Viongozi wengi hasa wa nchi Za kiafrika Sijui huwa wanautupa wapi uwezo Wao wa kufikiri waluopewa na Mungu!!!. Tatizo ni kuwa huwa wanadanganyika na kuamini kuwa Mambo ni static - yataendelea kuwa hivyo hivyo. Madhara yake ni kuwa mipango yoyote wanayopanga huifanya kwa kuzibgatia kuwa Wao watakuwa madarakani milele! Matokeo yake ni kuwa silaha walizonunua, mipango waliopanga, sheria walizotunga kwa lengo la kuwakabili wapinzani Wao HUWAGEUKA pale Mambo yanapogeuka! Nchi zote zinazopata shida sio kwamba hakuna Kesho, Polisi, Magereza wala Usalama wa Taifa! Vyombo vyote vya usalama vipo lakini Mambo hubadilika tu...
Kwa jinsi Mambo yanavyokwenda katika nchi hii Nina wasiwasi kama viongozi wa sasa wanataka hali! Mwenye Akili ataona maandalizi yanayofanyika yana nia ovu... Jamani tunawaomba muache michezo hiyo kwa kuwa Tanzania ni nchi ya wote. Kukiwa na Matatizo sote tutapata shida, taabu na mahangaiko.... Mungu ibariki Tanzania