Fursa na changamoto za ict kwa serikali na taasisi zake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fursa na changamoto za ict kwa serikali na taasisi zake

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Mtazamaji, Aug 8, 2010.

 1. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #1
  Aug 8, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Wanajamvi
  Nina mjadala, dukuduku,ushauri chanagamoto oghhhh sijui utavyoita wewe soma utoe maoni yako.

  Ni kuhusu ofisi za serikali na taasisi nyingine binafsi kama kweli zinatumia fursa za Teknolojia ya habri na mawasiliona kuboresha utendaji, kutoa huduma bora na kusaidia kufanya maamuzi sahihi.

  Najua taasisi nyingi zinatumia fusra za ICT kurekodi na kurahisisha processing ya mambo fulani.na sana sana zinahusiana na Mishahara, Uhasibu na HR. Mifumo mingi ya ICT ipo katika hali inayoitwa database.

  Ningependa kujua kama Idara ya Polisi ina intgergated IS

  • Inayowawezesha kuwa na acess kufanya analssya ya Data zilizopo kwenye daftari la mpiga kura pindi may be yanapopelekwa mashtaka ya mtu fulani
  • na baadhi ya system za TRA may be ya usajili wa magari.Inayowawezesha wakitaka Kujua Raia XYZ ana miliki magari mangapi.
  Sitashangaa kusikia Polisi wanataka kutengeza system amabazo taarifa zake Zipo kwenye daftari la wapiga kura. Kuna changamoto ya Duplication ya system hasa kwenye serikali. Hii inasababisha matumizi makubwa ya pesa kwa kitu ambacho kimeshafanyiwa kazi na tasisi nyingine ya serikali.

  Changamoto au mfano huu wa Duplication ya system unaweza kuwasadia hata wizara ya ardhi na nyumba. Kupata ramani ya jiji ilivyo sasa ni kazi lakini wakishirikiana na googlemaps. Wizara inaweza kujikuta inatumia kiasi kidogo kuliko kufanya zoezi lao kivyao


  Kuna fusa nyingi kuna changamoto nyingi za ICT je wewe unamawazo gani katika sekta gani?


  Nawasilisha
   
 2. Mpogoro

  Mpogoro JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2010
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 361
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hao kwenye bold hapo....Jeshi la Polisi kwa kweli nafikiri ni moja ya idara za serikali ambazo ziko nyuma sana kwenye ICT.Na nafikiri moja ya sababu kubwa ni ukosefu wa wataalamu.Unaweza kukuta boss ICT katika jeshi ukiacha tu kuwa uwelewo wake kwenye ICT ni mdogo sana,utakuta hana shule ya ICT ya kutosha na muhimu zaidi exposure.

  Unajua haya mambo ya ICT bwana kama huna exposure inakuwa ni tatizo...nafikiri wangefikiria kuchukua vijana na kuwapeleka sehemu nyingine ambazo POLICE imeendelea kwenye technolojia ya habari na mawasiliano ili wajufunze...nina uhakika kama watu wanapata exposure ya kutosha wana nafasi ya kufikiria au kuja na mawazo ya teknolojia raisi ambazo zinaweza kuleta ufanisi katika utendaji wa jeshi la polisi!
   
 3. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kuna uhaba wa vifaa vya maabara kufundishia mashuleni. Wanafunzi wanajikuta wanajifunza practical kwa theory tena kwa theor ya maandishi tu. Je Viongozi wa Mashule yaliyo mjini, walimu na serikali inaweza kutumia fursa zinatotolewa na webiste kama youtube.

  Hata kama kuna uhaba wa vifaa lakini wanafuzi wakionyeshwa process ya mfano fermantation au condesation kwa kutumia malekezo yanayopatikana youtube itawasaidia zaidi kuelewa kuliko malezo yaliyonadikwa na kukarii kwenye daftari tu.

  Maelezo hapa juu ni changamoto kwa wizara ya elimu. inawezekana walimu wengi wa sekondari hawajui fursa hizi amabazo zinaweza kuwasaidia kukabilina na tatizo la uhaba wa vifaa vya kufundishia. Wizara ya elimu inatakiwa kuwaelimisha walimu fursa za ICT wanazoweza kutumia katika kufundisha.

  Nawasilisha
   
 4. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #4
  Aug 10, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Wizara ya Maliasili na utalii pia inaweza kutumia fursa ya googlemap kutangza vivutio vya tanzania . Vile Vile kwangu naona kutangaza Tanzania kwa TOVUTI ni bora zaidi kuliko kuitangza kwenye vituo kama CNN . Tovuti inayoweza kufaa ni yahoo.

  Wakifanya tathmini sahihi ni wateja gani hasa wanawalenga au ni umri gani hasa ya wateja wanalenga kwa matangazo nahakika njia ya TOVUTI inalipa zaidi.
   
 5. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #5
  Aug 10, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Tz kuna fursa nyingi sana za ICT tatizo mfumo mlalo na mgamdo wa sirikali yetu katika kwenda na wakati katika fani hii ndio unawakwamisha wataalamu wengi ambao wanahaha huku na kule kusaka kazi za kuajiriwaa zenye maslahi mazuri badala ya kulitumikia taifa kwa kutoa mchango wa uujuzi wao
   
 6. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #6
  Aug 14, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Serikali ngazi ya wilaya na Mkoa zinatakiwa kuazisha ofisi au vituo vya ICT zilizounganishwa na internet . kwa jina la kitaalamu Computing Center. Ofisi hizi na ofisa wa ofisi hii atawasaidia watumishi mbali mbali kupata curent na latest information kuhusu mambo mbali mbali. Zitawanufaisha walimu kudownload kuhusu mada mbali mbali ambazo shule zao zimekosa vitabu vya kiada juu ya jambo fulani. Vituo hivi vitawanufaisha wafanyakazi wa sekta za afya, wahandisi , maofisa kilimo.Wafanyabiashara na hata wanafuzni

  Ninachomaanisha hapa Serrikali ngazi ya wialya na Mkoa zinatakuwa kuwa na kitu nachoweza kusema ni "Internet-cafe"

  Tayari kuna mikoa ina maktaba ambazo hazina vitabu vinavyokwenda na wakati. Serikali kwa kutumia fursa ya ICT inaweza kubadlisha sehemu za maktaba hizi kuwa computing center inayowajibika kuwapatia na kuwatafutia watu taarifa fulani.

  Fursa nyingine seikali kwa.kutumia gharama ndogokwa vitabu vya makataba inaweza kujiandikisha kwenye taasisi mbali mbali zenye maktaba ya vitabu/ video online. usumbufu wa vitabu kupotea u kubiwa maktaba utaondoka na vile vile kutazifanya maktaba zetu kwenda na wakati .kwa kuongea na taasisi kama ACM Online Books and Courses na nyingine kama hii kunaweza kufufua makataba zetu .

  NB
  Mawazo kama haya inabidi watu waliojairiwa ofisi za mikoa kama watalaama wa ICT wawape wakubwa. Tusiwalaumu wakubwa wakati sisi hatuwi creative. Usimlamu mkubwa wakati hujawai kushika kalamu na kuandika ushauri wowote akaukataa.
   
Loading...