Mbunge wa CCM
JF-Expert Member
- Nov 13, 2009
- 475
- 25
Wapenndwa wanaJF, natumaini mnaendelea vizuri na kazi za ujenzi wa taifa na mijadala mbalimbali iliyopamba moto kila kona ya mchi yetu juu ya masuala muhimu ya mustakabali wa taifa kama sio kabali zinalopigwa taifa kwa sasa.
Nimekuwa nikitafakari sana hotuba ya mwenyekiti wa chama chetu katika kilele cha maadhimisho ya miaka 34 ya uhai wa CCM nikajikuta nsukumwa kuanza mara moja maandalizi ya kushika uongozi wa chama katika ngazi fulanifulani. Kuna kitu kimoja dhahiri kilichoonekana katika hotuba ile; kuwa chama cha CHADEMA huenda ndicho kinaongoza nchi kwani sehemu kubwa ya hotuba ile ilikuwa kujibu namna anavyohusika au kushughulikia ajenda za CHADEMA na sio hali ya siasa wala ilani ya chama! Hapa napenda niwape pongezi za dhati viongozi na wanachama wa CHADEMA kwa kufanikiwa kukiweka chama chao katika nafasi hiyo iliyo na nguvu nchini mwetu. Hakika hicho ni chama ambacho kila mwanachama wake anayo sababu ya kujivuna kukiunga mkono.
Lakini, leo nimeona nigusie kidogo juu ya umuhimu wa kujiandaa kwa uchaguzi mkuu wa chama cha CCM unaotarajiwa kufanyika hapo mwakani, hasa kwa vijana kama mimi.
imekuwa kawaida sasa kusikia watu wakilaumu jinsi viongozi wa chama wasivyowajibika au walivyo na udhaifu wa kiuongozi. lakini sote tunajua kuwa kulaumu pekee sio suluhisho la matatizo yetu. sisi tunaoamini kuwa tuna sifa, uwezo na wajibu wa kuchangia katika maendeleo ya taifa letu ni lazima tujitoe kushiriki katika uongozi wa ngazi zote ndani ya vyama vyetu na katika serikali yetu. hlo litafikiwa ikiwa tutajitokeza kwa wingi kugombea nafasi za kuchaguliwa kila fursa inapojitokeza. kama viongozi wa sasa ni dhaifu na sisi tumeishaona udhaifu wao, basi tusijiweke kando, tujiandae kuchukua nafasi zao na kutoa mchango wetu kwa maendeleo ya taifa letu. CCM au chama kingine chochote kinaweza kuwa dhahifu kama taasisi na pia kinaweza kisiwe dhaifu kama taasisi ila kikawa na viongozi dhaifu.
mimi naamini CCM ni taasisi nzuri na iliyokomaa (mature) ila inaongozwa na watu wenye mapungufu mengi. hivyo kwa jicho langu hilo, tayari nimeanza maandalizi ya kugombea nafasi za kuchaguliwa ndani ya chama katika ngazi mbalimbali zikiwemo za uwakilishi katika halmashauri kuu na kamti kuu ya chama wakati uchaguzi wa mwakani utakapowadia.
kwa uzoefu wangu mdogo katika uchaguzi mkuu wa rais na wabunge uliomalizika october mwaka jana, fursa, maandalizi na dhamira ya dhati ni vitu muhimu sana. wengi wetu huanza harakati za kugombea pale fursa inapotangazwa, kumbe tulipaswaa kuiona fursa mapema kabla haijawadia na kuanza maandalizi ili ikiwadia basi tuwe tayari. hapa nazungumzia maandalizi ya kisaikolojia, rasilimali na mtandao wa kukuunga mkono. tusipuuze au kudharau kitu au mtu. ni vizuri kuanzia sasa anayetaka kugombea ndani ya chama kuanza kujiweka karibu na wanaCCM ambao ndio wapiga kura na kuweka tayari rasilimali watu, fedha na vifaa anavyohitaji kwa kampeni na masuala mazima ya uchaguzi. usidharau kitu hapo, siyo lazima uwe na mamilioni au maVX. hata kama unayo baiskeli na unaamini itakusaidia kukufikisha mahali unapotaka kufika, iweke tayari na spea zake uziandae mapema sio muda unafika unakuta tyubu yake imetiwa viraka vingi hadi haifai tena.
kwa haya mafupi naamini nimetimiza wajinbu wangu kwa vijana wenzangu na wanaCCM wenzangu na nawatakia kila la heri katika maandalizi yenu.
Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki Afrika
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI