Watanzania tunajikuta tukiburuzwa bila kufanya utafiti wa kutosha. Upo uwezekano wa kesho kukuta magazeti mengi yakaandika habari ya Ballali, lakini bado najiuliza je, kuna NINI hadi tufikie mahali pa serikali KUPWAYA KIASI CHA KUENDESHWA NA KISANII? MUTAKUJA KUKUBALIANA NA MIMI KWAMBA kutatokea taarifa za KISANII SANA
Duh! Kaazi kweli kweli! Utafiti gani tena unaotaka ufanywe vya kutosha!?
Ushahidi wa kutosha uliandikwa magazeti na hao wahusika walishindwa kuupinga huo ushahidi. Ripoti ya BOT inafanyiwa usanii eti iko kwenye mchakato! Ama kweli Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu! Halafu bado kuna watu wanataka kumtetea yule aliyekuwa kinara wakati $250 millioni zinapotea!
Chumvi, chumvi, chumviinazidishwa ndio maana, maana kuna vitu vingine lazima uwe karibu especially unapo nukuu maneno ya mtu "nakuhsauri usirudi tena huko Bongo" maana yake ulikuwepo otherwise msg delivered.
BowBow, humu ndani mara kwa mara uwe unasubiri kwanza maana hadi mtu anapoamua kuweka hard facts kama hizo, ujue ana uhakika na kwa kuwa humu ndani wengi hatutumii majina halisi (japo mimi ni Halisi) kama linalosemwa unajua zaidi ama unajua kinyume chake toa maelezo yako kupinga ama kuunga mkono lakini si vyema sana kutaka kujua chanzo. Pengine muda si mrefu utaelewa ni kwanini hata yanasemwa. Jambo la msingi uwe na kumbukumbu ama uwe unafuatilia bila kukosa ili usipoteze mtiririko. Kila la kheir
Mtaalamu, wenzi hawataki aje huko.. sasa wewe unataka aje ili kiwe nini?
Huyu Bwana hata akifa ni sawa tu
Maana tangu alipoondoka Tz alisema anaumwa na ni routine checkup
alizokuwa anafanyiwa But ghafla akasema atafanyiwa operation na sasa tunaambiwa mahututi pamoja na kuresign.
Cha kushangaza sio serikali, BoT wala familia yake inayosema chochote kuhusiana na ugonjwa unaomsumbua. Je sio danganya toto ya kukwepa kujibu tuhuma?
Kuna mahali kwenye thread moja walisema huyu bwana ndio kakimbia nchi na sasa tunaanza kuona ukweli.
Je kwa nini tusiamini kwamba yeye ni mmoja wapo wa mamafia wanaotumiwa na WB, IMF na mamafia wengine kuibia nchi masikini
Nitamuombea Dua Afe kabisa
Habari za kuthibitishwa zinasema kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Bw. Daudi Balali amejiuzulu wadhifa wake huo kutokana na sababu za kiafya.
Bowbow,
Kama unazo kumbukumbu sahihi, hata wakati Mwalimu anaelekea London 1999 serikali ilitangaza kuwa anakwenda "routine medical check up." Hata pale hali yake ilipokuwa inazidi kuwa mbaya Ikulu ya Mkapa ilikuwa inatuambia kuwa anaendelea vizuri na matibabu. Hiyo inaitwa "lugha ya kiserikali." You have to read between the lines.