Gari ipi itanisaidia kubana matumizi

Cuf.jpg
Fuel Consumption Zero Majani tu na Ufagio wa kuzolea hanyari Punda akiachia au unamshoneshea mfuko kwenye masaburi asichafue mazingira.. Bei ni Poa unahitaji kama million moja tu
Donkey Carry
Status:Available
Ref. No:MM2
Year :2005
Mileage :19000
Engine Type:Punda Force IIA
CC:500
Transmission Type:Manual
Location:Tanzania
Asking Price:TZS 1,000,000
Includes all taxes Ministry of Maliasili na Utalii
Interior features:Carry Body Features:
» AM/FM Miluzi
» Hand Power string
Additional Features:
Financial Features:
» Price is negotiable
» Registration included
Dereva Wanapatikana


ur grt thnker. Nasikia ni full AC
 
wenye uzoefu na magari nisaidieni, nahitaji kununua gari

my concern;
1. iwe na consumption ya mafuta kiasi...
2. mahali ninapoishi na ofisini ni km 20 kwenda 20 kurudi kila siku
3.most wkends nina misele ya mkuranga na mlandizi (nina vijibustani huko lol)
4. nafikiria kununua cami au swift je zitamudu hayo masafa? na je hazisumbui?
5. nilikuwa na gari yenye cc 2200 ila hiyo hela ninayopoteza kwenye mafuta naona ni bora niingize kwenye vijiproject vyangu huko mkuranga,nahitaji gari itakoyonimuvuzisha from point A to B full stop.
6. na-prefer gari isiyozidi cc 1300.

Ushauri tafadhali.
Nakushauri ununue ka-Starlet kama haka ka kwangu......... huwa naenda nako hapo Moshi from Dar kama kawaida huku nikijimiminia Castle za kopo.....Ukiweka Full tank unasahau kabisaaaaa. Na spea zimejaa bwerere kwa bei ya kutupa.

Angalizo: Usiwe na hasira wadau watakapokuambia hebu weka "babysitter" yako kule pembeni wenye magari tupite........
 
nakushauri ununue ka-starlet kama haka ka kwangu......... Huwa naenda nako hapo moshi from dar kama kawaida huku nikijimiminia castle za kopo.....ukiweka full tank unasahau kabisaaaaa. Na spea zimejaa bwerere kwa bei ya kutupa.

Angalizo: Usiwe na hasira wadau watakapokuambia hebu weka "babysitter" yako kule pembeni wenye magari tupite........

lmfao....
 
Naam hakuna tofauti yeyote kwa foleni ya dar siku hizi naona bora mtu kuendesha baiskeli kuliko kuendesha V8 katikati ya jiji la Dar.

Umezungumzia distance from Tegeta to Nyerere road maeneo haya yana foleni sana asubuhi na jioni kuanzia mwenge, morocco kwenda tangi bovu. Ushauri wangu unaweza kuendesha baiskeli in between and then kuendelea huko ukachukua gari lako ulilopaki mwenge kwenda zako nyerere road. Wakati wa kurudi kutoka kazini pia unaendesha gari yako mpaka mwenge unalipaki na kuchukua baiskeli au daladala mpaka kwako Tegeta.

Binafsi mwakani mungu akipenda nimeweka malengo nianze kuendesha baiskeli kutokea mahali nakopaki gari yangu hadi ofisini kwangu. Kwani kuanzia mjini (city centre) mpaka ofisini natumia dk 15 kutembea kwa miguu ila kwa gari it takes around 1 hour or 30 minutes. Gari yangu ni CC 2900 na hivyo inamaana kwa safari ya pole pole naweza kuwa natumia si chini ya Tshs 10,000. Bado sijaweka hasara ya gharama za kulika kwa clutch, accelerator, mikwaruzo ya gari nk. Tuseme kama 50,000. Hivyo nitalichukua gari langu hadi karibia na mjini napaki nachukua baiskeli naingia nayo katikati ya mji.

Na wewe jipange ndugu gari yeyote ina faida zake na hasara zake asikudanganye mtu. Nimeendesha gari ya CC 1100 (Suzuki Jimmy), Nimeendesha gari ya CC 2000 , Nimeendesha gari ya CC 1500 na sasa naendesha gari ya CC 2900 sioni tofauti yeyote ni nidhamu ya matumizi tu ndio cha msingi hakuna zaidi.

Safi sana mkuu una experience nzuri na magari, ninashangaa kwa nini haujaanza kutumia baiskeli na unamshauri mwenzio atumie baiskeli

hali za miundo mbinu za wenzetu ulaya na sisi ni tofauti sana achilia mbali weather. Is easier to drive bycle in Newyork than in DSM...tuwe realistic kidogo.

halafu tofauti ya CC kwenye magari ni considerable haingii akilini gari la cc 650 say suzuki kei kuwa na consumption sawa na gari la cc 3000 say isuzu bighorn! kama inakutokea check mambo mengine kama A/C na other services ambazo zinakula mafuta
 
Ndio nilichokuwa najaribu kumuhabarisha ndugu hapa. Ukinunua gari ya mafuta kidogo. Utakuta spea zake bei mbaya au hazipatikani. Ukinunua gari ya bei rahisi unaweza kukuta uimara wake ni finyu na matokeo yake kila siku gari liko kwa fundi. Mfano gari za Toyota sio sawa na Honda au Nissan. Nissan ikipata matunzo mazuri au honda kwa fundi wa magari ni mwiko unaweza kumsahau. Toyota ijapokuwa bei yake ni ndogo lakini hauchelewi kuwa unaweka mahudhurio mazuri kwa fundi.

Gari yeyote ina faida na hasara zake hata kama ikiwa ni gari ya umeme (isiyotumia mafuta kabisa lakini utakuta speed mwisho km 50 kwa saa au less na spea zake usiulize bei yake). La muhimu ni mpangilio mzuri tu wa maisha na kama huwezi kuafford achana na gari tafuta usafiri mwengineo au tumia usafiri wa jamii kama mabasi au baiskeli au bajaj.

imetulia hii mddj
 
Safi sana mkuu una experience nzuri na magari, ninashangaa kwa nini haujaanza kutumia baiskeli na unamshauri mwenzio atumie baiskeli

hali za miundo mbinu za wenzetu ulaya na sisi ni tofauti sana achilia mbali weather. Is easier to drive bycle in Newyork than in DSM...tuwe realistic kidogo.

halafu tofauti ya CC kwenye magari ni considerable haingii akilini gari la cc 650 say suzuki kei kuwa na consumption sawa na gari la cc 3000 say isuzu bighorn! kama inakutokea check mambo mengine kama A/C na other services ambazo zinakula mafuta

Mkuu,

Mwakani ninaanza kutumia baiskeli nimeshaagiza bike yangu nitakuwa naiendesha mjini kwenda na kurudi. Tatizo lililopo ni sehemu ya kupakia magari ya usalama kwani Tanzania zaidi ya unavyoifahamu mkuu. Nilitegemea sehemu fulani maeneo ya Drive in ningelikuwa nishaanza but kuna tatizo limetokea nikakosa sehemu ile ya kupark gari.

Kaka/dada miundo mbinu ya maeneo ya magomeni, upanga, oysterbay ni mizuri sana haina tofauti na ulaya. Tatizo labda liko katika usalama wa mtumiaji njia such as wezi nk. Hilo linaweza kuepukika kwa kuwa muangalifu. Ila tukiangalia usafiri wa magari sasa hivi mijini ni hasara na kero. Nikiwa maeneo ya mikocheni, msasani naweza kutumia more than 2 hours kufika ofisini asubuhi. Ukiendesha baiskeli inakuchukua karibia dk 37-45 kufika ofisini na afya inaimarika mkuu. Kuhusu mvua baiskeli za kukunja unaweza kupanda nazo taksi zinakunjika kama begi na kupanda nazo taksi au kwenda nayo ofisini.

Believe me gari yenye CC ndogo au kubwa hazina tofauti utakutakana na msumari wa gharama somewhere.
 
Ndg yangu nakushauli tafuta spacio pia nayo inasaidia kubana matumizi kwani haili kabisa mafuta jalibu uone
 
Kweli kaka/dada if you cannot afford to maintain a car why not buy a bicycle. Hivi unajua Waziri kama Vince Cable (waziri wa biashara na Viwanda UK) anaendesha baiskeli kwenda ofisini kwake. Meya wa London Boris Johnson naye pia anaendesha baiskeli kwenda ofisini kwake. Na ukiwaona wana afya nzuri sana. Sisi tuna masukari, mablood pressure, vitambi kwasababu hatuna exercise yeyote. Gari yeyote utakayonunua itakuwa ina manufaa na hasara zake. Unaweza kununua Hyundai i10 but ukawa usalama wako uko hatarini, barabara nyingi huwezi kupita, safari ndefu hazifiki zinachemsha n.k. Vile vile unaweza kununua V8 ukawa unatumia mafuta mengi bila ya sababu (mfano kuendesha katikati ya mji kama Dar), parking tabu nk.
Kwaio unamshauri anunue bike ili awe anaenda nayo mllandizi sio?
 
Wazo zuri sana hili la kutumia baiskeli, lakinikwa miundombinu hii ya Bongo, sijui kama linawezekana, usalama wako utakuwa hatarini sana
Kaka unajua dar NA ukiiongelea London Kwa hao mawazir utakuta umbal wao wanaotembea Kwa baiskel ni Kama kutoka kivukoni na labda manzese tu n nahisi mbali tusisahau kuwa uingereza ni kisiwa Hivo sio kubwa Kama liinchi let au dar... Na pia Hali ya hewa ni tofaut kuanzia JUA HAD MVUA ZETU SOMETIME NI TOFAUT
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom