Nashauri sifa za kuwa/kugombea ubunge zirekebishwe,mbunge angalao awe na elimu ngazi ya degree.
Uchague mgombea mwenye degree au darasa la saba matokeo ni yaleyale...........
Ukweli usiosemwa ni kwamba mbunge hana chochote cha kuwaletea wapiga kura wake zaidi ya kutatua kero ndogo ndogo tu......
Unless jimbo lake likutwe limo ndani ya mikakati au vipaumbele vya kitaifa.
mfano; Ni UONGO mbunge wa Tabora kuwaambia wapigakura wake nimewaletea maji kutoka ziwa Victoria.
Ni UONGO Mbunge wa Dodoma mjini kuwaaminisha Wananchi aliwaboreshea miundombinu.
Ni UONGO kwa mbunge yeyote wa Dar es Salaam kuwaahidi watu atatatua kero ya foleni kwenye eneo lake..
Hakuna Jimbo au wilaya ambalo hela hazipelekwi....isipokuwa mahitaji ni makubwa mno kuliko mgawo ulioletwa majimboni..
Sasa ni ubunifu wako wewe mbunge kuwaaminisha watu wajue kuna kitu ulifanya, iwe ni kweli au porojo.
Ndio maana mbunge kama Baba levo kwa kujua restrictions hizo ameamua kuwa mkweli kwa kutrend na vitu vyepesi vyepesi kama
Pilau la bure, daftari bure, bodaboda za mikataba nafuu,
Kuliko kuwalaghai watu kwa ahadi ngumu ambazo ni ngumu kuzipata hasa kwa kipindi hiki ambacho serikali ina hela za matumizi yake tu, sio za maendeleo.