Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,014
- 144,371
Sometimes huwa nawaza badala ya kulifanyia matengenezo gari la Lissu lillomiminiwa risasi zaidi ya 30 kama Tembo, ni bora gari lile likahifadhiwa mahali, ikiwezekana hata makao makuu ya chama, ili libaki kama kumbukumbu ya tukio lile la kusikitisha.
Wanaweza kutoa engine na vifaa vingine vya thamani na lile gari likachwa kama lilivyo ili kutunza kumbukumbu ya tukio lile.
Shambulio lile halikuwa shambulio kwa Lissu pekee,bali ilikuwa shambulio kwa watu wote wapenda demokrasia na wazalendo wa nchi hii.
Gari lile kama halijafanyiwa matengeneo na ukaamua kulihifadhi na hata kutoza kiasi kidogo cha fedha kama shilingi 500 kwa anaetaka kuliona, nina hakika watu watakuwa tayari kulipia na pengine kurudisha kiasi fulani cha fedha ya matibabu iliyotumiwa na chama ama familia kumuuguza.
Kwasababu uchunguzi bado,naamini hata lile gari litakuwa limeachwaaa kama lilivyo ili lije kutumika wakati wa uchunguzi na kuandaa ushahidi wa kupeleka mahakamani wakati ukifika.
Tukubali lile tukio halikuwa la kawaida na mpaka sasa limevuta hisia za watu wengi ndani na nje ya nchi kwahiyo ni muhimu liwekee kumbukumbu kadri inavyowezekana.