Gaddafi amlaumu Osama

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Gaddafi amlaumu Osama

Kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi amekiambia kituo cha televisheni cha taifa kuwa Osama Bin Laden na wafuasi wake, ndio wa kulaumiwa kwa maandamano yanayotikisa nchi yake.


Muammar Ghaddafi

Katika hutuba aliyotoa kupitia simu, mahsusi kwa ajili ya wakazi wa mji wa al-Zawiya, Kanali Gaddafi amesema vijana wanadanganywa kwa kupewa dawa za kulevya na pombe ili washiriki katika "uharibifu na hujuma".

Kanali Ghaddafi anajitahidi kurejesha udhibiti wa mji mkuu Tripoli na maeneo ya magharibi.

Waandamanaji wamekuwa wakipata nguvu katika miji ya mashariki.


Mmoja wa waandamanaji akichoma picha ya Gaddafi

Wanasiasa wa upinzani na viongozi wa kikabila wamefanya mkutano muhimu katika mji wa mashariki wa al-Badya, kuonesha umoja dhidi ya Kanali Gaddafi.

Hotuba hiyo ililenga mji wa al-Zawiya uliopo kilomita 50 magharibi mwa mji mkuu, ambapo kumekuwa na ripoti za milio ya risasi mitaani.


Osama bin Laden

Kanali Ghaddafi amesema waandamanaji hawana madai yenye msingi, na walikuwa wakiongozwa na kiongozi wa al-Qaeda.

"Bin Laden.... huyu ndio adui anayewadanganya watu. Msidanganywe na Bin Laden," amesema.

"Ni wazi kuwa sasa jambo hili linaongozwa na al-Qaeda. Vijana wenye silaha, watoto wetu, wanachochewa na watu ambao wanatafutwa na Marekani na nchi za Magharibi.

"Wale wanaochochea ni wachache, na hatuna budi kuwakamata."

Amesema vijana hao waandamanaji "wanafurahia kupiga risasi hasa wakiwa wamelewa".

Amesema Libya sio kama Misri na Tunisia, ambazo zimeshuhudia viongozi wao wakiondolewa madarakani, kwa sababu watu wa Libya wana uwezo wa kubadili maisha yao kwa kupitia kamati.

BBC Swahili - Habari - Gaddafi amlaumu Osama
 
Mfa maji hakosi kutapatapa; It remains to be seen how long this guy will manage to hold on to power - my take ni kwamba Ghadaffi amepania kubaki madarakani at all cost even if it means killing all the Libyan people!
 
Back
Top Bottom