Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,218
- 25,625
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Misugusugu, wilayani Kibaha wamefunga barabara ya Morogoro kufuatia wenzao watatu kugongwa na gari la polisi mapema leo.
Inasemekena wanafunzi hao watatu au kati yao wamefariki dunia. Wanafunzi hao waligongwa walipokuwa wakitaka kuvuka kuelekea shuleni kwao.
Lori la mafuta lilisimama kuwapisha wanafunzi wavuke kwenye pundamilia. Lakini gari ya polisi iliovertake kwa kasi na kuwasomba wanafunzi hao wa Shule ya Msingi Misugusugu.
Tayari barabara imeshafungwa na wanafunzi hao na kusababisha adha kubwa kwa wasafiri na wasafirishaji.
Taarifa zaidi zitafuata.
==================================
UPDATES:
JamiiForums said:Polisi mkoani Pwani wanamshikilia askari wake aliyesababisha ajali iliyoua mwanafunzi mmoja
WANAFUNZI wa Shule ya Msingi Misugusugu Kibaha mkoani Pwani, wamefunga barabara ya Morogoro kwa masaa kadhaa baada ya wenzao wawili kugongwa na gari la Jeshi la Polisi mapema leo asubuhi.
Aidha, askari Polisi aliyesababisha ajali baada ya kuwagonga wanafunzi hao, ambapo mmoja kati yao alifariki dunia muda mchache baada ya ajali hiyo.
Kufuatia tukio hilo, wanafunzi na wananchi wa eneo hilo walifunga barabara ya Morogoro kwa saa kadhaa wakitaka hatua za kisheria zichukuliwe ili kuepusha matukio kama hayo.
Akizungumza na Mwanadishi wetu Kamanda wa Polisi mkoani humo, Jafari Ibrahim, amesema tayari Jeshi hilo limekwisha kuchukua hatua za kiusalama ikiwa ni pamoja na kumsweka rumande askari aliyesababisha ajali hiyo.
"Kinachoendelea sasa hivi ni mkutano tunaoufanya hapa na wanafunzi na baadhi ya wananchi wa eneo hili, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, pamoja na Meneja wa Tanroad mkoa, Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD), na viongozi wengine na tunawaelimisha wananchi na kuwapa pole kutokana na ajali hii ili barabara ipitike kwa" alieleza Kamanda Ibrahim.
Hata hivyo, amesema pamoja na mambo mengine wamekwisha chukua hatua kwa dereva aliyesababisha ajali hiyo na kuwa wanaendelea kuwaelimisha wananchi katika suala la kutii sheria na kuacha kujichukulia hatua mikononi. Amesema kwa kuwa wapo na Meneja wa Tanroad atazungumza kama mtaalamu na watasikiliza kuwa kitu gani atakachokizungumza.
"Tumekwisha kumkamata askari aliyesababisha ajali na mauaji na tumemuweka mahabusu na taratibu za kumshtaki zinazendelea" aliongeza Kamanda Ibrahim.
Amesema mwili wa mwanafunzi aliyekufa katika ajali hiyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Tumbi iliyopo Kibaha mkoani Pwani inagwa hakutaja jina la mwanafunzi huyo kutokana na hali ya usalama ilivyo katika eneo la tukio.