Gari Ghali Zaidi Duniani: Mercedes 300 SLR!

bless on

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2026
Posts
1,113
Reaction score
2,718
Kama unadhani Bugatti Chiron ya dola milioni 3.5 (TSh bilioni 9.5) ndiyo mwisho wa matumizi ya kijinga ya fedha, basi hujaiona 1955 Mercedes-Benz 300 SLR Uhlenhaut Coupé iliyouzwa kwa dola milioni 142 (TSh bilioni 380)!

Kwa bei ya Mercedes hii moja tu, unaweza kununua msururu wa Bugatti Chiron 40 mpya kabisa na bado ukabakiwa na chenji ya kununua kisiwa!

Kwanini chuma cha mwaka 1955 kiwe cha bei mbaya hivi?

1. Ukigonga Bugatti unalia; ukigonga Mercedes unafuta historia
Ukigonga Bugatti Chiron, unapigia simu bima na kuagiza ingine mpya. Ukigonga hii Mercedes 300 SLR, hujagonga gari—umefuta sura nzima ya historia ya Mercdes.

2. Bugatti zipo kibao; Mercedes zipo MBILI pekee duniani
Bugatti wametengeneza mamia ya Chiron. Mercedes walitengeneza magari Aina hii MBILI TU mwaka 1955. Moja ipo makumbusho milele, na ya pili ndiyo hii iliyouzwa. Hata uwe na pesa za kununua nchi, huwezi kupata ya tatu!

3. Roketi ya Formula 1 ya mwaka 1955
Hii ilikuwa ni gari la mashindano ya Formula 1 lililowekwa taa ili litembee mtaani. Mwaka 1955 mhandisi wake alikuwa akiendesha kwenda kazini kwa kasi ya 290 km/h—wakati magari mengine yakijaribu kufikisha 100 km/h injini zilikuwa zinalipuka!

Leo tumeushtua umaskini kidogo, MUNGU atutie nguvu ya kupambana walau hata tusipo miliki magari kama hayo, basi tupate uhakika wa ugali wa kula na matumizi mengine ya muhimu tusiwe wasindikizaji hapa DUNIANI.
 
Attachments

  • Bugatti_Chiron_1.jpg
    Bugatti_Chiron_1.jpg
    1,013.3 KB · Views: 4
  • images (3).jpeg
    images (3).jpeg
    12.4 KB · Views: 6

Mwaka 1955 mzungu anafanya haya mambo aseeh kweli sisi tumechelewa sana
 
Back
Top Bottom