G55 walamba vyeo Chaumma

Kwa kweli kwa sasa sina kabisa imani na hivi vyama vyetu vya upinzani hapa Tanzania haswa baada ya kugundua kuwa Zitto na Mbowe walikuwa vibaraka wa CCM. Mtu pekee ambaye angeweza kuleta mapinduzi hapa Tanzania ni Lissu na CCM inajuwa hivyo na ndiyo maana wanamfanyia figisu makusudi tu kumtikisa na kumpakazia habari za uongo ili wananchi wamuone kuwa ni gaidi. CCM imeshindwa kuliongoza hili taifa na ndiyo maana wanatumia ushenzi kutaka kubakia madarakani kwa nguvu.
 
Makubaliano? Ya nani na nani? Vyeo vinatolewa kwa makubaliano? Duh Haya msajili wa vyama kazi kwako
 
Naomba nikiri kwamba msajili wa vyama ni mpumbavu! Yaani vyeo vya kupigiwa kura vinagawiwa kama njugu? Ni lini chaumma kiliitisha uchaguzi mkuu?
 
😂😂😂😂kituko mwanachama wa siku moja.... Anapewa na cheo..... Hivi ni vituko vya mwaka
Unaona ni kituko sasa hivi? Kwani lowassa alipokodishiwa chama kugombelea urais alikuwa mwanachama wa miaka mingapi?
 
Kumbe madai kuwa G55 ni "mradi" fulani wanaweza kuwa sahihi!
 
Hao waliojiuzulu wamelipwa stahiki zao kama walivyokubaliana?
 
Salum Mwalim Ufanye kazi Channel Ten na Magic Fm yenye makao makuu pale katikati ya jiji la Dar kwenye makao makuu ya Chama, kwa miaka mingi halafu leo hii uje utuambie wewe ni MPINZANI WA CCM?

Anyway pesa ya ruzuku tamu nyie
 
Na mfadhili wa chama atakuwa ni Aikael
 
Same thing waliyofanya Chadema walipompokea na kumpa agombee uraisi.
Acha kupotosha.
Lowassa kwanza alipokelewa kama mwanachama wa kawaida.
Kisha baadaye akachukua fomu ya kuomba kugombea urais kwa kuwa mchakato wa kufanya hivyo ulikuwa tayari umetangazwa.
Jina lake likajadiliwa na kamati kuu na baadaye mkutano mkuu ukaitishwa na jina lake likapigiwa kura na kuidhinishwa kuwa mgombea urais.

Lowassa hakupokelewa na kuwa kiongozi wala kupewa fomu za kugombea urais.
 
Natamani waitishe mkutano kama anavyofanya Heche
 
Sure
 
Aisee kwani hapo msajili ana comment gani kwao, uanachama na cheo cha juu kabisa on the same day. Waliokuwa kwenye hizo nafasi wameelekea wapi.

Kwamba unahitaji kuwa na D 2 kujua usanii wa kisiasa hapa nchini, haya matawi ya kijani ni shida sana
 
Msajili ana semaje hawa wamepewa vyeo kikatiba sio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…