Fursa za biashara zipo, vijana wa Dar es Salaam ni wazembe tu

hapo kwenye alizeti na asali nimekusoma asali kupata kibali sio inshu sana ila mkaa ni kusumbuana na maliasili kupata kibali ni inshu na kama huna kibali kusafirisha mkaa ni kwa kuficha sana pia bado wale jamaa wakikuta na hata gunia 3 na kibali hauna watakuzingua utadhani wamekukuta na meno ya tembo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi kweli ununue mkaa kutoka dar upeleke morogoro mtoa mada uko serious kweli?

Utoe asali dar upeleke tabora au singida hiyo faida utaipataje sasa.

Mada uliyoleta ni nzuri ila punguza utani mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Tobora ndo inapatikana asali kwa wingi.dar ndo kuna mahitaji makubwa ya mkaa sasa yeye kafanya kinyume chake.mleta mada nae ni comedy sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhan hamjamuelew wakuu jamaa kaja kinyume nyume yaan anamaanisha watoa hizo bidhaa mikoa mingine na kuzileta Dar ndo maana asema watu wasikariri biashara ya nguo n.k bali kuna kutoka pia kivingine.


Sent using Jamii Forums mobile app
Ana tatizo la akili naweza liita wenge. Unaandikaje kama unakimbizwa matokeo anaandika kinyume nyume.
 
Mimi nilipoanza kulima ndipo niliona Dar kuna vijana wazembe sana yaani wamekaa na wanawaza kuuza viatu na nguo tu hakuna mawazo mbadala yaani hawawazi mambo makubwa.

Nimetoka Dar na nimefanikiwa katika kilimo ila Dar wanawaza tu kufungua maduka ya nguo, viatu na simu. Mfano kijana hapo Dar kuna magunia mengi ya mkaa yanaingia kila siku kutoka maeneo mbalimbali ukichukua magunia yako 10 na Canter upeleke Morogoro au Tanga ndani ya siku 3 mkaa umeisha unarudi Dar kufunga mzigo mwingine.

Basi achana na hilo la mkaa, chukua zako asali lita kuanzia 100 weka kwenye vibebeo safi na nembo yako pia, ingia Tabora au Singida uza ndani ya muda mfupi unarudi kufunga mzigo mwingine hiyo kumbuka ni chini ya wiki moja unaweza kuuza lita 100 za asali.

Chukua mafuta ya Alizeti kiasi cha kutosha ingia Mwanza piga biashara usisubiri serikalini ikuambie fursa, fursa ni nyingi sana hapo Dar ila wengi wamekariri fursa aina moja tu.

Kama kuna yeyote atakuwa tayari nitamsaidia alete biashara yake huku nitamsaidia kutafuta masoko. Pia mjaribu kwenye kilimo sio biashara tu.



Sent using Jamii Forums mobile app

Asante ndugu dalali


Sent using IPhone X
 
Back
Top Bottom