Fursa kilimo cha mahindi mkoa wa Ruvuma

Fursa kilimo cha mahindi mkoa wa Ruvuma

Hii hapa gharama ya uzalishaji kwa eka moja View attachment 1602150
Kuna vitu hapa bado hujafafanua. Kitaalamu katika hesabu au aina za Gharama Kuna Gharama zinazobadilika kulingana na Uzalishaji (Variable Costs), na kuna zenye hazibadiliki kulingana na Uzalishaji (Fixed Costs).

Mfano hapo usafiri wa pembejeo kwenda shambani ina maana hata nikitaka heka 3 utaongexeka?

Halafu pili Kuna Gharama ambazo kadiri unavyozalisha zaidi ndio zinajifidia na zingine. Labda mbolea mfuko mmoja ni kweli ni heka moja kamili haibaki hata kidogo?

Pia mtu akihitaji heka 10 gharama za usimamizi ni bei hiyo hiyo 100,000/- haipungui?
 
Karibuni wote tuwahudumie kwa huduma mbalimbali za kilimo biashara wasiliana nasi
Kwani mkuu wewe kunilimia Mimi ukapata only 100,000/- na ukilima mwenyewe ukapata 700,000/- kipi bora? Au wewe ndugu yetu hutaki hizo hela? Au Mimi nitoe tu hiyo 690,000/- lakin kilimo kikikataa ni hasara yangu?
 
Kuna vitu hapa bado hujafafanua. Kitaalamu katika hesabu au aina za Gharama Kuna Gharama zinazobadilika kulingana na Uzalishaji (Variable Costs), na kuna zenye hazibadiliki kulingana na Uzalishaji (Fixed Costs).

Mfano hapo usafiri wa pembejeo kwenda shambani ina maana hata nikitaka heka 3 utaongexeka?

Halafu pili Kuna Gharama ambazo kadiri unavyozalisha zaidi ndio zinajifidia na zingine. Labda mbolea mfuko mmoja ni kweli ni heka moja kamili haibaki hata kidogo?

Pia mtu akihitaji heka 10 gharama za usimamizi ni bei hiyo hiyo 100,000/- haipungui?
Hizi ni gharama ya uzalishaji kwa eka moja, maana yake ukiwa na ekari 10 gharama haiwezi kubaki vile vile utazidisha kulingana na ukubwa wa shamba lako, umezungumzia habari ya usafirishaji pembejeo hiyo ni ya ekari moja, ukilima zaidi unazidisha pia maana pembejeo za kusafirisha zinakuwa nyingi, umezungumzia kwa habari ya mbolea kubaki ;ndugu yangu mfuko mmoja kwa eka moja ibaki tena mbolea kwa kilimo cha mahindi ? Kuhusu gharama ya usimamizi inapungua pale ekari zinapokuwa nyingi. Asante.
 
Kwani mkuu wewe kunilimia Mimi ukapata only 100,000/- na ukilima mwenyewe ukapata 700,000/- kipi bora? Au wewe ndugu yetu hutaki hizo hela? Au Mimi nitoe tu hiyo 690,000/- lakin kilimo kikikataa ni hasara yangu?
Kama huhitaji huduma yetu acha tu kuna ambao wanazitumia huduma zetu wanafika kila siku ofisini kwetu na kutupa kazi zao
 
Yaani nitoe pesa nipate hasara halafu nikulipe? Haiingii akilini, huwezi fananisha uwakili na biashara yenu...havifanani.
.
.
Walimieni watu kwa pesa zenu,mkishavuna ndo mchukue faida yenu hapo, otherwise ni utapeli.
Kama watalima kwa pesa zao mazao yatakuwaje yako?hebu fikiri kwanza
 
Nilishawahi kutumia huduma kama hizi na unakuta maelezo matamu , ofisi nzuri , wataalam wapo pale mfano kwenye miradi ya Nyuki na Sungura( Namaingo)......lakini baada tu ya kutoa pesa ya uwekezaji , stori zinabadilika kabisa...sijui huwa ni nini
 
Kwani mkuu wewe kunilimia Mimi ukapata only 100,000/- na ukilima mwenyewe ukapata 700,000/- kipi bora? Au wewe ndugu yetu hutaki hizo hela? Au Mimi nitoe tu hiyo 690,000/- lakin kilimo kikikataa ni hasara yangu?

Ruvuma si ndo kuna Mbinga, na huko Mbinga si ndo kuna Mkako! Mkako si ndo kuna bilionea wa mahindi!

Mlamu, unganisha hizo nukta utaelewa watu wa Ruvuma wana ukarimu wa ajabu!
 
Back
Top Bottom