fursa za uongozi wa kisiasa ndani ya CCM

fursa za uongozi wa kisiasa ndani ya CCM

Mh.Mbunge itawezekana kushawishi vijana kuingia kwenye chaguzi mbalimbali,lakini kabla ya hapo vijana wa CCM mungetafuta vipoozeo vya kuwapooza wananchi na hasira zao kuhusu ukiritiba,uzandiki na unyampala wa CCM mulionao, huku mukiwaacha makabwela wakijikunq'utakung'uta vumbi ya umaskini na ufukara,je Mh.Ustaarabu uliojitokeza ndani ya CCM ya kuongea uongo kwa kila jambo unadhani vijana wataamini munataka kubadilika kweli au wataona ni janja ya nyani yaani vijana wengi wametambua kwamba mumetumia migongo yao kujipatia ubunge ,kuliko kawaida sasa sijui ni vipi mutaweza kukinga hilo nadhani mukijipanga sawa labda watagombea uongozi ,kwa sasa wengi wanajua nyie kama makanjanja wasema mbofumbofu tuu,Laakini ni kusifu kwa kuchota saikolojia ya watu ili mujue kosa lenu liko wapi
 
Wapenndwa wanaJF, natumaini mnaendelea vizuri na kazi za ujenzi wa taifa na mijadala mbalimbali iliyopamba moto kila kona ya mchi yetu juu ya masuala muhimu ya mustakabali wa taifa kama sio kabali zinalopigwa taifa kwa sasa.

Nimekuwa nikitafakari sana hotuba ya mwenyekiti wa chama chetu katika kilele cha maadhimisho ya miaka 34 ya uhai wa CCM nikajikuta nsukumwa kuanza mara moja maandalizi ya kushika uongozi wa chama katika ngazi fulanifulani. Kuna kitu kimoja dhahiri kilichoonekana katika hotuba ile; kuwa chama cha CHADEMA huenda ndicho kinaongoza nchi kwani sehemu kubwa ya hotuba ile ilikuwa kujibu namna anavyohusika au kushughulikia ajenda za CHADEMA na sio hali ya siasa wala ilani ya chama! Hapa napenda niwape pongezi za dhati viongozi na wanachama wa CHADEMA kwa kufanikiwa kukiweka chama chao katika nafasi hiyo iliyo na nguvu nchini mwetu. Hakika hicho ni chama ambacho kila mwanachama wake anayo sababu ya kujivuna kukiunga mkono.

Lakini, leo nimeona nigusie kidogo juu ya umuhimu wa kujiandaa kwa uchaguzi mkuu wa chama cha CCM unaotarajiwa kufanyika hapo mwakani, hasa kwa vijana kama mimi.

imekuwa kawaida sasa kusikia watu wakilaumu jinsi viongozi wa chama wasivyowajibika au walivyo na udhaifu wa kiuongozi. lakini sote tunajua kuwa kulaumu pekee sio suluhisho la matatizo yetu. sisi tunaoamini kuwa tuna sifa, uwezo na wajibu wa kuchangia katika maendeleo ya taifa letu ni lazima tujitoe kushiriki katika uongozi wa ngazi zote ndani ya vyama vyetu na katika serikali yetu. hlo litafikiwa ikiwa tutajitokeza kwa wingi kugombea nafasi za kuchaguliwa kila fursa inapojitokeza. kama viongozi wa sasa ni dhaifu na sisi tumeishaona udhaifu wao, basi tusijiweke kando, tujiandae kuchukua nafasi zao na kutoa mchango wetu kwa maendeleo ya taifa letu. CCM au chama kingine chochote kinaweza kuwa dhahifu kama taasisi na pia kinaweza kisiwe dhaifu kama taasisi ila kikawa na viongozi dhaifu.

mimi naamini CCM ni taasisi nzuri na iliyokomaa (mature) ila inaongozwa na watu wenye mapungufu mengi. hivyo kwa jicho langu hilo, tayari nimeanza maandalizi ya kugombea nafasi za kuchaguliwa ndani ya chama katika ngazi mbalimbali zikiwemo za uwakilishi katika halmashauri kuu na kamti kuu ya chama wakati uchaguzi wa mwakani utakapowadia.

kwa uzoefu wangu mdogo katika uchaguzi mkuu wa rais na wabunge uliomalizika october mwaka jana, fursa, maandalizi na dhamira ya dhati ni vitu muhimu sana. wengi wetu huanza harakati za kugombea pale fursa inapotangazwa, kumbe tulipaswaa kuiona fursa mapema kabla haijawadia na kuanza maandalizi ili ikiwadia basi tuwe tayari. hapa nazungumzia maandalizi ya kisaikolojia, rasilimali na mtandao wa kukuunga mkono. tusipuuze au kudharau kitu au mtu. ni vizuri kuanzia sasa anayetaka kugombea ndani ya chama kuanza kujiweka karibu na wanaCCM ambao ndio wapiga kura na kuweka tayari rasilimali watu, fedha na vifaa anavyohitaji kwa kampeni na masuala mazima ya uchaguzi. usidharau kitu hapo, siyo lazima uwe na mamilioni au maVX. hata kama unayo baiskeli na unaamini itakusaidia kukufikisha mahali unapotaka kufika, iweke tayari na spea zake uziandae mapema sio muda unafika unakuta tyubu yake imetiwa viraka vingi hadi haifai tena.

kwa haya mafupi naamini nimetimiza wajinbu wangu kwa vijana wenzangu na wanaCCM wenzangu na nawatakia kila la heri katika maandalizi yenu.

Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki Afrika
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

...Ndugu mbunge, wito wako ni wa busara, ila, hujatilia maanani jinsi ambavyo ni vigumu kwa watu wenye kuitakia mema nchi hii kuingia na kupata uongozi ndani ya ccm. Chama hiko ni kama kampuni au mali binafsi ya kundi fulani la watu. Hata Komba huimba - ccm ina wenyewe..... -

...Vijana wengi humu hawana tofauti na kijana mwenzao Nape, watauliza na kukemea hatimaye mtawatupa nje. Nani anataka kujikuta katika nafasi hiyo?

...Kama kweli mko serious, chakachueni kwanza safu za uongozi kuanzia mashinani mpaka taifa, na kuweka watu wenye nia na uwezo wa kujenga nchi, watu waone imekaaje wafanye maamuzi.
 
Mheshimiwa Mbunge hii salaam ni machukizo mbele za Mungu.
Zaidi sana wengine tuna aleji nayo.

Je, bado mnafikiri ni salaam sahihi??
Mnataka chama chenu kidumu katika nini??

duh, kweli watu wamechoka na CCM!
 
Wapenndwa wanaJF, natumaini mnaendelea vizuri na kazi za ujenzi wa taifa na mijadala mbalimbali iliyopamba moto kila kona ya mchi yetu juu ya masuala muhimu ya mustakabali wa taifa kama sio kabali zinalopigwa taifa kwa sasa.

Nimekuwa nikitafakari sana .......................................
kwa haya mafupi naamini nimetimiza wajinbu wangu kwa vijana wenzangu na wanaCCM wenzangu na nawatakia kila la heri katika maandalizi yenu.

Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki Afrika
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

tunashukuru kijana mwenzetu kwa kutuhamasisha, ngoja tutafakari zaidi na nina hakika miongoni mwetu watajitokeza. stay blessed mheshimiwa. usitusahau kwenye vikao vyako dodoma
 
...Ndugu mbunge, wito wako ni wa busara, ila, hujatilia maanani jinsi ambavyo ni vigumu kwa watu wenye kuitakia mema nchi hii kuingia na kupata uongozi ndani ya ccm. Chama hiko ni kama kampuni au mali binafsi ya kundi fulani la watu. Hata Komba huimba - ccm ina wenyewe..... -

...Vijana wengi humu hawana tofauti na kijana mwenzao Nape, watauliza na kukemea hatimaye mtawatupa nje. Nani anataka kujikuta katika nafasi hiyo?

...Kama kweli mko serious, chakachueni kwanza safu za uongozi kuanzia mashinani mpaka taifa, na kuweka watu wenye nia na uwezo wa kujenga nchi, watu waone imekaaje wafanye maamuzi
.

mkuu, natumanini wakati unaadika haya ulikuwa hujaijua vyema dhamira ya mwenyekiti wa CCM na hata hukuwa umenielewa vizuri nilichokisema kwenye rai yangu ya kuwataka vijana tujiandae mapema kushiriki chaguzi mbalimbali ndani ya chama hapo mwakani. mfano wa Nape ulioutoa, nafikiri wewe mwenyewe unajua Nape yuko level gani kwa sasa ndani ya CCM na hilo li nadhihirisha kuwa "kelele" zake zile zilikuwa si bure, alikuwa akisiskika na sasa ameinuliwa!

tukimchukulia Nape kama mfano halisi,bado nasisitiza kuwa kama kijana na raia mzalendo wa taifa, timiza wajibu wako bila kuogopa kukatishwa tamaa. kama nilivyosema kwenye hoja yangu ya msingi CCM ni taasisi mature sana na yenye historia ndefu kwa hiyo lazima itakuwa na tabia zinazoweza kuwakwaza ama kuwakatisha tamaa wengine kama urasimu nk, lakini hayo yasitukwaze ama kutukatisha tamaa, ni suala la wakati tu. tujipange tutimize wajibu wetu na INAWEZEKANA!

wakati unazidi kuyoyoma, hima tujipange kugombea uongozi wa kisiasa ndani ya CCM

MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU IBARIKI AFRIKA
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
 
Back
Top Bottom