Gari la mkopo laibiwa

hao u trackk wanapatikana wapi asee?

Wapo Dar es salaam na Arusha...! Kwa Arusha wapo along Himo road karibia na kwa mrefu kituo cha mafuta cha BP, but Dar es salaam wapo pale mikocheni
 
Hii ngoma bado mbichi ngoja waje wajuvi wa haya mambo! kuna mshkaji aliuza nyumba Mill 60 kaenda kununua Rav 4 number A ambayo ilishatumika iliyobaki kaenda kapanga nyumba kawatupa huko familia yake nyingne anatengenezea heshima bar!

Jambazi;
Unamwonea mwenzio gele?? Ulikuwepo akiwa anazitafuta hizo hela za kiwanja mpaka nyumba? Kama hiyo familia imefika kwake ikakuta anavyo hivyo vyote halafu hawamheshimu wataka afanye nini??
Bora heshima ya siku mbili kuliko kuvunjiwa heshima miaka 20. Auze, ale zikiisha atakuwa keshapata marafiki napia akili mpya. Castle lager ina hishima yake banaa, haswa ukijua kuwa bado ganda ni gumu kulibanjua.
 
Wapo Dar es salaam na Arusha...! Kwa Arusha wapo along Himo road karibia na kwa mrefu kituo cha mafuta cha BP, but Dar es salaam wapo pale mikocheni
Suluhisho ya haya yote ni chombo chako kukilipa insuarance ya comprehensive basii kila kitu umemaliza. We ukusikia juzi wezi wa magar wakitaka kuchukua gari zenye security systems wanaweka sumaku kwenye boneti na gar wanaondoka nalo?! Akili kichwan mwako
 

Hilo gari kwan hakulikatia comprehensive insurance? Kama alikata bima kubwa asiwe na wasi wasi
 
kwanza wewe kama mtu wa karibu yake umemshauri nini?cha msingi maisha ni maisha akomae tu.atasonga tu.kuna watu wamepoteza familia, nyumba hata walezi na wenzi wao.cha msingi aende kwa washauri wa saikoloji watamsaidia.
 

Gari hali ibiwi halina linachomiliki. Gari LIMEIBWA. sasa katika hoja yako ni kwamba Gari lolote la mkopo tena wa benki wapo makini sana na sheria zinazingatiwa kwa umakini wa hali ya juu.
Lazima LINA BIMA.
 
kwa hiyo alikopa ili gari aifanyie biashara ndo alipe hilo deni crdb, au anamiradi mingine?
 

Umeongea vizuri sana........ila nina wasiwasi na mtoa thread...........kama sio zogo anapiga.........basi huyo rafiki yake ni mbulula nambari one........kuweka rehani nyumba kukopa gari............
 
Hivi mimi nauliza, hizi gar zikiibiwa zinapelekwa wap? Maana Nina ndugu yangu aliibiwa Rav 4 hakuipata!

Kama na wewe una Rav4 siku ukienda kununua spares ambazo ni used, utanunua vifaa vya gari yake. Hiyo gari ilichinjwa na parts zake zinauzwa kama used parts.
 
Hivi inakuwaje ukinunu nyumba ambayo imewekwa zamana benk. Nani atakamatwa kati yangu niliyeuziwa na aliyeuza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…