Fursa ya kuchimba dhahabu chunya

Orketeemi

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
4,913
12,119
Ndugu zangu salaam.

Baada ya kutafuta sehem ya kufanya kazi ( teaching) bila mafanikio nimeamua kwenda Chunya kuangalia fursa ya kuchimba madini ili kujikwamua kiuchumi.

Kwa wanaofaham mambo haya naomba wanipe ABC za huko ili nipate pa kuanzia maana sijawahi kujishughulisha na masuala ya madini Kwa namna yoyote ile.

Wanajamiiforum wenzangu mliopo huko je mnaushauri gani kwangu?
Niliwahi anzisha thread ya kuomba member yeyote anikopeshe mtaji but sikupata ila Member mmoja anaitwa MKWEPAKODI alisema niende Chunya nikamsaidie kazi hizi za madini but nilipomfuata PM hajanijibu so MKWEPAKODI ukiuona Uzi huu nipe mawasiliano yako.

Samahan Kwa maelezo mengi.
 
Mimi hutakiwi kunifahamu maana ndiyo maana ya kutumia id fake, we njoo tu huku makongolosi au nenda itumbi anza kuomba kazi kwenye malongobesi utanikuta huko ila hutajua kama ni mimi, nitakusaidia kimyakimya kupata kazi ya kutoa felo na baadae ukipata uzoefu utaanza kuchoronga na kuponchi, ukiwa mvumilivu na mwenye bidii shimo likitoa hela hutakosa milioni au zaidi ya mtaji wa biashara unayotaka kuifanya
 
wewe kweli ni MKWEPA KODI..
 
Kazi hiyo unaipenda?au k2akua umekosa mtanji ndio umeamua uende?sikia bro wangu kazi ya madin inahitaji moyo wa dhat si kila mvaajoho jeupe ni daktar wengine ni wauza nyama buchan.

~Swali langu kwako hakuna kaz nyingine iwezayo kukupatia mtaji mpaka ukachekeche au ukachoronge?

Ngoja wataalam waje
 
Back
Top Bottom