Fursa katika kilimo cha viazi lishe, tuchangamkieni upesi

KILIMO CHA VIAZI LISHE NI UTAJIRI WA WAZI, TUCHANGAMKIE!

Tukupe nini tena mkulima wetu. Kama soko tumekutafutia tena ni soko la uhakika kabisa. Kazi uliyobaki nayo kwa sasa ni moja tu, kuzalisha viazi. Sehemu ya kuuzia wala hutagangaika. Kinasoru East Africa Tanzania Ltd imefanya kazi kwa niaba yako.

Awali tuliegemea kwenye viazi aina ya Mataya na Jewel pekee, lakini kwa sasa, tunaendelea kuwashawishi wadau wetu ili waweze kuchukua na aina nyingine za viazi lishe ili wakulima wengi zaidi waweze kunufaika. Na kwa hili, kwakweli, tunaelekea kufanikiwa.

Tulikuwa kimya kwa muda mrefu lakini ukimya wetu ulikuwa na majukumu mengi na makubwa nyuma ya pazia. Moja ya jukumu tulilokuwa tukishughulika nalo, ilikuwa ni kutafuta barua ya ithibati kutoka kwenye taasisi inayotambulika ili kuwabebea dhamana wakulima ambao mbegu zao hawakuzitoa kutoka kwenye vyanzo vinavyotambulika.
Tunashukuru hilo tuliweza kulifanikisha na tunawashukuru sana wahusika waliyotusaidia.

Vilevile tulikuwa tunaandaa kanzi data ya wakulima wa viazi lishe na hasa wale wakulima ambao viazi vyao viko tayari kwenda sokoni. Hadi sasa tumefanikiwa kupata ekari zaidi ya 200 za viazi lishe vilivyozalishwa bila mkataba wetu na viko tayari kwenda sokoni. Na mashamba mengine zaidi ya ekari 100 ziko kwenye hatua mbalimbali. Na mashamba yote hayo tumeshayatambua na kuyaingiza kwenye kanzi data yetu.

Na juzi kulikuwa na kikao cha bodi kilichojadiri mambo ya uvunaji, upakiji na usafirishaji. Ni namna gani wakulima wavune, wapaki na wasafirishe viazi vyao kutoka shambani hadi kwenye ghala la kukusanyia viazi kabla ya kuvisafirisha kwenda kwenye soko la kimataifa.

Kwenye suala la uvunaji ilijadiliwa kuwa mkulima anapaswa kuwa makini sana kwani haitakiwi kiazi kichubuliwe kwa namna yoyote ile, lakini vile kiazi hakitakiwi kikatwa. Kiazi kinapochimbwa kinapaswa kitoke na ile kamba yake ya kwenye ncha.

Lakini kwenye upande wa upakiji, mkulima anatakiwa kupaki vizuri kwenye kreti maalum za plastiki au mabox ya mbao na si kwenye mifuko ya viroba ya sandarausi au magunia ya katani kama ilivyozoeleka. Vifaa hivyo ndivyo vitakavyotumika kusafirishia viazi kwenda Dsm kwenye ghala maalum lililoandaliwa kwa ajili ya kukusanyia viazi kabla ya kuvisafirisha kwenda kwenye soko letu la kimataifa.

Sasa hivi tuko kwenye hatua za mwisho mwisho za kukamilisha taratibu zitakazowezesha kuanza kwa zoezi la ununuaji wa viazi kutoka kwa wakulima. Na ikiwa wewe ni mkulima na una viazi ambavyo viko tayari kwenda sokoni, tafadhali tutumie sample kwa njia whatsap, chagua viazi vizuri ambavyo havijaliwa na wadudu na viazi hivyo vitatumika kutoa picha ya jumla ya viazi uliyonao shambani kwako. Katika picha za viazi utakazotutumia utapaswa kuonyesha urefu wa kiazi kwa maana ya sentimeta pamoja na uzito wake kwa maana ya Kilogram.

Kama una aina nyingi ya viazi katika shamba lako, basi utachimba viazi kadhaa kila aina kisha utafuata utaratibu wa upimaji wa kila aina ya viazi kama nilivyoelekeza hapo juu na kisha utapiga picha na kututumia kwa njia ya whatsap. Kiazi tunachokitaka kinatakiwa kiwe na wastani wa uzito angalau kuanzia gram 300 hadi 600 kwa kiazi kimoja.

Hiki ndicho kilimo cha viazi lishe. Unaweza kuona kama unasumbuliwa lakini lengo ni kuona kama vinafaa kwa soko letu la kimataifa. Ni muhimu sana kila mkulima akazingatia kanuni za kilimo bora.

Mkulima ataweza kuuza kilo moja ya viazi vyake kwa TZS 800 haijalishi una mzigo kiasi, soko letu ni kubwa sana ndiyo maana kila siku tunaendelea kuhamasisha wakulima wengi zaidi ili waweze kuingia kwenye fursa hii. Fanya kazi upate hela.

Kwa wakulima wapya na hasa wakulima wanaolima pamoja yaani Block farming, tunaendelea kutoa mikataba kwa ajili ya kuwapa uhakika wa soko, vigezo na masharti kuzingatiwa.

Kinasoru East Africa (T) ina fursa nyingi kwenye kilimo biashara, na kwa sasa fursa zilizo tayari ni Kilimo cha Papai aina ya Malkia, Pilipili kichaa pamoja na viazi lishe vyenyewe.

Fursa ya Maboga Vibuyu au Butternut Squash iko njiani inakuja, kwa sasa unafanyika kwanza utaratibu wa kuagiza mbegu zinazotakiwa kwa ajili ya maboga hayo. Kwahakika, kwenye kilimo chetu hakuna kubeti, ukiweka jitihada utapata kadiri ya jitihada yako. Lazima tumuunge mkono Mheshimiwa Rais wetu kwa kutekeleza kauli mbiu yake ya hapa kazi tu kwa vitendo.

Papai moja lenye wastani wa uzito wa kilo moja linanunuliwa kwaTZS 500 wakati Pilipili Kichaa yenyewe ikiwa mbichi inanunuliwa kwa TZS 2000 kwa kilo moja na ile iliyokaushwa inanunuliwa kwa TZS 4000. Shamba la ekari moja lililolimwa pilipili kichaa linatoa si chini ya tani sita kwa wastani wa mivuno mnne.

Na hii ndiyo habari niliyopanga kuwapa siku ya leo.

Kama kuna lolote la ufafanuzi tafadhali tuwasiliane kwa anuani zetu hapo chini.

Aman Ng'oma
Mkurugenzi Mtendaji
Kinasoru East Africa Tanzania Ltd
Msalato Bible
+255767989713, +255655038210, +255786989713
Email: amanngoma@gmail.com
Dodoma
Tanzania.
 
YES, MAMBO NI WAWA!

Hayo ndiyo maandalizi ya ghala la kukusanyia mazao yetu ya kipaumbele. Viazi lishe, Pilipili kichaa, Maboga Vibuyu na Maboga ya kawaida, Mapapai pamoja na Soya Lishe. Changamkia fursa sasa. Ukiingia mkataba nasi utajiweka kwenye nafasi nzuri ya kuendesha kilimo chenye tija.
 
*YES, MAMBO SASA NI WAWA!*

Leo kwa mara nyingine tena kampuni yetu ya *Kinasoru East Africa (T) Ltd* imerudi kwenu kwa ajili ya kutoa mrejesho wa programu yetu ya masoko kwa mazao ya kipaumbele ambayo ni *Viazi lishe, Pilipili Kichaa, Mpapai, Maboga Vibuyu (Butternut) na Maboga ya Kawaida.* Tuko kwenye hatua za mwisho kabisa za kuanza kutoa masoko hayo kwa wakulima wetu.

Ni habari njema hii, unalima huku ukiwa na uhakika wa masoko.

Aina ya viazi tunavyovihitaji ni kama ilivyo ada ni *Mataya na Jewel,* hatujapata mabadiliko. Wenye mikataba ndiyo tutakaowapa kipaumbele katika masoko yetu kwasababu uzalishaji wao tuliuweka kwenye mpango wetu. Kwahivyo, tutaendelea kuwapa soko kadiri ya makubaliano na kama tutahitaji ziada basi tutachukua kutoka kwa wakulima wengine ambao hatukuingia nao mkataba.

Soko la kimataifa siku zote lina masharti kidogo kwa mazao wanayoyataka. Na kwa kipindi chote tulikuwa tukiendelea kupambana kuhakikisha kuwa kila kipengele cha mkataba wa soko letu tunatimiza. Tunazishukuru taasisi zote zilizosimama nasi kutusaidia kutimiza vigezo na masharti ya soko letu.

Kwa sasa tumekwisha kukamilisha utengenezaji wa mabox maalum kwa ajili ya kusafirishia mazao yetu ya kipaumbele. Na hapa tulipo, tuko kwenye hatua za mwisho kabisa ili tuanze rasmi zoezi letu la ununuzi wa mazao kutoka kwa wakulima.

Tunashukuru pia tumefanikiwa kupata ghala kubwa na la kisasa jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuhifadhia mazao yetu kabla ya kusafirishwa nje kwenye soko letu. Tunajiandaa kufunga "coldrooms” zitakazotuwezesha kulinda ubora wa mazao yetu hasa ukizingatia kuwa mazao yetu mengi ni ya kuharibika haraka kwa mfano Viazi na Mapapai.

Baada ya kufikia hatua hizo, sasa tunaendelea kwa kasi kubwa kutoa mikataba kwa wakulima wote wanaohitaji na wenye uwezo wa kuzalisha kati ya mazao niliyoyaorodhesha hapo juu.

Tuna soko kubwa na la uhakika. Na ni soko endelevu siyo soko la msimu. Ni muhimu mkulima ukachangamkia fursa hii.

Na unapokuja kwa ajili ya mkataba, hakikisha kuwa umekwisha kuandaa shamba lako tayari na ofisini kwetu utalipia mbegu kwa ajili ya shamba lako na baada ya kulipia, hapo hapo utapewa mkataba unaolingana na mbegu ulizolipia. Hatutoi mkabata kwa mkulima ambaye hatutomuuzia mbegu. Lengo letu kubwa, kwanza tuweze kupata mazao bora yanayokidhi soko letu, na pili kumwepusha mkulima kuzalisha mazao kwa kutumia mbegu tusiyoihitaji sisi. Mikataba yote inasainiwa Dar es salaam.

Kinasoru East Africa kwa kushirikiana na wadau wetu tunazo mbegu za kutosha na kwa mazao yote ya kipaumbele.

Bei za kununulia mazao kwa mkulima baada ya kutuletea kwenye ghala letu ni kama ifuatavyo, Viazi lishe kilo moja 800/=, Kipilipili Kichaa kilo moja ikiwa mbichi TZS 2000/= Iliyokaushwa 4000/=, Papai moja la wastani wa Kilo moja TZS 500/= Maboga ya Vibuyu (Buttternut) na Maboga ya kawaida kilo moja ni TZS 2000/=. Hapo kazi ni kwako, tumekudondoshea hiyo fursa.

Kwa watumishi ambao wangependa kunufaika na hii fursa yetu lakini kwa mujibu wa majukumu yao ya kazi, wanakosa muda wa kuweza kusimamia kilimo hiki, tunao utaratibu mzuri kwa ajili yenu ili muweze nanyi kwa upande wenu kunufaika na fursa zetu. Tunatoa huduma ya usimamizi wa mashamba kuanzia ekari 1 hadi 30 kupitia “block farming.”

Tunachokikifanya ni kukupa mchanganuo kamali wa gharama zote zitakazohitajika kwenye mradi utakao uchagua ikiwemo gharama za huduma za usimamizi. Ukiwa na Kinasoru East Africa unaweza kutengeza pesa huku ukitulia zako ofisini. Kazi yetu ni moja tu, tunakupatia Fursa na bei zake na wewe ukabaki na uhuru wa kuchagua fursa unayoitaka kuifanya.

Kwa ajili ya kujenga uelewa wa fursa hizi, timu yetu imejipanga vyema kuendesha mafunzo kwa wakulima na wenye kuhitaji kulima. Iwe mtu binafsi kikundi, taasisi ama Shirika. Tuko tayari utoa huduma.

Ukifanya kazi pesa ipo, ni muhimu kufanya maamuzi bora na sahihi. Kinasoru inazidi kukupa fursa zaidi.

Kwa maelezo ya ziada tafadhali wasiliana nasi kupitia anuani zetu hapo chini.

Aman Ng’oma
Mkurugenzi Mtendaji
Kinasoru East Africa (T) Ltd
Msalato Bible
+255767989713, +255655038210, +255786989713
Email: amanngoma@gmail.com
Dodoma, Tanzania.
 
Asante kwa ufafanuzi, ingawa ni muda kidogo umepita tangu tuulize hiyo clarification Dr!

YES, MAMBO NI WAWA!

Hayo ndiyo maandalizi ya ghala la kukusanyia mazao yetu ya kipaumbele. Viazi lishe, Pilipili kichaa, Maboga Vibuyu na Maboga ya kawaida, Mapapai pamoja na Soya Lishe. Changamkia fursa sasa. Ukiingia mkataba nasi utajiweka kwenye nafasi nzuri ya kuendesha kilimo chenye tija.
Vipi kuhusu Maboga vibuyu. Bado mnashughulika mayo.? Japo ni bandiko la miaka mitatu, iliyopita ila nimeliona leo.
 
Viazi lishe ni aina ya viazi vitamu vyenye mwonekano wa rangi ya njano kwa ndani vikimenywa. Viazi lishe ni biashara mpya katika kilimo biashara ambacho hakijamulikwa vyema na wakulima wetu. Hii ni fursa muhimu na ya kipekee kwa wakulima wanaolenga utajiri kutokana na kilimo. Kwa kifupi huku kuna pesa kuliko kawaida. Ni muhimu tukaichangamkia fursa hii. Kilimo cha viazi lishe ni kama ilivyo kwa viazi vingine vitamu ni rahisi sana ukilinganisha na aina nyingine ya kilimo.

Viazi lishe hutumia muda wa miezi mitatu toka kupandwa hadi kuvunwa. Na kama vikilimwa kwa ajili ya mbegu, vyazi hivyo hutumia miezi miwili tu na vinakuwa tayari kuvunwa na kupelekwa shambani.

Viazi lishe vina beta karotini ambayo ni chanzo muhimu cha vitamini A. Viazi lishe vinatengeneza bidhaa mbalimbali zikiwemo Chipsi, Kripsi pamoja na Unga ambao hutumika kutengenezea bidhaa mbalimbali kama vile Mikate, Keki, Maandazi, chapati, Biskuti na vitafunwa vinginevyo. Kwa kifupi, kwa kutumia viazi lishe, tunaweza kutengeza bedhaa zote ambazo unga wa ngano unatengeneza. Majani ya viazi lishe hutumika kama mboga.

Ekari moja huitaji mbegu elfu 12 na kila mbegu moja tunaiuza kwa tsh 60/= kwa mteja anayechukua mbegu kuanzia elfu 12 na kuendelea lakini chini ya hapo mbegu moja inauzwa kwa tsh 100/=. Tunatoa huduma ya kukusafirishia hadi ulipo kwa kukupostia mzigo kwenye gari na huduma yetu ni bora sana .

Katika ekari moja una uwezo wa kuvuna tani 19 hadi 24 kutegemeana na matunzo yako. Kwa kawaida mbegu moja ya viazi lishe iliyopandwa inatoa kilo 2 za viazi. Kadiri unavyoweka matuta makubwa ndivyo unatakavyovuna viazi vikubwa zaidi. Upandaji wa viazi lishe kati ya shina moja na jingine ni futi moja moja na kati ya tuta moja na tuta jingine pia ni futi moja.

Viazi lishe ni vitamu sana. Vina unga wa kutosha na mwonekano wake huwavutia wateja wengi sokoni ukilininganisha na viazi vitamu vya kawaidi. Lakini vilevile viazi hivi vimepewa chapuo kubwa na wenzetu wataalam wa lishe kwa ajili kuboresha afya ya watoto, akina mama wajawazito pamoja na wazee.

Kilo moja ya viazi lishe inakwenda kwa tsh 1000/= sokoni. Na shina moja linatoa wastani wa kilo mbili na ekari moja ina mashina 12,000. Kwa haraka haraka ekari moja ikiwa utafuata na kuzingatia masharti yote muhimu utaweza kuvuna tani hadi 24. Sasa wewe rudisha nyuma hiyo hesabu, fanya utavuna tani 20 tu ambayo ni sawa na kilogramu 20,000. Je wajua kwa hiyo ekari moja utaweza kutengeneza tsh ngapi? Hapa utachukua 1000/= X 20,000KGS itakuwa sawasawa na tsh. 20 milioni. Hebu niambie kuna biashara gani unaweza kufanya kwa miezi michache tu ukaibuka na kiwango hicho cha pesa. Fursa ni nyingi mtaani tuzichangamkieni.

Hapo hatujaongealea biashara ya mbegu za viazi hivyo. Navyo ni hela pia. Ukiamua kuzalisha mbegu za viazi lishe kama nilivyosema hapo awali vyenyewe huchukua miezi miwili tu hadi kuvunwa. Katika ekari moja inatoa mbegu laki moja 1,046,000 na kila mbegu kwa bei inauzwa kwa tsh 30/= na sokoni kwa wale wateja wakubwa kabisa wanaochukua kuanzia mbegu 360,000 zinauzwa kwa tsh 50/=. Sasa ukichukua mbegu 1,046,000 x 30/= mkulima ataweza kupata jumla ya tsh 31,380,000/= . Je kuna biashara yeyote unayoweza kufananisha na kilimo hiki cha uzalishaji wa mbegu na viazi vyake?

Ni muhimu kukumbuka viazi ni miongoni mwa mazao yanayostahimili sana ukame hivyo vinamuhakikishia mkulima chakula cha uhakika. Vilevile kilimo hiki cha viazi lishe, hakina usumbufu kama ilivyo kwa aina nyingine ya kilimo. Ukipitisha trakta likavuruga ardhi, ukapanda mbegu kitakachofuata ni palizi tu. Kwa baadhi ya maeneo huhitaji mbolea lakini kuna baadhi ya maeneo mengine kama vile Morogoro hayahitaji hata mbolea, ukivichomeka tu basi utasubiri palizi kisha kuvuna.

Viazi lishe hustawi katika maeneo mengi ya nchi yetu lakini hustawi zaidi katika maeneo ya joto kwa mfano maeneo yote ya mikoa ya Pwani na Morogoro, maeneo yote ya Kanda ya ziwa na mikoa ya magharibi kama vile Tabora na Kigoma, Mikoa ya Kanda ya kati Singida na Dodoma pamoja na mikoa ya nyanda za juu kusini hasa Ruvuma, Rukwa na Katavi. Kwahiyo wakulima waliyo kwenye maeneo hayo wana fursa zaidi ya kuendesha kilimo hiki cha viazi lishe pamoja na mbegu zake.

Hii ndiyo fursa niliyoona niwashirikishe siku ya leo.
Kwa mahitaji yako ya Viazi lishe au Mbegu zake tafadhali wasiliana nami

Aman Ng'oma
Mkurugenzi Mtendaji
Kinasoru East Africa Tanzania Ltd
0767989713/0786989713
amanngoma@gmail.com
Dodoma.
View attachment 486804 View attachment 486805 View attachment 486806 View attachment 486807 View attachment 486810 View attachment 486811
Kilimo cha kwenye keyboard kutoka kwa motivational speaker!😁😁😂😂😂
 
Vipi wakulima wa viazi lishe,Kuna MTU una ushuhuda wa hii Biashara......!
Nimejiuliza hao jamaa wanaotangaza biashara ya kilimo je wao wamalima?
Je wanaweza nunua viazi vyote vya wakulima maana ardhi ya TZ inakubali viazi balaa.
Mimi nikushsuri kama unataka kulima viazi jitagutie soko mwenyewe, ongeza thamani viazi vyako kwa kusaga unga na utengeneze unga wa lishe.
Viziia msimu wa mpaka mwezi wa tatu maana sokoni huwa hakuna viazii vingi utapiga hela.
 
Nimejiuliza hao jamaa wanaotangaza biashara ya kilimo je wao wamalima?
Je wanaweza nunua viazi vyote vya wakulima maana ardhi ya TZ inakubali viazi balaa.
Mimi nikushsuri kama unataka kulima viazi jitagutie soko mwenyewe, ongeza thamani viazi vyako kwa kusaga unga na utengeneze unga wa lishe.
Viziia msimu wa mpaka mwezi wa tatu maana sokoni huwa hakuna viazii vingi utapiga hela.
Mbegu inapatikana wapi
 
Back
Top Bottom