Gari la Serikali lanaswa na madawa ya kulevya

Kiturilo

JF-Expert Member
Sep 27, 2021
709
2,850
Gazeti la mwananchi limeripoti kuwa gari lenye namba za serikali limenaswa likiwa na kilo 430 za dawa za kulevya huku mmiliki wake akitokomea kusikojulikana na anaendelea kusakwa kila kona bila mafanikio.

My take.
Kwa kasi hii mateja na watu wanaotoa udenda barabarani wataanza kuonekana tena. Paul Makonda rudi kazini aisee uokoe vijana wetu.

===

Moshi/Rombo. Vita dhidi ya biashara ya dawa za kulevya inazidi kushika kasi mkoani Kilimanjaro, baada ya watu wawili kutiwa mbaroni na Jeshi la Polisi wilayani Rombo kwa tuhuma za kusafirisha kilo 430 za dawa za kulevya aina ya mirungi.

Hata hivyo, inadaiwa mmiliki wa gari lililokuwa na namba za Serikali STK 5211 lililokutwa likisafirisha dawa hizo ni la mtumishi wa Serikali ambaye anasakwa kwa mahojiano.

Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro, Simon Maigwa alipoulizwa jana alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo na kwamba watu wawili wanashikiliwa na polisi kwa kusafirisha mirugi kwa kutumia gari lililokuwa na kibao cha namba za Serikali.

Alifafanua gari hilo lilikuwa mali ya Serikali na tayari liliuzwa kwa mnada na kwamba wasafirishaji walikuwa wakilitumia namba hizo, ili wapite kirahisi. Inaelezwa walikuwa wakiitoa mirungi hiyo Kenya na kuipeleka Singida.

Hata hivyo, Kamanda Maigwa alikataa kuingia kwa undani juu ya tukio hilo wala umiliki wa gari.

Vyanzo kutoka Dodoma na miji ya Moshi na Rombo, vimedai gari hilo aina ya Toyota Land Cruiser ni mali ya mtumishi huyo wa umma ambaye inadaiwa alilinunua katika mnada, ingawa haieleweki kwanini lilibaki na namba hizo.

Advertisement
Taarifa hizo zilidai wa kwanza kukamatwa ni watuhumiwa wawili waliokamatwa Januari 30, 2022 kati ya saa 2 na saa 3 asubuhi katika Kijiji cha Mamsera wakisafirisha bunda 880 za dawa hizo kutoka Rombo kuelekea Singida.

“Hiyo gari ilikamatwa ikiwa na plate namba STK 5211 ikionyesha ni gari ya Serikali, uchunguzi ulifanyika na cha ajabu kwenye vioo vilionyesha vimegongwa namba STJ 1972 ambazo ni tofauti na zilizokuwa zimebandikwa,” ilidaiwa.

“Bahati nzuri ndani ya hiyo gari kulikuwa na kadi yake ambayo sasa ilionyesha namba zake halisi za binafsi kuwa ni T 404 CMF na tulipochunguza TRA (Mamlaka ya Mapato) tulibaini huyu mtumishi huyo alilinua kwenye mnada,” ilielezwa.

Hata hivyo, bado kuna utata unaohitaji majibu wa ilikuwaje baada ya kununua gari hilo, mmiliki huyo mpya aliendelea kubaki na vibao vya namba za usajili za Serikali na hiyo ndio imefanya mtumishi huyo naye akamatwe kwa mahojiano.

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, baada ya watuhumiwa hao wawili walikuwa ndani ya gari hiyo kukamatwa wilayani Rombo na kuonekana gari ni mali ya mtumishi huyo, Jeshi la Polisi lilimtaka naye kufika polisi, ili ahojiwe kuhusiana na tukio hilo.

Taarifa ya hali ya dawa za kulevya ya mwaka 2020 inaonyesha kupanda kwa kiwango cha dawa aina ye heroin zilizokamatwa.

Taarifa inaonyesha mwaka 2020 jumla ya kilo 349.81 za heroin zilikamatwa ikilinganishwa na kilo 55.35 zilizokamatwa mwaka 2019.

Idadi ya watuhumiwa wanaokamatwa na Heroin na Cocaine imeendelea kuongezeka ambapo 428 walikamatwa na heroin wakati 80 wakikamatwa na cocaine tofauti na mwaka 2019 ambapo 318 walikamatwa na heroin na 31 cocaine.
20220204_112015.jpg
 

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
3,086
4,862
Gazeti la mwananchi limeripoti kuwa gari lenye namba za serikali limenaswa likiwa na kilo 430 za dawa za kulevya huku mmiliki wake akitokomea kusikojulikana na anaendelea kusakwa kila kona bila mafanikio.

My take.
Kwa kasi hii mateja na watu wanaotoa udenda barabarani wataanza kuonekana tena.
Paul Makonda rudi kazini aisee uokoe vijana wetu. View attachment 2107438
Arudi wakati ndio alikuwa anaifanya yeye hiyo biashara.
 

nyboma

JF-Expert Member
Aug 29, 2021
2,083
6,461
Huenda ikaisha pia kimyakimya
Sio rahisi hivyo mkuu, lazima sheria ichukue mkondo wake na huyo kijana aliyekimbia na huo mzigo lazima atakamatwa aje atueleze ni nani huwa anamtuma kumsafirishia huo unga
 

nyboma

JF-Expert Member
Aug 29, 2021
2,083
6,461
mbona wakikamatwa hatupati mrejesho wa mahakama wamefungwa au faini maana nakumbuka wanajeshi walikamata baharini kilo 1000 za dawa za kulevya mtwara walikuwa wapakistan lakini mpaka leo kimya
Mkuu ulishawahi udhuria mahakani kusikiliza hizi kesi, watu wanalimwa mvua kama kawaida sio kila hukumu ilitoka lazma iwe published na vyombo vya habari.
 
7 Reactions
Reply
Top Bottom