MGOMBEA ubunge wa jimbo la Vunjo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Agustine Mrema, amenusurika kupata kipigo kutoka kwa kundi la vijana wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Mbali ya Mrema kunusurika katika tukio hilo, gari lake liliharibiwa vibaya kwa kupigwa mawe hadi kioo chote cha mbele kupasuliwa na yeye kunusurika.
Tukio hilo, ambalo lilikuwa kama mchezo wa kuigiza, lilitokea juzi eneo la njia panda ya Himo, wakati Mrema alipokuwa akipita barabara kuu iendayo Dar es Salaam karibu na eneo ambalo mgombea ubunge wa CCM, Crispin Meela, alikuwa akifanya mkutano wa kampeni za kuomba kura kwa wapiga kura wake.
Mrema, aliwaambia waandishi wa habari kuwa katika tukio hilo, yeye hakujeruhiwa, lakini gari lake aina ya Toyota Land Cruizer lenye namba za usajili T 317 ALK lilivunjwa vibaya.
"Mimi nimesurika kupata kipigo, lakini gari langu limeharibiwa vibaya, kioo chote cha mbele kimevunjwa na kundi la watu wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa CCM," alisema Mrema.
Alisema tayari amefungua kesi katika kituo cha polisi Himo, yenye nambari HI/RB/2979/2010 akimshtaki mwana CCM Humphrey Njau maarufu kwa jina la Rasta ambaye anadai alimtambua wakati wa vurugu hizo.
Mrema, alisema tukio hilo lilitokea majira ya saa 11.50 jioni, wakati akitokea kijiji cha Lole, kata ya Mwika Kaskazini, akiwa ameongozana na gari lake la matangazo, lakini alipofika njia panda ambako ndiko yalipo makazi yake, aliona wananchi waliokuwa kwenye mkutano wa CCM wakianza kumshangilia, ghafla akatokea Rasta akarusha jiwe likapasua kioo.
"Njia panda hakuna uwanja wa kufanya mkutano wa kampeni, pale ni maduka ya watu ya biashara, sasa CCM wameona watu hawawafuati kwenye viwanja vya mikutano wameamua kuja kujibanza pembeni ya nyumba zao na kufanya mikutano, huku ni kuwasumbua wananchi kwenye biashara wanazoziendesha kwa mujibu wa sheria za nchi," alisema Mrema.
"Kwa kweli ni hatari jana (juzi) nilikuwa niuawe na CCM huku Vunjo, baada ya kuona wanazidiwa wameamua kutumia vurugu," alisema Mrema.
Kutokana na hali hiyo, Mrema amelihimiza Jeshi la Polisi kuchukua tahadhari ya kujipanga vizuri ili kukabiliana na fujo zisizokuwa za lazima. Kwa siku za hivi karibuni Mrema anadaiwa kuwa mstari wa mbele kumpigia debe mgombea urais wa CCM Jakaya Kikwete.
Akionyesha hali hiyo, hata alipoalikwa kwenye Mkutano Mkuu mkoani Dodoma, Mrema hakuficha hisia zake pale aliposimama na kucheza muziki uliokuwa ukiporomoshwa na kundi la Sanaa la Tanzania One Theatre (TOT).
Juhudi za kumpata Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Lucas Ng'ohoboko, kuzungumzia tukio hilo, ziligonga mwamba kutokana na simu zake za kiganjani kuita bila kupokelewa muda.
Hili ni tukio la kwanza kutokea tangu kivumbi cha kampeni kilipoanza Agosti 21 mwaka huu.