Fursa kwa Developers

blessideal

Member
Jan 19, 2020
5
2
Sio mwandishi mzuri lakini nataka kushare hii na watanzania,

Hii ni moja ya fursa kubwa zinazopatikana duniani kwa sasa,Kutokana na ukuaji wa masoko na mwendelezo wa ukuaji wa teknolojia. Leo hii nawaletea fursa kubwa ambayo inaweza kuwasaidia watu wenye ujuzi kuhusu masuala ya mitandao hasa ktk kudevelop.

Fursa hii inahusisha Program ya kompyuta inayotumiwa na watu wengi duniani katka kufanya masoko ya FOREX Metatrader4 na metatrader5.Unacho hitaji hapa ni ujuzi mdogo kuhusu FOREX na ujuzi mkubwa zaidi katika Kudevelop program endeshi za Computer au simu.

KAMPUNI YA METAQUOTES ambayo ndiyo wamiliki wa Metatrader4 na 5 walianzisha mfumo ambao awali walikua wanauendesha wao kama kampuni mfumo huo ulikua ni kuunda Trading Robots(Experts Advisor), Indicators na baadhi ya vitu mhimu vinavyoweza kutumiwa katika kurahisisha mfumo mzima wa FOREX TRADING. Tools hizo zilikua zikiuzwa huku nyingine zikitolewa bure. Mnamo mwaka 2018 waliruhusu rasmi watu binafsi au makampuni binafsi nje ya kampuni yao kufanya shughuli za uundaji wa tools hizo na kuzipublish katika website yao ya mql5.com

Mimi binafsi nilijiunga katika website hiyo mwezi februari mwaka 2020 nikaona fursa ambayo inaniingizia kipato cha ziada ambacho si kikubwa sana ila ni kikubwa kwa mtu ambae hana kazi na ana ujuzi wa maswala ya kudevelop.

Ili kuwa AUTHOR/Mwandishi katika website hiyo unahitaji Kua na vitambulisho ambavyo utatakiwa kuupload ili wakuverify kama Mwandishi rasmi wa programs katika website hiyo.

Unaweza kuunda tool na ikapendwa na watu hivyo ukawa top seller na ukaamua wewe uuze kwa bei ipi au ukodishe kwa bei ipi mfano unaweza kuunda Expert advisor(Trading Robot) ambae akapendwa na watu wengi duniani na watu wakampa Review ya five star. Tool yako ikipewa 5 stars hiyo ina maana kua imependwa zaidi na mtumiaji.
Screenshot 2020-12-12 133831.jpg

Mfano katika picha yetu hapo juu huyo ni miongoni mwa top developers ambae moja ya tools zake zinafanya vizuri sokon kama unavyoona hapo anapata mpaka Purchases 110 kwa mwezi ambapo ukifanya hesabu ya kawaida ya mwezi mmoja anapata Dollar 5500 kwa mwezi kwa maana kwamba yeye anauza tool yako $50 kwa hiyo $50 mara 110 unapata $5500 ambazo ni mishahara mirefu zaidi kwa wafanya kazi wa TZ.
Screenshot 2020-12-12 134636.jpg

Huyo yeye aliamua kuuza kwa $495 ambapo kwa mwezi ameuza copy 42 Copy 42 ukizidisha kwa $495 unapata karibia 20000 Dollars kwa mwezi.

Sitaki kuonyesha nini nilipata kwa sababu sikuweka muda wangu mwingi ktk website hiyo lakini kwa mwezi hua napata atleast $300-400 si haba kama napata hicho kuliko kukaa na ujuzi na hauutumii.
 
Mimi najua kuhusu Trading tu na sio mzuri sana wa Coding. Je naweza kutengeneza Trading robot kupitia wao?
 
Back
Top Bottom