Gaddafi: BASI KUPIGANA JAMANI, aomba asifanywe vibaya.

Pharaoh

JF-Expert Member
Mar 18, 2011
843
157
Hatimae Dikteta Muammar al Gadhafi ameiomba Nato isimamishe vita na yeye yuko tayari wanavyotaka, ilimradi asihamishwe nje au kuuawa.
yuko tayari kuipisha Libya mpya ijengwe na wengine, lakini abaki nyumbani na salama yeye na wanawe.
kwa nini alijidanganya tangu mwanzo?
 
mi ningemshauri atimke tu na mabilioni yoote na Dhahabu shehena ya Taifa, aje tumpe kisiwa kidogo yeye na familia yake wajenge na kutulia, tutamhakikishia usalama.
 
Naendelea kutizama maendeleo ya vita hii hadi mwisho wake. Kilicho dhahiri ni kuwa kwa vyovyote vile matokeo ya mwisho wa vita hii yatashawishi maendeleo ya kisiasa katika ukanda wa afrika ya kaskazini, mashariki ya kati na kwa namna flani afrika kusini mwa jangwa la sahara. Ngoja tusubiri nini kinafunguka kadiri siku ziendavyo.
 
Kwa hiyo kafulia?....kila chenye mwanzo hakikosi kuwa na mwisho...
 
Alishindwa Sadam ambaye hakuwa na waasi nchini kwake itauwaje yeye ambaye ana wanaompinga kwa silaha?
 
Dah? Mwana angekuja huku tumpe ukatibu mkuu wa nchi ingekuwa poa sana...
 
huyu mzee angesoma alama za nyakati wananchi wakisha kupinga aina jinsi ni mengi amefanya alipokuwa madarakani kwa wananchi wake ila pia alijisahau kuwa nchi hiyo siyo yake pekee yake inawengine pia wanataka waitawale kwa sababu ni yao pia na wanaye wakaingilia maamzi ya wananchi wenzao na kuanza kupiga watu wasio na hatia ndivyo ilivyo kwa mtu yeyote aliye ua kwa upanga basi naye atauwawa kwa upanga aliyebakia ni mugabe na ubabe wake wa kutawala nchi anavyotaka yeye,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom