The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Familia ya Katibu Mwenezi wa CCM Mbeya Mjini, Philimon Mng'ong'o, imekumbwa na hofu baada ya watu wasiojulikana kuvamia nyumbani kwake usiku wa kuamkia Aprili 22, 2025 na kuchoma gari. Moto huo pia ulianza kushika sehemu za nyumba, lakini watu 11 waliokuwemo waliokolewa salama.
Mng'ong'o amesema tukio hilo limetokea wiki moja baada ya wizi wa tairi jipya la gari lake, lakini amekanusha kuhusisha matukio hayo na masuala ya kisiasa, akisema hana mgogoro na mtu yeyote.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga, amethibitisha tukio hilo na kueleza kuwa uchunguzi unaendelea ili kubaini wahusika na chanzo cha tukio.
Chanzo: Dream FM
Picha: Highlands FM