Gari la Polisi lagonga wanafunzi Wawili, Mmoja afariki. Wanafunzi wafunga barabara

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,205
25,535
attachment.php


Wanafunzi wa Shule ya Msingi Misugusugu, wilayani Kibaha wamefunga barabara ya Morogoro kufuatia wenzao watatu kugongwa na gari la polisi mapema leo.

Inasemekena wanafunzi hao watatu au kati yao wamefariki dunia. Wanafunzi hao waligongwa walipokuwa wakitaka kuvuka kuelekea shuleni kwao.

Lori la mafuta lilisimama kuwapisha wanafunzi wavuke kwenye pundamilia. Lakini gari ya polisi iliovertake kwa kasi na kuwasomba wanafunzi hao wa Shule ya Msingi Misugusugu.

Tayari barabara imeshafungwa na wanafunzi hao na kusababisha adha kubwa kwa wasafiri na wasafirishaji.

Taarifa zaidi zitafuata.
==================================
UPDATES:

JamiiForums said:
Polisi mkoani Pwani wanamshikilia askari wake aliyesababisha ajali iliyoua mwanafunzi mmoja

WANAFUNZI wa Shule ya Msingi Misugusugu Kibaha mkoani Pwani, wamefunga barabara ya Morogoro kwa masaa kadhaa baada ya wenzao wawili kugongwa na gari la Jeshi la Polisi mapema leo asubuhi.

Aidha, askari Polisi aliyesababisha ajali baada ya kuwagonga wanafunzi hao, ambapo mmoja kati yao alifariki dunia muda mchache baada ya ajali hiyo.

Kufuatia tukio hilo, wanafunzi na wananchi wa eneo hilo walifunga barabara ya Morogoro kwa saa kadhaa wakitaka hatua za kisheria zichukuliwe ili kuepusha matukio kama hayo.

Akizungumza na Mwanadishi wetu Kamanda wa Polisi mkoani humo, Jafari Ibrahim, amesema tayari Jeshi hilo limekwisha kuchukua hatua za kiusalama ikiwa ni pamoja na kumsweka rumande askari aliyesababisha ajali hiyo.

"Kinachoendelea sasa hivi ni mkutano tunaoufanya hapa na wanafunzi na baadhi ya wananchi wa eneo hili, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, pamoja na Meneja wa Tanroad mkoa, Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD), na viongozi wengine na tunawaelimisha wananchi na kuwapa pole kutokana na ajali hii ili barabara ipitike kwa" alieleza Kamanda Ibrahim.

Hata hivyo, amesema pamoja na mambo mengine wamekwisha chukua hatua kwa dereva aliyesababisha ajali hiyo na kuwa wanaendelea kuwaelimisha wananchi katika suala la kutii sheria na kuacha kujichukulia hatua mikononi. Amesema kwa kuwa wapo na Meneja wa Tanroad atazungumza kama mtaalamu na watasikiliza kuwa kitu gani atakachokizungumza.

"Tumekwisha kumkamata askari aliyesababisha ajali na mauaji na tumemuweka mahabusu na taratibu za kumshtaki zinazendelea" aliongeza Kamanda Ibrahim.

Amesema mwili wa mwanafunzi aliyekufa katika ajali hiyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Tumbi iliyopo Kibaha mkoani Pwani inagwa hakutaja jina la mwanafunzi huyo kutokana na hali ya usalama ilivyo katika eneo la tukio.
 

Attachments

  • Ajali Kibaha,Pwani.jpg
    Ajali Kibaha,Pwani.jpg
    33.9 KB · Views: 2,873
  • Ajali Kibaha,Pwani.jpg
    Ajali Kibaha,Pwani.jpg
    9.5 KB · Views: 2,920
Kwa wenye taarifa au picha watuambie kuna ajali mbaya sana barabara ya kwenda kongowe wanafunzi watatu wamezolewa na defender ya police na mmoja wao amepoteza maisha huku wengine wawili hali zao zikiwa mbaya chanzo cha ajali ni mwendo kasi wa gari hilo la police bila kujali eneo hilo la shule lina alama za zebra kwa ajili ya watu kuvukia/ habari E FM radio
 
Yan wamewagonga na bado wanatumia ubabe kuwatawanya,oct 25 ni wakati wa kutumia vizuri kichanjio chako ili turudishe upya polisi jamii inayofanyia kazi kauli mbiu yake
 
Kwasasa wanafunzi wamerudi shuleni. Lakini watu wazima wameivamia barabara na kuifunga. Hata barabara ya zamani nayo imefungwa. Wanachoma vitu mbalimbali barabarani na kuzua taharuki kubwa. Polisi wameongezeka kuweka mambo sawa
 
Nimepokea taarifa toka kwa dereva ambaye naye yupo eneo la tukio. Anasema kuwa hadi muda huu bado mapambano yanaendelea. Wanachi wanawapiga polisi, na Polisi wanatumia mabomu ya machozi. Lakini wananchi hawarudi nyuma. Bado kumefungwa hakuna amani.


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Pole kwa wanafunz,pole sana kwa watu wa Misugusugu.....Upolisi ni moja ya kazi za ajabu sana duniani,,,,,,

Hapo tayar ushatengenezwa uhasama baina ya polisi na raia kwa eneo hilo,sasa lori limesimama wapite,wao wanaovertake,so wao wapo juu ya sheria????na hyo afande alogonga utaskia kahamishwa kituo tu na cheo atapandishwa......
 
mna uhakika wamepigwa mabomu au ndo ile akili ya kuambiwa kitu na kukibeba kama kilivyo bila kufikiri?
 
Back
Top Bottom