Gari Latumbukia Baharini Dar

Gari Latumbukia Baharini Dar

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
26,679
Reaction score
59,176
leo alfajiri gari mali ya Bakhresa imetumbukia baharini. ni yale magari yanayo somba ngano kutoka bandarini kwenda kiwandani. ilikuwa ishapack mizani tayari kwa kupima uzito, dreva aliposhuka kwenda kuandikisha ghafla ikaanza kurudi nyuma. na kutumbukia.

Ndani kulikuwemo msaidizi wa dreva,ambaye amezama nayo hadi sasa bado hajatoka. alikuwa kasinzia anashitushwa na kelel za watu gari ishatumbukia. alipotaka kuvua nguo aogelee maji yakamzidi nguvu. ni gari namba 43 iliyokuwa ikiendeshwa na Hilary.

Mia
 
ukute aliacha bila handbreak, noma sana! mkuu hata picha tu umeshindwa?
 
Wakiambiwa wafuate safety procedures wanaona wanasumbuliwa. Hairuhusiwi kupaki gari kwenye mzani huku inaunguruma na dereva anashuka! Na wheelchockers ndo msamiati kwao. Uzembe unatumaliza watz.
Waswahili ndivyop tulivyo. Hapo tutaanza kumsingizia Mungu kuwa hii ni kazi yake. Huyu msaidizi si ndiye alipaswa kutoka kwenye kufanya clearence inayohitajika hapo kwenye mizani! Kwa nini alishuka dereva huko gari ikiwa on?
 
Mi nikajua ni yale magari yanayovushwa na kivuko .
Pole kondakta mia
 
Hii inasikitisha sana. Hivi ngano inayoletwa na meli imetoka wapi? Mia.
 
Mbona taarifa hizi zinatoka kama mtoa taarifa alikuwepo?Kama kweli ulikuwepo niruhusu nikuulize maswali zaidi, kama si hivo basi tufahamishe chanzo tafadhali.
 
Wakiambiwa wafuate safety procedures wanaona wanasumbuliwa. Hairuhusiwi kupaki gari kwenye mzani huku inaunguruma na dereva anashuka! Na wheelchockers ndo msamiati kwao. Uzembe unatumaliza watz.

King'asti nakuzimia ulivyo sharp.
Haya yote unayajulia wapi mtu wangu?
Pamoja sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom