Fusion Leviathan: Ni Kompyuta Yenye Kasi Duniani

Fusion Leviathan: Ni Kompyuta Yenye Kasi Duniani

ManiTek TV

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2011
Posts
410
Reaction score
159

​
Ukizungumzia kompyuta za mezani, Fusion Leviathan ni mashine ambayo haina mpinzani kwa sasa katika kasi na nguvu. Hapa hatuzungumzii kupendeza kama kule kwa gajeti za Apple, tunazungumzia uwezo wa kompyuta kupiga mzigo na kuwa na ufanisi wa kila namna kwa matumizi ya kompyuta ya leo na hata miaka 20 ijayo. Kabla ya kueleza vielelezo vya kompyuta hii, tunatabiri kwamba kompyuta za Apple ambazo ni kompyuta za urembo labda zitafikia kasi na uwezo wa kompyuta hii mwaka 2020, weka msisitizo kwenye neno LABDA.


Kompyuta hii imetengenezwa na kampuni isiyo na umaarufu mkubwa inayojulikana kama Chillblast iliyoko Uingereza, taarifa za kompyuta hii ni kwa mujibu wa mtandao rasmi wa Chillblast na jarida la Tech toleo la wiki inayoanzia tarehe 28/03/2013. Prosesa ya Fusion Leviathan ni Intel Xeon yenye koo (core) 12, ikiwa na jumla ya kasi ya 55.2 Ghz kwa pamoja. Hivyo kasi ya koo hizo ni 4.6 kwa kila moja wapo. Mashine hii ina RAM kiasi cha 48 GB, hata hivyo ina slot za kutosha za kuiongezea RAM hadi kufikia 768 GB.


Huu ni wazimu kwa sababu hakuna anayehitaji nguvu ya namna hii katika shughuli yoyote ya desktop, hivyo hii ni kompyuta iliyoutangulia wakati kwa muda mrefu sana. Chillblast walitakiwa waitoe kompyuta hii miaka 15 ijayo. Disk ina ukubwa wa 21 TB, kwa waliozoea GB zidisha 21 mara 1024, hivyo ni 21,504 GB. Hii unaweza kutumia umri wako wote bila ya kuijaza na sijui utawezaje kuzimudu (manage) data za namna hii.


​
Bei ya kuanzia ni $2,499. Hata hivyo utakapochagua nini unataka uwekewe kwenye kompyuta hii bei inaweza kufikia $26,000 bila ya kupata taabu sana. Hivyo kompyuta hii sio tu ina nguvu bali bei nayo si ya kawaida ukizingatia kwa bei ya $26,000 unaweza kupata gari ya maana ikiwa na maili 0, yaani mpya kabisa. Bila ya shaka yoyote Chillblast wameitengeneza kompyuta hii kwa ajili ya watu wenye ugonjwa (addiction) wa kompyuta na wenye fedha ya ziada ambayo haina kazi. Yaani wale ambao pesa sio tatizo, tatizo ni matumizi.


Chillblast pia wanatengeza kompyuta mbali mbali zenye nguvu kubwa kwa bei nzuri, mashine kama vile Silverstone, Fusion 7 na Fusion Thunderbird. Ingawa hizi hazina nguvu kama ya Fusion Leviathan lakini itazizidi kompyuta nyingi tu za hali ya juu, na pia unaweza kuipata kwa bei nafuu sana ukilinganisha na iMac ya mwaka 2013. Chillblast wanafanya biashara kwa mtindo wa kupokea oda kwanza. Baada ya kutoa oda huchukua si zaidi ya siku 10 kukujengea kompyuta yako.

Chanzo:
 
Duh thanks for the information mkuu,jf chuo tosha
 
mkuu miaka 20 ijayo??? Omba mungu labda graphene isifae ila kila kitu duniani kitachange. Kwa graphene core moja tu yenye speed ya 500ghz inaieka hio pc into shame
 
duh design ya imagination hv!!!
 
mkuu miaka 20 ijayo??? Omba mungu labda graphene isifae ila kila kitu duniani kitachange. Kwa graphene core moja tu yenye speed ya 500ghz inaieka hio pc into shame
Ngoja nishangae tu.
Hata sijui ni nini!
 
Now I am not an Apple fan, never have been and never will. In fact I do not own a single Apple product.

Lakini.

Mtu yeyote anayesema kompyuta iliyopo sasa haiwezi kupitwa labda 2020 hafahamu trends za computing na Moore's Law and it's remnants inavyofanya computing isiwe that easily predictable.

Why, by 2020 people are focusing on targets of a paradigm shift, say quantum computing, that will make the entire concept of RAM as presented here just about medieval!
 
duuh hii PC labda wanunue kina #mengi maana bei si mchezo
:amen:
 
Wewe umeingilia fani za watu kweli kweli!Eti in speed ya 55.2 Ghz! speed ya computer siyo product ya number of cores na speed ya individual core! Fanya research kabla ya kupoteza watu. And for the record hiyo computer haipo hata kwenye top 10,na ukitaka kujua sifa ya kitu usiende kwenye site ya kampuni waliotengeneza coz wao lazima wasifie kitu chao kwamba it is the fastest
 
Keyser Söze;6032737 said:
Wewe umeingilia fani za watu kweli kweli!Eti in speed ya 55.2 Ghz! speed ya computer siyo product ya number of cores na speed ya individual core! Fanya research kabla ya kupoteza watu. And for the record hiyo computer haipo hata kwenye top 10,na ukitaka kujua sifa ya kitu usiende kwenye site ya kampuni waliotengeneza coz wao lazima wasifie kitu chao kwamba it is the fastest
Ingelikuwa vyema ungetaja desktop ambayo ina specs zilizo ni fasta kuliko hii (usije ukaleta mainframe computer au concept) kuliko tu kusema "fani za watu", kwa hiyo tubasubri hiyo yenye individual kasi zaidi ya 4.6 Ghz, RAM 48 na HD zaidi ya 21 TB halafu iko dukani inauzwa.
 
Wachumi wanapotqbiri future wana kyu wanaita CETERIS PETIBUS, halafu hii inajibu hoja yako
http://m.extremetech.com/extremetec...very-long-way-from,50ce8d3594f4be716930b738/4

angalia tena link yako mkuu, siwezi ifungua.

So wewe uliposema baada ya miaka 20 still hio computer ndo itakua na speed zaidi haikuhusu hio ceteris peribus? (na sio petibus)

maana ceteris peribus inamaanisha other factor remain constant so lazma na wewe u assume other factor zibaki vile vile ikiwemo graphene isifae

öñè mätèrîäl tö rûlè thèm äll
 
Keyser Söze;6032985 said:
click hyo top 10 ni link utaziona,

Nimeangalia chart yako ya PC World, a wameiweka Maingear Shift kama ndio top PC, Sasa hebu tuilinganishe na Fusion Leviathan:

Processor

Intel Core i7-3960X processor ndio iliyotumika kwenye ile ambayo PC World wameiweka top, hii prosessa ina clock speed ya 4.8 Ghz lakini ina Core 6 sidhani kama unaweza kulinganisha na Prosesa ya Fusion Leviathan ambayo clock speed ni 4.6 lakini in acore 12 .

RAM

Maingear Shift: 16 GG na Fusion Leviathan ni 48 GB.

HDD

Maingear Shift 3 TB + SSD 3 (kila moja 120 GB) na Fusion Leviathan 21 TB, hapa unaweza ku-argue huenda SSD zinaweza kuisaidia kasi Maingear shift, lakini kama unavyoona kwenye storage inaonekana mediocre.

External Drive

Zote zina aina moja ya Blueray Disk Drive. Na vitaka taka vingine vinafanana au kupishana kidogo.


Ulichokuwa hujazingatia ni kuwa list yako ni ya ina zaidi ya mwaka. (dated 7th March 2012). Nilidhani utakuja na clear cut winner, lakini sidhani kama ulizingatia sana uliposoma hii makala. The only desktop computer that could beat this one is Core MC Enterprise Pro, ambayo imetengezwa na Music Computing. Sijaiweka hii kwa sababu bado haipo madukani. (as far as I understand)

Kwa hiyo ile kauli yako umeingilia "fani za watu" na kuniamrisha nifanye research, wewe mwenye fani yako na uliyefanya research ndio umekuja na orodha ya mwaka jana ambayo top computer ina RAM 16 (sawa na Macbook Pro Laptop) na 3TB HD, halafu unalinganisha na PC yenye 48GB RAM (upgradeable to 768 GB) na 21TB HDD na kuona kwamba hiyo list hii ndio ina PC zenye kasi na ubora.

Nadhani ulikuwa unatania.
 
mkuu hebu tupe na source naona mada imekua nzuri sasa nimejaribu kuigoogle processor hio sjapata hata 1
 
mkuu hebu tupe na source naona mada imekua nzuri sasa nimejaribu kuigoogle processor hio sjapata hata 1

Chillblast - The UK's most awarded Custom PC builder - Cheap PCs - Gaming PCs - Workstations Millah nimesoma kwenye hiyo link kuna sehemu wamesema " The Fusion Leviathan takes insane performance to the next level, and
was designed to be the world's
fastest PC using desktop"
It means was only designed to be but haipo practical kwa sasa kuwa fastest PC! Au nimeelewa vibaya??
 
Last edited by a moderator:
First of all there are some point that whatever RAM you increase there is no increase in performance,and to be clear,your 21TB HDD doesnt contribute to any performance,third there is no Xeon processor with 12 cores,i gave you the list of last year because even though the fusion is from this year still it can be beaten by the PC's from last year. That was my point
 
Keyser Söze;6034353 said:
And if you are about to say whar is the most powerful pc around now,then it got to be this beast

Hii itasaidia kwenye rendering maana watu wa animation walikuwa wanahangaika mpaka naskia rendering ya avatar ilibidi ikifanyikie rendering farm HOlland
 
Keyser Söze;6034353 said:
And if you are about to say whar is the most powerful pc around now,then it got to be this beast

Mbona unarudia, si nilishaizungumzia hii kompyuta na jina nimekuwekea hapo juu ninukuu "
Core MC Enterprise Pro, ambayo imetengezwa na Music Computing."
 
Now I am not an Apple fan, never have been and never will. In fact I do not own a single Apple product.

Lakini.

Mtu yeyote anayesema kompyuta iliyopo sasa haiwezi kupitwa labda 2020 hafahamu trends za computing na Moore's Law and it's remnants inavyofanya computing isiwe that easily predictable.

Why, by 2020 people are focusing on targets of a paradigm shift, say quantum computing, that will make the entire concept of RAM as presented here just about medieval!

I real love the commercial, it is brilliant coz things are changing in magnificent speed, you can't predict what will come of the tomorrow
 
Back
Top Bottom