Fursa za frontend development

Superpower

JF-Expert Member
Oct 11, 2018
826
912
Jamani habarini za jumapili nashukuru mungu mm kwangu imeenda poa.
Poleni waliokutana na matatizo ya hapa na pale.

Ni hivi kipindi hicho 2018 nilijiingiza katika kujifunza computer programming japo niliacha baada ya kujiunga na chuo na pia kupoteza pc. Sasa Jana nikiwa na simu yangu nilikua nikitafuta app playstore ni kaona Kama Zina nishawishi kurudi Tena katika ulimwengu huu wa programming. Sasa ningependa kuwauliza wadau mliopo katika miji mikubwa kuwa fursa ipoje.
Screenshot_20210704-155347.png
 
Siku zote fursa zipo ikiwa umeiva vizuri, ila sasa mtihani uko hapo pa kuiva, kubali kukeshea haya mavitu ujifunze balaa na pia usigande tu kwenye frontend, piga mzigo wote mpaka backend.
Soko la Afrika halijawa saturated, developers bado wanatafutwa na kulipwa vizuri, ila ni kwa walioiva sio wale wa kupoteza muda kwenye miradi ya watu.
 
Noted
 
Jamani habarini za jumapili nashukuru mungu mm kwangu imeenda poa.
Poleni waliokutana na matatizo ya hapa na pale.

Ni hivi kipindi hicho 2018 nilijiingiza katika kujifunza computer programming japo niliacha baada ya kujiunga na chuo na pia kupoteza pc. Sasa Jana nikiwa na simu yangu nilikua nikitafuta app playstore ni kaona Kama Zina nishawishi kurudi Tena katika ulimwengu huu wa programming. Sasa ningependa kuwauliza wadau mliopo katika miji mikubwa kuwa fursa ipoje.View attachment 1840775
Frontend zipo fursa online tu, offline kibongo bongo you have to fall in love with both front and back end yaani full stack developer.

Hata hizo za online ni chache, bado unahitaji kupiga nyuma na mbele sio mbele tu.
 
sawa mkuu ila online Kuna ushindani wakibabe hatari
 
Siku zote fursa zipo ikiwa umeiva vizuri, ila sasa mtihani uko hapo pa kuiva, kubali kukeshea haya mavitu ujifunze balaa na pia usigande tu kwenye frontend, piga mzigo wote mpaka backend.
Soko la Afrika halijawa saturated, developers bado wanatafutwa na kulipwa vizuri, ila ni kwa walioiva sio wale wa kupoteza muda kwenye miradi ya watu.
Developers wanatengenezaje hela vizuri kwa hapa Tanzania?
 
Kibongo bongo unawezaje kutengeneza mkwanja?

Ukiwa vizuri kama umejichimbia vya kutosha na kujipa uzoefu wala hata hautahitaji kujitangaza, utatafutwa wewe, soko la hapa Afrika Mashariki hatuna developers wa kutosha, miradi inakwama na hugharmu sana kumpata developer. Kunao vijana wengi wanaojiita developers, lakini kama nilivyotaja hapo, lazima ujichimbie na kujiandaa vizuri ili kazi zikufuate.
Ukitengeneza mfumo wa mteja mmoja, mfumo uliokomaa ambao unafanya majukumu yake vizuri na kwamba ulipokeza kwa muda sahihi bila maugomvi, mbona kazi zitakufuata tu, utajikuta unazikatalia baadhi kisa ulivyozongwa......na hapo ndipo mkwanja upo maana bei yako utakua unaitaja mwenyewe....
 
Jamani habarini za jumapili nashukuru mungu mm kwangu imeenda poa.
Poleni waliokutana na matatizo ya hapa na pale.

Ni hivi kipindi hicho 2018 nilijiingiza katika kujifunza computer programming japo niliacha baada ya kujiunga na chuo na pia kupoteza pc. Sasa Jana nikiwa na simu yangu nilikua nikitafuta app playstore ni kaona Kama Zina nishawishi kurudi Tena katika ulimwengu huu wa programming. Sasa ningependa kuwauliza wadau mliopo katika miji mikubwa kuwa fursa ipoje.View attachment 1840775
Soma Sana JavaScript hii iakusaidia Sana katika framework zinazotumia JavaScript kama jQuery,React js,Node js nk ,pia kama una basics za html na css Anza na framework ya bootstrap, kisha soma Ajax na jQuery ukiziweza hizi utakuwa vizuri
 
Soma sana,haribu sana macho,vaa miwani kisha mtafute Ontario atakuajiri kwenye kampuni yake ya 360capital
 
Back
Top Bottom