(GMT+08:00) 2011-02-23 18:01:15
Vurugu ziliyosababishwa na maandamano yaliyofanyika kwa siku mfululizo nchini Libya imesababisha vifo vya zaidi ya watu mia moja. Kiongozi wa Libya Bw. Muammar Gadhafi tarehe 22 alitoa hotuba akisema, kamwe hatajiuzulu na hataondoka nchini Libya katika siku za baadaye, bora awe mtu wa kujitolea mhanga.
Serikali ya Libya jana usiku ilitangaza kupitia televisheni ikisema, vurugu hizo imesababisha vifo vya raia na askari 300, lakini takwimu kutoka televisheni ya Al Jazeera zilionesha kuwa watu 500 wamefariki kutokana na vurugu hizo na wengine 1, 400 hawajajulikana walipo. Habari nyingine zinasema, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa tarehe 22 liliitisha mkutano wa dharura kuhusu hali ya Libya, na kuitaka serikali ya Libya ikomeshe mara moja vurugu hizo na kukidhi matakwa halali ya wananchi hatua kwa hatua.