Fursa Hii Hapa: Naomba Ushauri Wenu

Fursa Hii Hapa: Naomba Ushauri Wenu

Amba Samedi

Senior Member
Joined
Apr 5, 2024
Posts
193
Reaction score
326
Habari wanaJF,
Natumaini mnaendelea vizuri. Nimerudi tena (na kasi yangu imenipa zawadi ya "can't stop" ya JF). Asante sana Maxcence and the team.

Juzi kati nilipigiwa simu na mdau mmoja. Akaniambia kuwa anataka nimsaidie mfumo wa SMS wa kumsapoti wakati wa harusi yake. Request nyepesi lakini nikaona mbali kidogo.

Of course kwanza nikapitia nyuzi mbalimbali hapa JF, nkaona kuwa watu wanaprovide huduma kama hiyo. Lakini nkataka kutanua wigo kidogo.

Chachu ya Mawazo
Nilipigiwa simu na jamaa mmoja akawa anataka mfumo wa dukani kwake. Niliandika uzi mrefu hapa namna nilivyotatua shida yake. Aliniomba namna ya kutuma SMS, tukafikia kutengeneza mfumo wa kurahisisha kazi.

Niliona suala hili likiwa la kujirudia rudia katika baadhi za biashara nilizointeract nazo: wanataka SMS au mawasiliano, lakini tunaishia kutengeneza mfumo wa wateja na hulka zao kwanza.

Nikaconclude: Mafanikio = Mfumo (Wateja) + Mrefeji wa Mawasiliano (SMS, Email, WA nk)

Ombi la Rafiki Yangu
Rafiki yangu anataka kufunga harusi kama nlivyotangulia kusema. Kawaida, watu hufanya hivi:
  • Wanaorodhesha watu kwenye karatasi
  • Wanahamisha kwenye excel (kwa wenye uwezo huo)
  • Wanafuatilia huku waki update mmoja mmoja.
  • Zoezi linaendelea kwa kipindi kizima cha kufanya mipango ya harusi.
Lakini baada ya kuteseka wakati nafunga ya kwangu, nkaona kuwa tusiishie tu kutuma message, bali tuwe na mfumo kamili ambao utasaidia kuendesha shughuli nzima, ikiwamo:
  1. Kutengeneza safu ya kamati. Wote wawe registered na namba zao za simu
  2. Kuunda mkeka wa watoaji. Hii ni pamoja na jina, status, na mchango alioahidi.
  3. Kuandaa calendar nzima ya matukio na kuyatupia, pamoja na tarehe zote za vikao, ili kutoa update kila kukicha
  4. Kupokea michango na kuupdate. Kila mchango unapopatikana, kuwe na record sahihi, na shukrani kwa aliyetoa kwa njia ya SMS. Hii ni pamoja na mnyabulisho wa amount aliyotoa, kilichobaki (kwa kile alichoahidi), na tarehe za deadline. Updates ziwaendee mhasibu na mwenye shughuli wakati huo kumpa update ya hali halisi ya michango.
  5. Kila siku/wiki, kuwe na updates za email ambazo zitaruka kwa wanakamati wote kuwapa mwenendo wa shughuli, kilichofanyika, kilichobaki, hali ya michango, nk
  6. Mfumo utume autoreminders kwa wanaodaiwa michango. pamoja na kwamba bw. arusi atapiga simu, lakini system imsapoti katika kukumbushia.
Hivi ni baadhi ya vitu nilivyoviwaza.

Ushauri Wenu
Nimeleta hili wazo hapa ili kujua kama kitu kama hiki kinafaa kwenda sokoni. Nawaza hapa, ili nisijetumia nguvu kubwa kuua sisimizi kutumia risasi au mnati. Je, service kama hii wewe ungepewa ungenunua? Kwa gharama ipi?

Na endapo kuna ushauri au jamba ambalo halijaeleweka, niko hapa kuelezea.

Signed,
Amba Jnr.
 
Mfumo wa sms tu unachaji bei gani?
Inategemea. Bei zinaanzia 10,000 kwa mwezi. Kuna premium SMS (ya SMS moja moja kuanzia 25. hii inakujaga na jina km TAMISEMI), na lokoSMS ambayo inatumia simu na line yako lakini kwa njia ya kuwatumia watu wengi kwa mpigo.

Kwa taarifa zaidi nicheki whatsapp +255742308110
 
Back
Top Bottom