Osama Bin Laden HardDrive Documentary imethibitisha kwenye Harddisk za Osama zilikuwa zina pornography

BabaMorgan

JF-Expert Member
Dec 18, 2017
4,050
10,490
Baada ya shambulio la mauaji ya Mastermind wa September 11 the only and one Osama Bin Laden aliyekuwa tishio kwa Marekani wataalamu wa uchunguzi walienda extra mile kukagua vitu vyake hususani electronic devices.

Kwenye Harddisk zake walikuta email za kimkakati alizokuwa akiwasiliana na kutoa order kwa watu wake, video zilozorekodiwa zikionyesha mazingira ya alipokuwa akiishi kwa siri, video za katuni na video za ngono.

Video za ngono wataalamu wanashindwa kuhitimisha kuwa video hizo za ngono zilikuwa zikitizamwa na Osama Bin Laden wanatoa suggestions inawezekana kuwa watoto wa Osama Bin Laden ndio walikuwa wakitazama hizo video na hii ni kutokana na personality na misingi ya dini aliyokuwa nayo Osama.

Mtazamo wangu katika information age ni ngumu sana kumtenganisha mtu na sexual contents.
 
sikumbuki lakini kuna mahala niliona haohao CIA wanasema Osama akuwa akitumia mawasilino yoyote ya kimtandao.
Hard drive sio kifaa cha mawasiliano ya kimtandao. Yani kuwa na DVD player (deki kwa kibongo) au kuwa na USB flash drive au memory card pamoja na TV set hakukufanyi uwe miongoni mwa watu wenye vifaa vya mawasiliano ya kimtandao.

Osama alikuwa anakwepa kutumia satellite communication na cellular connection sababu zinaweza kuwa tracked. Ila analog DVD player na TV zikionyesha movie unatrack vipi wakati hamna mawimbi yanatumwa au kupokelewa.

Usingeweza kumuona Osama na simu au kompyuta, alitumia messengers wakibadilishana barua na maagizo ya mdomoni.
 
Osama huyo huyo alikua akishirikiana na USA na kumpiga Mrusi, Osama huyo huyo watu wake alipshirikiana nao kulipua 9/11 walikua uraiani Marekani na Fbi wakikata kuwakamata CIA wanawakongia kifua, Al Qaeda hao hao Mossad wanasema hawana Ugomvi nao ndio maana wanawatibu. Connect dot.
 
1. Osama hajawahi shirikiana na Marekani, ni Mujahideen pekee ilishirikiana na Marekani kuiondoa Soviet Union pale Afghanistan.

2. Hao Al Qaeda walipotakiwa kukamatwa na FBI ila CIA inakataa ni kina nani majina yao.

3. Mossad haitibu watu, sio wizara ya afya ile. Na wala Israel haitibu Al Qaeda tu, inatibu mtu yeyote yule as long as ni binadamu haijalishi ni mwizi, gaidi, mkimbizi, Mwislamu au Mkristo. Mkuu wa Hamas bwana Haniyeh yeye watu wake wameishatibiwa Israel mara kadhaa. Mjukuu wake, mamamkwe wake, mpwa wake, shemeji yake na dada yake wote waliwahi tibiwa Israel na kuna mmoja katibiwa wiki jana.

Hata Hamas waliojeruhiwa kwenye shambulizi lao mwaka jana walitibwa ushahidi upo.
 
Mujahideen sio mtu ama kikundi, ni muunganiko wa vikundi, for your Information Ayman Al Zawahir second in Command wa Osama alikua amefungwa Egpty, Ni USA ndio wali wa pressure Egpty wamuachie akaenda Afghanistan na Osama pamoja na wenzake kina Zawahir walipokea Misaada toka USA kupigana na Urusi.

Soma hapo, Taliban walikua tayari kumtoa Osama ila USA hawakutaka, na wakaendelea na vita.
2. Hao Al Qaeda walipotakiwa kukamatwa na FBI ila CIA inakataa ni kina nani majina yao.

Hio hapo article yenye Ushahidi wa Kutosha kwamba CIA waliwalinda Saudi waliolipua 9/11 ambao hao hao tumeambiwa ni Al Qaeda.
3. Mossad haitibu watu, sio wizara ya afya ile. Na wala Israel haitibu Al Qaeda tu, inatibu mtu yeyote yule as long as ni binadamu haijalishi ni mwizi, gaidi, mkimbizi, Mwislamu au Mkristo. Mkuu wa Hamas bwana Haniyeh yeye watu wake wameishatibiwa Israel mara kadhaa. Mjukuu wake, mamamkwe wake, mpwa wake, shemeji yake na dada yake wote waliwahi tibiwa Israel na kuna mmoja katibiwa wiki jana.

Hata Hamas waliojeruhiwa kwenye shambulizi lao mwaka jana walitibwa ushahidi upo.
Kwa hio kwako wewe ni sawa Israel Kuwatibu Al Qaeda kundi hatari Duniani na kuwaachia wakapigane Tena? Tena sio tu Kuwatibu mpaka Viongozi wa Serikalini kwenda kuwatembelea Wodini? Kwa mahaba kama haya? Hebu try to Convince me hili ni jambo la kawaida.
n00655052-b.jpg

Pia Hamas ni kundi lililoanzishwa na Israel ambalo limeasi kwao, wao kuwa na past relationship na Israel si jambo geni.
 
Mujahideen sio mtu ama kikundi, ni muunganiko wa vikundi, for your Information Ayman Al Zawahir second in Command wa Osama alikua amefungwa Egpty, Ni USA ndio wali wa pressure Egpty wamuachie akaenda Afghanistan na Osama pamoja na wenzake kina Zawahir walipokea Misaada toka USA kupigana na Urusi.
Mama akizaa mtoto na baadae mtoto akiwa mtu mzima akawa kibaka tunasema mama alizaa kibaka? Mtoto mwenyewe si ndio ameamua ukubwani kuwa kibaka. Angeamua kuwa sheikh au mchungaji angeweza pia.

Mbona kuna members wa Mujahideen walipigana na Urusi, baadae wakapigana na Marekani, baadae wakapigana na serikali zao za Kiarabu, baadae wakapigana na Urusi na Iran tena wakiwa ISIS. Hivyo tuseme Iran, Russia, USSR, US, nchi za Kiarabu wote kwa pamoja waliunga mkono magaidi.
Hio hapo article yenye Ushahidi wa Kutosha kwamba CIA waliwalinda Saudi waliolipua 9/11 ambao hao hao tumeambiwa ni Al Qaeda.
Zipo articles zinazodai zina ushahidi wa kutosha kwamba Al Qaeda walihusika. Kama issue ni articles hata mia naweza ziweka.
Kwa hio kwako wewe ni sawa Israel Kuwatibu Al Qaeda kundi hatari Duniani na kuwaachia wakapigane Tena?
Ndio ni sawa, Israel haiendeshwi kwa roho za kwanini na ugaidi mioyoni. Kila majeruhi ana haki kama raia mwingine wa kawaida, kila mtuhumiwa ana haki ya kusikilizwa ndio maana Israel kuna wafungwa magaidi ingekuwa ni tit for tat hao magaidi wangeuwawa. Hao sio wale mwizi akatwe mkono. Unashangaa Al Qaeda, hapa ni mwaka jana, gaidi la Hamas limempiga risasi ya mgongo binti, nalo likapigwa risasi na askari. Wote wako hospitali moja, chumba kimoja
1000250200.jpg
Bado waliojeruhiwa Gaza wanatibiwa
1000250199.jpg

Bado family member mmoja wa mkuu wa Hamas last week katibiwa Israel. Waliozoea kujilipua hawaelewi huu ubinadamu.
Tena sio tu Kuwatibu mpaka Viongozi wa Serikalini kwenda kuwatembelea Wodini? Kwa mahaba kama haya? Hebu try to Convince me hili ni jambo la kawaida.
View attachment 2897846
Huyo si ni mgonjwa kwenye hospitali ya Israel. Kuna ajabu gani kiongozi wa Israel kutembelea hospital na kumuona.
Pia Hamas ni kundi lililoanzishwa na Israel ambalo limeasi kwao, wao kuwa na past relationship na Israel si jambo geni.
Past relationships za lini. 2008, 2012, 2014, 2021, 2022 na 2023 &2024 Israel na Hamas wamepigana. Familia ya mkuu wa Hamas, Haniyeh waliotibiwa nchini Israel:

1. Mjukuu wake alitibiwa mwaka 2013

2. Mama mkwe alitibiwa 2014

3. Dada yake kajifungulia Israel mwaka huu (kwa makafiri ambapo nchi yao imelaaniwa na Joshua Mollel Mtanzania aliuwawa kwa sababu ameenda nchi ya makafiri). Alikuwa na complications ndio maana.

4. Mwaka 2014 binti yake akatibiwa

5. Mwaka 2021 mpwa wake akatibiwa

Alafu kwanini kila kinachotokea kwa magaidi wa Kiarabu inasingiziwa Israel. Ina maana ukiachana na kutokula kitimoto na kuoa wake wengi, mambo mengine yote hao Waarabu wanafuata maelekezo ya Israel? Hata wakiamua kujifia, Israel inalaumiwa.
 
Hard drive sio kifaa cha mawasiliano ya kimtandao. Yani kuwa na DVD player (deki kwa kibongo) au kuwa na USB flash drive au memory card pamoja na TV set hakukufanyi uwe miongoni mwa watu wenye vifaa vya mawasiliano ya kimtandao.

Osama alikuwa anakwepa kutumia satellite communication na cellular connection sababu zinaweza kuwa tracked. Ila analog DVD player na TV zikionyesha movie unatrack vipi wakati hamna mawimbi yanatumwa au kupokelewa.

Usingeweza kumuona Osama na simu au kompyuta, alitumia messengers wakibadilishana barua na maagizo ya mdomoni.
E.mail je??
 
Back
Top Bottom