Libya: Mtoto wa Gaddafi Saif al-Islam yuko hai ataka kuongoza Libya

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879

Libya: Mtoto wa Gaddafi Saif al-Islam yuko hai ataka kuongoza Libya​

31 Julai 2021
Saif al-Islam

CHANZO CHA PICHA,MAHMUD TURKIA/AFP VIA GETTY IMAGES
Saif al-Islam, mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa Libya Muammar al-Gaddafi, anasema anataka "kurejesha umoja" nchini humo .
Islam mwenye umri wa miaka 49, katika mahojiano na gazeti la Marekani la New York Times, alizungumza kuhusu mambo mengi yanayohusiana na nchi hiyo ya Kaskazini mwa Afrika ya Libya na siasa.
Pia hakufuta uwezekano wa kugombea urais nchini Libya.
Mnamo Agosti 2011, takribani muongo mmoja uliopita, waasi walidhibiti mji mkuu wa Libya Tripoli. Baada ya hayo, mnamo Oktoba 2011, Gaddafi alipigwa aliuawa kwa kupigwa risasi .
Saif al-Islam, aliyewahi kufikiriwa kuwa mrithi wa baba yake, anasema viongozi wa Libya "hawajaleta chochote ila mateso" kwa watu nchini Libya katika miaka 10 iliyopita.

'Libya inavuja hakuna pesa wala usalama'​

Islam , ambaye alionekana baada ya miaka mingi, alisema, "Sasa ni wakati wa kurudi nyumbani nchi inaangamia ... hakuna pesa, hakuna usalama. Hakuna maisha."
Alifanya mahojiano haya na New York Times ndani ya jumba la kifahari la ghorofa mbili .
Saif al-Islam, aliyewahi kufikiriwa kuwa mrithi wa baba yake

CHANZO CHA PICHA,REUTERS
Islam alisema katika mahojiano hayo kuwa sasa yeye ni mtu huru na anajiandaa kurudi tena katika siasa .
Alidai pia kwamba watu ambao walikuwa wamemfunga jela hapo awali sasa wamekuwa 'marafiki' zake.
Atakubaliwa kurejea Libya?
Hatahivyo, kurudi kwa Islam nchini Libya hakutakuwa rahisi. Sio tu kwamba anakabiliwa na shutuma za uhalifu wa kivita dhidi ya binadamu katika mahakama ya ICC, anakabiliwa pia na hukumu ya korti moja ya Tripoli
The New York Times iliandika kwamba licha ya haya yote, mtoto wa Muammar Gaddafi Saif al-Islam anaonekana kuwa 'thabiti'.
"Nina hakika masuala haya ya kisheria yanaweza kutatuliwa ikiwa watu wa Libya watanichagua kuwa kiongozi wao," alisema.
Islam aliongeza , "Nimekuwa mbali na watu wa Libya kwa miaka 10. Ili kurudi, nitalazimika kufanya kazi polepole kama mchezaji densi anayeitikia mirindimo ya muziki . Kucheza na akili za watu kidogo."
Mnamo mwaka wa 2011, wakati alikuwa akikimbia kuokoa maisha yake, je! Hakuona ni ajabu kujificha katika nyumba za watu nchini Libya?
Kujibu swali hili, Islam ilisema, "Sisi ni kama samaki na watu wa Libya ni kama bahari kwetu. Bila wao tutakufa. Kutoka kwao tunapata msaada. Tunajificha hapa na kupigana hapa." . Watu wa Libya ni bahari zetu. "
Saif Al Islam alikuwa wapi hadi sasa?
Saif Al Islam ana PhD kutoka London School of Economics. Hakuna habari kamili juu ya mahali alipokuwa kwa miaka kadhaa iliyopita.
Islam anashutumiwa kwa uhalifu wa kivita na kwa hivyo Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) pia ilikuwa ikimtafuta.
Alikuwa akikimbia kwa karibu miezi mitatu baada ya waasi kuchukua udhibiti wa Tripoli mnamo 2011, lakini akakamatwa na kufungwa na waasi.
Saif al- Islam

CHANZO CHA PICHA,KARIM JAAFAR/AFP VIA GETTY IMAGES
Waasi walikuwa wamemfunga katika mji wa Xintan kwa karibu miaka sita, lakini katika mwaka wa 2017 habari za kuachiliwa kwake zilijitokeza.
Hatahivyo, haikujulikana kwa sababu gani aliachiliwa na yuko wapi baada ya kuachiliwa.
Mnamo mwaka wa 2015, alihukumiwa kifo na korti ya Tripoli lakini kundi moja lenye msimamo mkali wa kidini lilikataa kumsalimisha.

Islam wakati mmoja alitazamwa kuwa kama mwanamageuzi​

Miaka mingi iliyopita, Saif al-Islam alionekana kama sura ya mageuzi katik utawala wa baba yake Gaddafi wakati alipokuwa na jukumu muhimu katika kuboresha uhusiano wa Libya na nchi za Magharibi.
Lakini baada ya hii, mnamo mwaka 2011, alishtumiwa kuchochea mauaji ya waandamanaji waliokuwa wakipinga utawala wa baba yake.
Islam wakati wa mazishi ya kaka yake, Picha:Mei 2 mwaka 2011

CHANZO CHA PICHA,AFP VIA GETTY IMAGES
Muammar Gaddafi na familia yake walikuwa madarakani nchini Libya kwa karibu miongo minne, lakini baada ya Mapinduzi ya Kiarabu mnamo 2011, uasi uliibuka huko pia.
Katika machafuko hayo , waasi walichukua udhibiti wa mji mkuu Tripoli, na kisha Gaddafi akauawa na waasi .
Watoto saba wa kiume wa Gaddafi pia waliuawa katika kipindi cha uasi , lakini Islam kwa namna fulani alifaulu kutoroka.
Kabla ya mahojiano haya, Saif al-Islam alionekana mara ya mwisho mnamo 2014 kupitia video kutoka mji wa Xintan kwenye kesi yake katika mahakama moja ya Tripoli.
 
Maswali yote haya aulizwe CIA. Na kama kweli huyu bwana yupo hai,basi kauli zake hizi na kufanikiwa kwake kunapangwa na CIA. Kama wameshapanga hili kwa maslahi yao, hakuna atakaezuia. Utashangaa jinsi jamaa anapewa nchi hata kwa shaba. Atapewa kauwezo kadogo ka kuua wapinzani na kuleta amani itakayowatosha kina BP, ESSO, TOTAL, n.k kukaa na kunyonya mafuta , kwisha kazi.
 
Wazungu ni wabaya sana,
Halafu kuna watu tena weusiiii na hata weupe pia wapo wanapenda na kuukumbatia uzunguuuu,
Shtuka chukua hatua sasa
 
Back
Top Bottom