Gari la serikali limekamatwa limebeba twiga na swala

Kiwi

JF-Expert Member
Sep 30, 2009
1,054
990
Gari la serikali lenye namba STK 4394 limekamatwa likiwa limebeba twiga na swala wenye thamani ya sh 55 milioni.

Source twitter #ujangili ippmedia.

My take:
Yataisha lini? jk na serikali yako acheni kuifilisi Tanzania, siyo nchi yenu, ni ya watanzania. Vizazi vijavyo vitatuhukumu...
 
kitakacho leta vita tanzania sio siasa ni ufaidikaji wa wachache kwenye rasilimali za taifa.itafika kipindi kila mtu atajichukulia chochote anachoona mbele yake ilimradi tu kimsaidie kuishi japo siku mbili tatu.mbaya zaidi ni wale waliopewa dhamana ya kuzilinda ndio hao hao wa kwanza kujineemesha nazo
 
Askari wa Magereza mbaroni kwa ujangili

John-Minja.jpg

Kamishna Mkuu wa Magereza,John Minja

Kikosi cha Kuzuia Ujangili Kanda ya Kati kwa kushirikiana na Askari wa Misitu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, wamewakamata watu saba wanaodhaniwa kuwa majangili, wakiwamo askari watatu wa Magereza Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara kwa tuhuma za kukutwa na nyara za serikali zenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 55.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka mjini Kibaya wilayani Kiteto, Kamanda wa Kikosi hicho, Paschal Mrina alisema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa Julai 23, mwaka huu majira ya saa 6 mchana wakiwa kwenye gari la Magereza aina ya Toyota Land-Cruiser lenye namba za usajili STK 4394 likiwa linasafirisha nyara hizo.

"Nakutaarifu ni kweli tumewakamata wakiwa na gari la magereza likiwa na Twiga wawili, Pundamilia wawili, Swalapalapala majike wawili na Mbuni wawili wenye thamani ya shilingi milioni 55,543,686.20. Huu ni ujangili wenye taswira ya kuhujumu uchumi kwani twiga na swala palapala majike hayaruhusiwi kuuawa," alisema.

Mrina aliwataja waliokamatwa kuwa ni Mrakibu wa Msaidizi wa Magereza, Kimaro Joseph Sauli, WDR Richard Barick Peter na Koplo Silvester Dionis Bukha.

Aliwataja watuhumiwa wengine ambao ni raia ni kuwa ni Abubakari Ngaula, Hamza Mdachi, Saidi Iddi na Hosseni Gola, Wakazi wa Kiteto ambao alisema walikutwa na bunduki aina ya SAR ya magereza na Rifle.

Alisema wakiwa katika operesheni ya kudhibiti vitendo vya ujangili waliwakuta watuhumiwa hao katika maeneo ya uwindaji na baada ya kulitilia shaka gari hilo, walilisimamisha na kuwakuta na nyara hizo.

Alisema wakati wakiwa katika harakati za kuwadhibiti dereva wa gari hilo ambaye hakufahamika jina lake alitoroka kusikojulikana.

Alisema katika upekuzi wao, waliwakuta watuhumiwa hao wakiwa na kibali kilichoombwa na Hassan Omari kilichowaruhusu kuua nyati mmoja na pundamilia wawili.

Alisema lakini walipofika kwenye eneo la uwindaji walikiuka sheria na kuua wanyama ambao hawakuwa wamewaombea kibali na pia hawaruhusiwi kuuwawa.

Mrina alisema kuwa watuhumiwa hao, wanatarajiwa kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Manyara kujibu mashtaka ya kuhujumu uchumi.

Alisema kikosi hicho kimeweka kambi katika hifadhi ya misitu hiyo yenye mkondo unaotoka hifadhi ya taifa ya Tarangire kuelekea Mikumi ili kudhibiti ujangili unaondelea kutikisa hifadhi hizo.

Akizungumzia kuhusu changamoto zinazowakabili katika operesheni hiyo, alisema kazi yao inakuwa ngumu pindi magari ya serikali yanapotumika kwenye uhalifu na kwamba ni vigumu kuyatilia shaka.

"Umeona mwandishi changamoto ni magari kama haya kubaini kuwa yanatumika ni vigumu lakini kumbe umdhaniaye siye kumbe ndiye, sasa askari kama hao ndiyo wangekuwa mstari wa mbele kudhibiti ujangili, lakini badala yake wamekuwa nstari wa mbele katika kuhujumu, lakini sisi hatutaangalia sura ama cheo mhalifu ni mahlifu tutamdhibiti," alisisitiza Kamanda huyo.

Alisema hifadhi zilizopo kwenye mkondo huo zimekuwa zikutumiwa na majangili wanaoingia kinyemela kuangamiza nyara hizo za serikali.

Alisema miezi miwili iliyopita, watu wawili walikutwa na maboga wakiwa katika harakati za kuwaua tembo kwa kutumia sumu inayowekwa ndani yake.

Mlolongo wa matukio ya ujangili ambayo umekuwa ukiwahusisha askari wa majeshi mbalimbali nchini umeendelea kutikisa.

Miongoni mwao ni Sajini wa Jeshi la Wananchi Tanzania, Azizi Athuman Yusufu ambayo inadaiwa alikamatwa Januari 20, mkoani Arusha akiwa pembe mbili za ndovu na bunduki aina ya Riffle yenye namba 458.

Mwanajeshi huyo pia inadaiwa kuwa alikuwa akitumia gari ya mkufunzi wa kijeshi kutoka Zimbabwe anayefundisha nchini.

Imeandikwa na Cynthia Mwilolezi, Arusha na Gideon Mwakanosya, Songea.

CHANZO: NIPASHE

kitakacho leta vita tanzania sio siasa ni ufaidikaji wa wachache kwenye rasilimali za taifa.itafika kipindi kila mtu atajichukulia chochote anachoona mbele yake ilimradi tu kimsaidie kuishi japo siku mbili tatu.mbaya zaidi ni wale waliopewa dhamana ya kuzilinda ndio hao hao wa kwanza kujineemesha nazo

Ungekuwa karibu ningekubeba, umenena vyema!
 
askari watatu wakiwa na gari la serikali namba STK 4394! Sio rahisi hii operations kufanyika bila ya incharge wao kuwa na taarifa. Taifa hili bila kuchukua hatua za haraka na za makusudi linaangamia tusidanganyane.
 
Ipo siku hata watu/wananchi tutauzwa na kubebwa kama twiga na swala, hii ndo serikali adilifu yenye sera nzuri za maendeleo zisizo na tija kwa wananchi wake.
 
Hao ni waliokamatwa, maelfu mabgapi ya wanyama wanasafirishwa? In the near future hatutakuwa na watalii wa nje, waje kufanya nini na wanyama wote wako kwao tayari! Yaani wanaofanya hujuma hii ni ma ku...ayo kabisa. Inauma sana na inaudhi sana. Leo hii wananchi wanaoishi karibu na mbuga hata kuwinda sungura kwa ajili ya kitoweo hawaruhusiwi. Pumba.....vu zenu wahusika
 
Gari la serikali lenye namba STK 4394 limekamatwa likiwa limebeba twiga na swala wenye thamani ya sh 55 milioni.

Source twitter #ujangili ippmedia.

My take:
Yataisha lini? jk na serikali yako acheni kuifilisi Tanzania, siyo nchi yenu, ni ya watanzania. Vizazi vijavyo vitatuhukumu...

...kwani Meli ya Knn imeishatia nanga Bandarini? au ni Ndege ya Waarabu imeishawasili KIA?
 
KAma askari anaua raia Mwema kwa issue za kisiasa halafu huyo askari akapandishwa cheo. Hiyo ni tafsri kuwa wamepewa na mamlaka ya kufanya chochote katika nchi hii! wakulaumu sio askari bali wenye mamlaka maana wamewapa mamlaka ya kuwa juu ya sheria! Ni holela holela tu!!!
 
......Nadhani hawa jamaa walimuelewa vibaya Pinda pale aliposema ''wapigwe tu maana tumeshachoka'', walidhani hadi wanyama pori nao wapigwe. Kauli ya ''Bend'' itasababisha tuone mengi.
 
Hao ni waliokamatwa, maelfu mabgapi ya wanyama wanasafirishwa? In the near future hatutakuwa na watalii wa nje, waje kufanya nini na wanyama wote wako kwao tayari! Yaani wanaofanya hujuma hii ni ma ku...ayo kabisa. Inauma sana na inaudhi sana. Leo hii wananchi wanaoishi karibu na mbuga hata kuwinda sungura kwa ajili ya kitoweo hawaruhusiwi. Pumba.....vu zenu wahusika
Kweli inatia uchungu jinsi hawa watawala wahuni wanavyo inajisi TZ, ila punguza hasira kwani waweza jipa magonjwa bure.
 
Mlinzi anapogeuka kuwa mwizi nambari moja. Kwa mwendo huu itafika kipindi tutaondoa taswira za wanyama kwenye fedha, nembo ya taifa n.k.
 
Usione watu wanatajirika tu nchi hii we ukadhani wamebarikiwa na Mungu! Imekula kwako
 
Siamini kama dreva wa gari la serikali ana nguvu na mamlaka ya kutumia hilo gari bila idhini ya mkubwa (supervisor) wake.
 
Back
Top Bottom