Gari la wolper sokoni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gari la wolper sokoni

Discussion in 'Jamii Photos' started by MziziMkavu, Aug 29, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 29, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,003
  Likes Received: 3,609
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  garilaWOLPER.jpg ​[​IMG]


  KUNA madai kwamba ule ‘mkoko’ wa kifahari wa staa wa maigizo Bongo, Jacqueline Wolper aina ya BMW X6 lenye Namba za Usajili T574 BXF linatarajiwa kuingizwa sokoni wakati wowote na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) baada ya muda aliopewa nyota huyo kulipia deni lake la kukwepa ushuru wa shilingi milioni 70 kupita bila mwenyewe kusema chochote.

  Kwa mujibu wa chanzo chetu, ‘mchuma’ huo ambao ‘umetaitiwa’ na Kampuni ya Udalali ya Majembe ya jijini Dar es Salaam kwenye yadi yao ya Mikocheni, umekuwa ukipata wateja kila kukicha ambao wanakwenda kuulizia siku ya mnada.
  Chanzo kingine kilisema kuwa mbali na wateja kumiminika yadi ya Majembe, kumekuwa na usumbufu mwingi kwenye ofisi za TRA, Posta jijini Dar ambapo baadhi ya matajiri nao wamekuwa wakilifukuzia gari hilo kwa lengo la kulinunua.
  “Tunashangaa sana, watu na fedha zao wanakuja hapa kulitaka gari la Wolper, mbona kuna magari mengi yapo toka mwaka juzi (2009) hawaji kuyanunua au kwa sababu hili ni la supastaa wa Bongo?” alihoji mfanyakazi mmoja wa TRA akiomba jina lake lisitajwe gazetini.
  Akaongeza: “Unajua tatizo liko wapi? Baadhi ya wafanyakazi wa TRA nao wamekaa mkao wa kusubiri siku ya kutajwa kwa tarehe ya kulipiga mnada gari hilo ili wasuke mipango ya kupata cha juu kutoka kwa matajiri watakawaopigia debe na kushinda,” kilisema chanzo.
  Amani lilipoongea na Wolper kuhusu gari lake hilo likitaka kujua nini kitatokea kama hatalikomboa kwa siku alizopewa na TRA ambazo zimepita, alijibu hivi:
  “Kisheria gari linatakiwa likombolewe ndani ya miezi mitatu lakini mimi niliandikisha kuwa kwa mwezi mmoja nitakuwa tayari nimemaliza kila kitu. Hata hivyo, kimsingi na mimi nilimfikisha polisi Ndama Mtoto wa Ng’ombe ambaye alisimamia ununuzi wake mwanzo hadi mwisho. Kwa hiyo kama ni kukwepa ushuru ni yeye.
  Gari la Wolper lilikamatwa Juni 28, 2012 kwa madai ya kukwepa ushuru, hadi Agosti 28, mwaka huu litakuwa limefikisha miezi mitatu ambayo ni ya kisheria lakini mwezi mmoja aliotaka Wolper uliisha Julai 28, 2012 hivyo kutoa fursa kwa TRA kutangaza siku ya kulipiga bei.
  Wolper alilinunua gari hilo kwa shilingi milioni 250 za Kitanzania likiwa na sifa nyingi tofauti na magari mengine.
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Aug 29, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,460
  Likes Received: 127
  Trophy Points: 160
  Nimeona bei ya hii gari ni $90,000 plus. Kwa nini ushuru wake uwe milioni 70?
   
 3. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #3
  Aug 29, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 8,691
  Likes Received: 3,576
  Trophy Points: 280
  Basi tena hawezi kuligomboa ingawa jamaa yake ana pesa mingi!!
   
 4. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #4
  Aug 29, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,846
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  moshi wa vifuu
   
 5. Elungata

  Elungata JF-Expert Member

  #5
  Aug 29, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 26,034
  Likes Received: 5,965
  Trophy Points: 280
  Hilo gari liko na toilet ndani ama?
   
 6. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #6
  Aug 29, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,411
  Likes Received: 709
  Trophy Points: 280
  Gari lina kitanda ndani!!!!
   
 7. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #7
  Aug 29, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,145
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Waigizaji wetu wanataka kuigiza hadi lifestyle ya Hollywood. Haya twende sasa.
   
 8. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #8
  Aug 29, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  Huyu dada nimemuona hapa Tanga juzi mitaa ya club lacassa chica akiwa kwenye mkoko mwingine mkali tu! Duuh ama kweli usicheze na watoto wa kike!
   
 9. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #9
  Aug 29, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Chezea mtandao wa tGO, mpaka TA?
   
 10. Bwana Mapesa

  Bwana Mapesa JF-Expert Member

  #10
  Aug 29, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,771
  Likes Received: 574
  Trophy Points: 280
  nani anunue gari guest hyo?kwan nyi hamu wajui bongo movie?
   
 11. Bwana Mapesa

  Bwana Mapesa JF-Expert Member

  #11
  Aug 29, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,771
  Likes Received: 574
  Trophy Points: 280
  mengine ya kukodi kaka..angalia usije kuingizwa mjin
   
 12. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #12
  Aug 30, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,111
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Chezea vya bure ndo gharama yake hy fundisho kwa kina dada wanaohongwa magari mengine ya motooo wataungua nyambaffff!!
   
 13. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #13
  Aug 30, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 2,960
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kama ni gesti halina haja
   
 14. LexAid

  LexAid JF-Expert Member

  #14
  Aug 31, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 1,950
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Kama ametoa 250mill kununua bmw x6 iliyotumika then atakua mpumbavu ipAsavyo. Bora wagemaji wampige tuu!
   
 15. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #15
  Aug 31, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,341
  Likes Received: 991
  Trophy Points: 280
  TRA wameona hilo la Wolper tu?? yapo mengi sana mjini..
   
 16. c

  christmas JF-Expert Member

  #16
  Aug 31, 2012
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 2,483
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  huyo bwana ake anaempaisha hewan si angelipa hlo deni
   
 17. K

  Kifulambute JF-Expert Member

  #17
  Aug 31, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,500
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Hilo gari linazaa watoto?
   
 18. Yummy

  Yummy JF-Expert Member

  #18
  Aug 31, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,801
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Duuh......hahahaaa humu ndani ni raha sana
   
 19. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #19
  Aug 31, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 11,362
  Likes Received: 2,775
  Trophy Points: 280
  Duh! 0713 at work!!!!!!!!!!
   
Loading...