Gari/Shamba langu.....! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gari/Shamba langu.....!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kipenzi Chao, Mar 14, 2011.

 1. K

  Kipenzi Chao Member

  #1
  Mar 14, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 99
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Karibu mara zote watu wamekuwa wakichukua magari second hands na kuyafanya vifaa vyao vya maisha hadi kifo....! Magari mengine yanakuwa yakiibiwa kwa muda bila mwenyewe kushtukia kama gari lake linaibiwa, na baadaye akigundua basi watu wengine humkalisha chini na kumuona tena akiwa na amani na gari lake....! Wengine hushtukia lakini hukubaliana na hali hiyo, japo bila hiari yake, na kuendelea kukitumia akijua gari sio lake peke yake....! Wengine huamua kabisa kutumia maarifa, nguvu, na kila mbinu kuchukua gari la mwenzie, na kusishi nayo kwa furaha na amani kabisa.....! Wengine hawaridhiki na magari yao, hadi wameendesha magari ya wengine, walau mara moja, mbili, tatu.....! Wengine huchukuwa magari second hands, tena yaliyokwisha tumika kuoteshea mbegu na mbegu hiyo ikaota na kustawi....! Nao wanaishi kwa amani na furaha tele.....!

  Lakini mimi nimekuwa tofauti kidogo.....! Kila nikikumbuka nina gari/shamba second hand roho inataka kunitoka.....! Mbegu yangu nimeotesha na imeota, na pia inastawi vizuri sana....! Hakuna mtu mwingine aliyekwisha rutubisha mbegu zake na zikaota kama ilivyo kwa baadhi ya wale niliowashuhusia...!

  Sasa nawauliza wenye uzoefu wanisaidie hili.....

  1. Nikabiliane vipi na hali niliyonayo?
  2. Je, kutokana na roho yangu ilivyo, ikitokea nikagundua kuwa huwa nikiipaki gari langu, basi kuna mtu anakuja na kuliendesha, itakuwaje?
  3. Kama gari/shamba langu kuwa second hand tu inanisumbua, je ingekuwa kuna mbegu naziona zikistawi kutoka kwa mtu mwingine ingekuwaje?
  Nawasilisha.....!
   
 2. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #2
  Mar 14, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Hongera tu kwanza kwa kupata A ya kiswahili toka nursery school mpaka chuo kikuu
   
Loading...