Fursa za Jangwani

CONTROLA

JF-Expert Member
Sep 15, 2019
4,046
2,000
KUVUSHWA KWA KUBEBWA MGONGONI

Hapa Jana ilikuwa ndio option iliyopo maana kulikuwa hamna option ingine, unapanda mgongoni unavushwa mpaka ng'ambo jamaa anaenda kukuacha kwenye ktuo cha mwendokasi kisha anatafuta wakurudi nae kama yupo kama hamna anarudi peke yake kufuata mwingine.

Bei kwa huduma hii jana ilikua 1500 ILA leo kwakuwa maji hamna ni tope tu bei ni 500 tu unadandia mgongo wa mtu unayeona anakuweza anakuvusha hii ni kwa wale waogopa matope, na slay kwini.

KUVUSHWA KWA TOROLI

Hapa mnajazwa kwenye toroli kama wa 5 kisha jamaa anawavuta mpk ng'ambo ya pili mchezo wa wewe kukanyaga matope unakua hamna so ukishavuka unashuka unaendelea na safari zako, mbele gharama yake 1000 per kichwa so watano = 2500

KUVUSHWA KWA BODA BODA MPKA FIRE

Hapa ma braza meni na vislay kwini wengi walikuwa eneo hili ni kudandia tu boda boda mpaka ng'ambo mnapelekwa mpaka fire boda anawaacha kisha anarudi zake kula vichwa vingine, gharama yake 2000.

KUNAWISHWA MATOPE MIGUU NA VIATU

Hapa kuna wale wabishi kama CONTROLA yaani kubebwa hataki, kupanda toroli hataki, kupanda boda kutoa 2000 roho inamuuma anachoamua sasa ni kuvua viatu kupandisha suruali na kulikanyaga TOPE lile zito mithili ya UJI, mtu unazama ndani ya TOPE kisha ukifika ng'ambo kule mbele utakuta raia wamejipanga na ndoo zao na maji na masponji.

Unampa mguu anakunawisha vizuri na sponji anakusuuuza kisha unampa viatu anakufutia safi kabisa mwisho unampa chake unavaa viatu vyako huyooo unasepa zako na mishe zingine, Gharama ya huduma ya kuoshwa ni 200 sema hapa kwenye 200 kadri muda ulivyoenda mbele kuna wana walikuja haribu fursa ya wenzao wakawa wanaosha miguu wanatangaza sh 100,so ukienda unaoshwa miguu safi unatoa sh 100 mbele.

Bado kuna mtu yupo kakalisha mahali anasema hana kazi hana hata jero ya kula, DAR hamna kazi hamna ajira yupo tu tena na hii mvua ndio kabisa kajifungia ndani anaakwambia daah nitaenda wapi sasa maofisi yamefungwa.

Asee nyie maisha ya leo ukifa maskini ni dhambi tena siku ya mwisho Mungu achome moto vijana wote wasio na ulemavu na wamezeeka maskini achome moto kabisa waive.
 

Ukwaju

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
11,374
2,000
unashangaa nini eti?
kuna watu niliwakaribisha wahamie Jiji la Dodoma (Idodomya) wakanisanifu eti Jangwani hakuna mafuriko, si wamerejea tena Magomeni hawataki Dodoma na ni watumishi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom