Boss Man
JF-Expert Member
- Feb 10, 2022
- 458
- 995
Shukrani mkuu kwa infoBravo wana idadi kubwa ya waombaji hivyo inaweza kukuchukua muda sana kufikiwa batch yako. Mfano walioenda Wiki mbili zilizopita wamefanyiwa usaili mwezi wa 10 mwaka jana. Kwa maelezo ya mzee Mtemvu this coming interview watahitajika karibia watu elfu moja,hao wote hawaendi kwa mkupuo wataenda kwa batch kulingana na uharaka kwa section zinazohitaji man power replenishment.. nadhani kwa hizi kazi za Armarai-Saudi Arabia hazihitaji mtu uwe na haraka hata kama ukifanyiwa usaili. Hivyo ili uwe kwenye nafasi ya kwenda walau kwa wakati heri ukajisajili CIML maana wao hawajulikani sana na hawana namba kubwa ya waombaji.
Naomba kuuliza tena, ivi ukishafanyiwa interview baada ya hapo mnapewa deadline ya kufuatilia vitu kama vibali nk, ili katika kuondoka muweze kuondoka wote kwa pamoja, au hamna deadline ya kufuatilia mambo Kwa maana ya kwamba speed yako ndio itakufanya uwahi kuondoka au kuchelewa kwako ndipo kutakapo kuchelewesha