Fuso tatu za Mbowe zaigawa CHADEMA; Adaiwa kuchimbia kibindoni milioni 438/- : UHURU | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fuso tatu za Mbowe zaigawa CHADEMA; Adaiwa kuchimbia kibindoni milioni 438/- : UHURU

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, May 5, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Thursday, 05 May 2011 20:36 administrator  * Adaiwa kuchimbia kibindoni milioni 438/-
  * Dk. Slaa naye alipwa mshahara wa milioni 7.144/-
  * Adaiwa kununuliwa gari la milioni 78/-

  NA MWANDISHI WETU

  UAMUZI wa Kamati Kuu ya CHADEMA kununua magari matatu aina ya Fuso kutoka kwa Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe kwa zaidi ya sh. milioni 438 umewagawa wanachama. Hatua hiyo inatokana na wanachama hao kudai ni mpango maalumu wa kujinufaisha kwa Mbowe na Katibu Mkuu wake, Dk. Wilbroad Slaa kupitia ruzuku ya chama. Mbali na hilo, wanachama hao pia wamedai kuwa viongozi hao wamekuwa wabaguzi kwa viongozi wengine kutoka Zanzibar katika utoaji wa fedha za kuimarisha chama visiwani. Habari za kuaminika kutoka CHADEMA zinasema viongozi hao wamekuwa wakikingiana kifua kwa kila jambo linalogusa maslahi yao kwa wajumbe wengine wa Kamati Kuu. "Hatukubali katika hili... tume iliyoundwa na Katibu Mkuu kumshawishi Mwenyekiti kununua magari hayo ni yao wenyewe hasa kutokana na robo tatu ya wajumbe wa Kamati Kuu kuwa wao,'' alidai mmoja wa wanachama. Alidai mazingira hayo yanatoa fursa ya kufikiwa kwa uamuzi wa kukubali kununua malori hayo licha ya sheria ya manunuzi ya umma kutaka kuitishwa kwa zabuni juu ya manunuzi yoyote. Hata hivyo, chanzo chetu cha habari kilisema zabuni hiyo haijaitishwa na badala yake Katibu Mkuu alisema magari hayo yanapaswa kununuliwa na chama.

  [​IMG]


  "Dk. Slaa kusema kuwa malori hayo yalinunuliwa na Mbowe kwa biashara zake binafsi, lakini kwa kuwa chama kina matatizo ya usafiri ni vyema wayanunue ni mbinu zao kujinufaisha,'' alidai mwanachama huyo. Chanzo hicho kilidai kuwa hata uamuzi wa kumlipa mshahara na posho wa sh. milioni 7.144, Dk. Slaa ni uamuzi wa kumnufaisha kwa kuwa endapo akiondoka, mshahara huo hawezi kulipwa katibu mkuu yeyote.

  "Huu si utaratibu wa chama, bali unaonyesha kuwa chama kinaongozwa kwa sura, hasa ikizingatiwa awali Dk. Slaa alipokuwa bungeni alikuwa anasema mshahara kama huo anaolipwa mbunge ni mkubwa mno kwa nchi masikini kama Tanzania. "Watanzania wanapaswa kuwa makini na kauli za Dk. Slaa na Mbowe, kwani ni watu wenye kuamua mambo yao binafsi na ndio maana wamekuwa wakiuziana magari ya misaada kutoka kwa wahisani na kusema ni yao,'' kilidai chanzo hicho.

  Mgawanyiko huo pia umechangiwa na uamuzi wa Mbowe kupitia Kamati Kuu wa ununuzi wa gari aina ya Land Cruiser VX lenye namba za usajili T 843 ABJ kwa ajili ya Dk.Slaa. "Katibu Mkuu kanunuliwa gari kwa sh. milioni 78, lakini gari hilo ni miongoni mwa magari yaliyopatikana kutokana na fedha za misaada ya wahisani kukimarisha chama, lakini mwisho wa siku Mbowe anasema gari ni lake,'' chanzo hicho kilidai. Aidha, chanzo hicho kilidai kuwa viongozi hao wamekataa kuongeza sh. milioni 25 kwa ajili ya ununuzi wa jengo la ofisi ya kudumu ya chama visiwani Zanzibar. Jengo hilo linauzwa sh. milioni 45. "Wabunge wa CHADEMA kutoka Zanzibar walichanga na kufikisha sh. milioni 20 na kumuomba Katibu Mkuu awaongeze sh. milioni 25 ili wanunue kwa sh. milioni 45 ili kuepuka kodi ya sh. milioni 1.2 kwa mwaka, lakini alikataa,'' alidai mwanachama huyo.

  Viongozi hao kila wanapohojiwa na waandishi wa habari kutoa ufafanuzi wa madai hayo wanadai maamuzi yote yalifikiwa na Kamati Kuu na si uamuzi wa mtu mmoja mmoja ndani ya chama.
   
 2. G

  Giddy Mangi JF-Expert Member

  #2
  May 5, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 833
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  crap!ccm mnahangaika sana
   
 3. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #3
  May 5, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  majungu!!
   
 4. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #4
  May 5, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Gazeti gani hili mkuu???
  ahaaaa UTUMWA linalomilikiwa na MAGAMBA PARTY?
  NAPITA TU
   
 5. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #5
  May 5, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  hakuna "content" yoyote hapo
   
 6. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #6
  May 5, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  angaikieni magamba
   
 7. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #7
  May 5, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Mkaloge !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Hamtupati ngooooooooooo wafitini wakubwa C-C-M!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!uchwara mkaote jua mnasikia tu baridi baada ya kujichuna ngozi
   
 8. Dickson Ng'hily

  Dickson Ng'hily Verified User

  #8
  May 5, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60

  CCM....Mmeishiwa.....tehe tehe tehe tehe tehe...hahaha hahaha hahaha hahaha...kwikwi kwikwi kwikwi kwikwi....
   
 9. kitungi

  kitungi Senior Member

  #9
  May 5, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #10
  May 5, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,137
  Trophy Points: 280
  CCM bwana kweli wanasikitisha, wanatunga stori za kuwachafua na kuwachonganisha wana Chadema
   
 11. h

  hoyce JF-Expert Member

  #11
  May 5, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 1,119
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  wanaogopa kutaja gazeti gani
   
 12. fige

  fige JF-Expert Member

  #12
  May 5, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 376
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  aisee ajira ngumu siku hizi ,kumbe hata kuuza umbeya nayo ajira aisee !!!!!
   
 13. mwanapolo

  mwanapolo Senior Member

  #13
  May 5, 2011
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 194
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Watz sasa wanajua mbivu na mbichi. Sio kama zamani mpaka wahadithiwe
   
 14. Kitumbo

  Kitumbo JF-Expert Member

  #14
  May 5, 2011
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 547
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Uongo unapoisha inabidi urudierudie ili uendelee kuonekana unaongea...
   
 15. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #15
  May 5, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,684
  Likes Received: 642
  Trophy Points: 280
  Itachukua muda nyie kuwaelea hawa watu!.............ila mtawaelea tu!
   
 16. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #16
  May 5, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  hivi ile kesi ya kapteni john komba kujinufaisha na magari ya ccm TOT iliishia wapi?mbona amepata tena ubunge kupitia ccm?
   
 17. j

  jnuswe JF-Expert Member

  #17
  May 5, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,271
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  mchango wangu kwenye umbeya huo, wewe unaeongea habari ya gari la 78 million ni nyingi , akili huna, ulitaka katibu anunuliwe mkokoteni ? hicho kiasi ni cha kawaida mmno, jaribu kuleta hoja zenye maana , hii si hoja, na suala la posho mwache Dr. wa ukweli aendelee kulipwa hiyo anastahili ,huyo ni sawa na viongozi wenu wengine wajuu, sio katibu kama makatibu wa vyama vingine choka mbaya, ni mtazamo wangu
   
Loading...